MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, May 26, 2020

KUFANYA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU

26th May 2020


 

Isaya 55:6-13 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. 12 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. 13 Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

 

Neno kutafuta maana yake ni kitu ambacho kipo lakini unahitaji ukiendee mahali kilipo. Mungu yupo lakini lazima umuendee usipomtafuta Mungu hauwezi kumuona yeye.

 

Si wote wanaweza kumtafuta Mungu na kumuona kuna vigezo vya kumtafuta Mungu na kumuona. Wote tunatamnai utajiri lakini kuna vigezo vya kutafuta namna ambavyo unatafuta ndivyo umasikini unakimbia. Wote tunaweza kuwa sehemu moja kwa maana ya kumtafuta Mungu lakini kuna vigezo vya kumtafuta Mungu.

 

Kama Mungu anatafutwa maana yake kuna bidii katika kumtafuta yeye, unaweza kukaa kanisani lakini usimuone Mungu.

 

Ufanye nini ili sasa umfikie Mungu?

 

Biblia inasema mtu mbaya na aahe njia zake, kumbe katika kumtafuta Mungu kuna watu wabaya na wazuri na wote wanamuita Mungu na kumtafuta Mungu. Mtu mbaya hata akimuendea Mungu na kumtafuta hawezi kumuona. Ukiwa mtu mbaya hauwezi kumuita Mungu akaitika. Hauwezi kumkaribia Mungu akajifunua kwako.

 

Tungekuwa kwenye mfumo wa kawaida wa kutafuta fedha tungesema mtu mwenye matumizi mabaya ya fedha hawezi kupata utajiri. Mtu anayeheshimu kanuni za biashara au kazi atafanikiwa. Haya tungekuwa kwenye maisha ya kawaida tungesema hivyo.

Kwa hivyo tunamtafuta Mungu tukiwa na ubaya na tunatumaini kumuona Mungu. Unachokitafuta ni Kitakatifu tena cha dhamani na kwa kuwa ni Kitakatifu kinahitaji Utakatifu wa watu ambao wametoka kwenye njia mbaya na kuacha hizo njia. Watu wabaya wakipaza sauti zao inakuwa ni makelele mbele za Mungu.

 

Mtu mbaya hata mawazo yake yanakuwa mabaya na Mungu hawezi kusikiliza mawazo mabaya ndiyo maana maandiko yanasema “aonavyo mtu nafsi mwake ndivyo alivyo” Mithali 23:7. Usiwe na hatua ya kuanza kumsogelea Mungu wakati hauna sifa za kumsogelea Mungu. Mungu anapokuita kuna vigezo vya kumfanya yeye hakupokee. Kigezo cha kwanza ni kuacha njia mbaya kwa maana ya dhambi na kumrudia Mungu wako.

Ili Mungu akufanikishe lazima aachilie mawazo yake na hawezi kuyaachilia ili wewe uyapokee pasipo kumuona Mungu au kuwa pamoja na Mungu. Mungu anayo mawazo yake na shetani anayo pia mawazo yake. Ukiwa kwenye njia mbaya maana yake unaeneshwa na mawazo ya shetani.

 

Mawazo ya Mungu juu ya Adamu na Eva yalikuwa mazuri na wakapokea wazo la Nyoka ambaye alikuwa na mawazo yake. Adamu kwasababu ya kupokea wazo la shetani alishindwa kumsogelea MUNGU na kujiona yuko uchi. Ukiona aibu zinaufuata kuna uadui na kuna wazo la Mungu ambalo umeliacha. Adamu aliona yuko uchi na alianza kuangaika kujisitiri.

 

Mungu anapotoka kwenye maisha yako kuna uhitaji ambao unatokea. Shetani anapoingia mahali lazima aachilie aibu, anguko, vita na migogoro maana toka mbinguni anatolewa alitolewa kwa migogoro (Ufunuo 12:7-11). Asili yake shetani ni ugomvi asili yake ni migogoro na mabaya. Alikuwa mbinguni shetani akimsifu Mungu lakini wazo lilipomjia mabaya yakaanzia hapo.

 

Mwanadamu anaishi kwenye ufunuo kwa maana kuna wazo linakuja kwamba ufanye kile au hiki, kuna wazo linakuja kwamba Fulani anakuchukia na unaanza kulifanyia kazi wazo hilo.

 

Vita ya shetani anakuzuia hili usimpate Yesu ili ubaki kwenye ahadi ambazo hazitimii. Kamwe usikubali mawazo ya shetani ya kumondoa Yesu ndani yako.

 

Njia za Mungu si kama wanadamu, wanaposhindwa kuvuka siyo kwamba Mungu ameshindwa. Tunamuona Daudi ambaye waisraeli walikuwa wakipigana na Goliathi, lakini njia ya Mungu ya kuwashindia haikuwa silaha kama za mikuki na mishale. Goliathi alikuwa na silaha zote lakini hakuwa na jiwe tu ambalo Daudi alilitumia. Hata kama Daudi angemuonyesha kwamba nakuua kwa jiwe asingelipata kwasababu hakuwa nalo kwa wakati ule.

 

Kuna mahali unavuka leo na Bwana anakupeleka kwasababu njia zake hazichunguziki haleluyaaaa. …….

 

Tunamuona Esta ambaye walikuwa na wayahudi, adui alijua kwamba Mordekai anaishia njiani nah ana njia ya kuingia kwa mfalme kwasababu kuna sharia tayari ilipita ya kumaliza wayahudi. Njia ya Mungu ya kuokokoa si njia ya wanadamu. Ndiyo maana Esta aliwaambia wayahudi wawe na siku tatu za kumtafuta Bwana ili waende kinyume na utaratibu.

 

Sikiliza nikuambie madamu umempata Mungu utakwenda kinyume na sharia zao, adui zako hautawaona tena kwasababu utakwenda kinyuma na taratibu zao.

Waamini wakimshangilia Bwana katika ibada.


 

Walimtafuta Bwana siku tatu na Mungu hauwezi kumpangia utaratibu ukiwa na Mungu yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho ndiyo maana kila mahali yeye yupo.

 

Kila mahali nilikuambia yupo kwa madaktari anaitwa tabibu wa kweli kwenye mwamba yupo anaitwa jiwe lililokataliwa, kwa wayama anaitwa simba wa kabila la Yuda akinguruma wachawi wanaokoka, akinguruma watesi wako wanakimbia. Kwa wanasheria yeye ni wakili wetu, kwa majaji yeye ndiye jaji mkuu na hakimu wa kweli. Kwa wapishi yeye ni mpishi wa kweli alipikia watu elfu tano wakiwa wanaume tu. Kwa walimu yeye ni mwalimu mkuu. Kwenye njia yeye ni njia ya kweli.

No comments: