MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, October 19, 2019

MADHABAHU


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila


14TH October 2019


Hesabu 23:1-23

Hakuna wa kukulaani kama Mungu hajakulaani, hakuna wa kukulogha kama Mungu hakuruhusu ulogwe na yeyote leo aliyeinuka juu ya maisha yako anaanguka mbele yako.

Wapo waliowaza kama wanadamu walipoona unastawi, wakafikiri kama wanadamu kuizima ndoto yako. WANAFIKIRI WATAZUIA NJIA YAKO. LAKINI ASHUKURIWE MUNGU AMBAYE ANAKWENDA KUKUINUA NA KUKUPIGANIA.

Balaki alidhani kwamba anaweza kujenga madhabahu na kulaani wana wa Israeli lakini Mungu hazuiliwi na madhabahu ya aina yeyote.

Wana wa Israeli walikuwa kwenye maono yao ya kwenda Kanaani wala hawakujua kile ambacho kilikuwa kinaendelea kwenye ulimwengu wa Roho. Kumbe walikuwepo watu ambao wameshajenga madhabahu na kutoa sadaka kwaajili ya kurudisha ndoto zao nyuma.

Unapomtumainia Mungu utaona maajabu na adui zako watamuona Mungu wako. Balaki alijua mtu aliyelaaniwa hawezi kuwa na nguvu tena wala kusonga mbele na maono. Ndiyo maana Balaki alimuita Balaamu ili kulaani wana wa Israeli na alipokuwa kwenye madhabahu badala ya kuwalaani akawabariki. Na alipoendelea kuwabariki Balaki akamwambia ni heri isiwabariki na mimi usinibariki. USIOGOPE WALIO MBELE YAKO MUNGU NI ZAIDI YA HAO.

Mungu uwaacha maadui zako wajiandae na wakusogelee lakini wanapokusogelea Mungu anawaangusha chini hao adui zako ili wajue kwamba unaye Mungu wa kweli.

Mungu akikupa utiisho hata usiowategemea wataanguka mbele zako.

Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.

Wale waliokuchafua unakuwa na Amani tena. Wao wamepanga kama wanadamu lakini leo nakutamkia Mungu hakuinue tena ukang'ae kwa Damu ya Yesu. Kawaida ya Mungu wetu wakichafua yeye anasafisha kwa hivvyo kwa kadri ya wingi wa maneno yao ya kukuchafua ndivyo Mungu anakupandisha kiwango. Wakifunga njia moja zinafunguka saba, wakianza kukushutumu ndivyo Mungu anakutetea. Mithali 6:31. Madhabahu waliojenga badala ya kukulaani wewe itakutetea wewe kwa jina la Yesu.

Mungu akiwa ndani yako usifadhaike wala kuogopa, jambo linaloonekana kubwa kwako litakuwa dogo Mwanzo 15:1. Wana wa Israeli wakiwa kwenye safari zao huku watu wameandaa mabaya lakini wao walikuwa wanasonga mbele. ( HESABU 33:1)Na leo Mungu hakusaidie usonge mbele.

Ndani ya siku saba zilizobaki kuna watu wana ushuhuda tena.

Wanapokupeleka ili uangamie ndipo unakutana na Mungu wako. Usiwaze maadui walio kwenye njia bali waza njia ya Bwana anayokuwazia na utafika salama katika jina la Yesu. YEREMIA 29:11 Mungu aliwajua wana wa Israeli na aliwajua maadui zao lakini aliwapitisha kwenye ile njia. Mungu anajuwa wakati wa maadui zako kuangamia na siku yako ya kuheshimika.

Usiwaze vita waza ushindi wako. Usiwaze maadui zako bali Mungu wako. Maadui ni wengi Zaidi ya nywele za kichwa chako lakini hawatakuondoa kwenye maono yako Zaburi 69:4. Usipoteze muda kuwaza wanaokuchukia poteza muda kuboresha maono yako. Wanaokuchukia hawakuondolei chochote, wao wanakuona haufai lakini Mungu anayekuona unafaa anakuwazia mema. Maadui zako wengekuwa wanatoa wao Baraka usingepata lakini ashukuriwe Mungu iliyetubariki.  Waefeso 1:3

Wanajitahidi kuzuia kwa unganga wao na uchawi lakini hashukuriwe Mungu aliyeondo uchawi.

Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!

Wamewaza kama wao walipoona Baraka zako na wakadhani wanaweza kukuzima kwa mahirizi yao lakini Mungu amesema HAKIKA HAPANA UCHAWI. Kuna wakati mambo yanatokea kwenye maisha yako ambayo Mungu anaruhusu yatokee ili kuwe na ushuhuda. Usiogope kwa hali unayopitia Mungu anakutengenezea ushuhuda.

Mungu aliyepindua madhabahu ya Balaamu leo atapindua madhabahu ya adui zako.

Usiwaze ya misri waza leo ya kanaani. Usiwaze ya jana kwanini Mungu hakukutetea waza ya leo Mungu anakutetea. Walikufunga na uchawi wao lakini ashukuriwe Mungu leo anakata uchawi wao. Na leo tunakata uchawi wa Bibi, uchawi wa jirani yako kwa jina la Yesu.

Mungu anasema hakuna uchawi kwasababu hakuna madhabahu yeyote itakayotaja jina lako kubaki salama. Na leo watakapo peleka jina lako au sura yako au biashara yako hiyo madhabahu ipasuke vipande vipande.


Omba .... sasa kwa jina la Yesu kwasababu hakuna uchawi tena juu yako..........

No comments: