MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, March 24, 2021

MAOMBI YA KULIVUA VAZI LA KIPEPO ULILOVIKWA NA SHETANI.

 MAOMBI YA KULIVUA VAZI LA KIPEPO ULILOVIKWA NA SHETANI.


Na Pastor Daniel Lema


Neno vazi lina maana ya kitu chenye kuvaliwa. Wakati mwingine vazi ni utambulisho wa mwilini na Rohoni. Yesu atakapo kaa kwenye kiti cha Rehema ni tofauti na atakapokaa kwenye kiti cha hukumu. Kila cheo katika ulimwengu wa Roho kina vazi(utambulisho) Lipo vazi la Mwanajeshi pia hutambulishwa kwa njia ya vazi na vazi Hilo linakuwa na cheo Bwana Yesu asifiwe! Katika ulimwengu yapo mavazi yanayokutambulisha na yapo

kukuruusu kuingia sehemu flani. Kwa hivyo sababu ya vazi lake tayari kila mtu anajua wajibu wake. Ukienda hotel wale wahudumu huwa wana vazi maalumu. Linawatambulisha. Na vazi Hilo linamfanya atumwe Na mteja! Au amuhudumie mteja bila kuulizwa maswali. Kanisani vazi la mhudumu linamfanya aweze kukusanya sadaka na watu wasiwe na wasiwasi maana wanajua kazi ya lile vazi.

KWA IYO VAZI LINAWAKILISHA KAZI.

VAZI LA HAKIMU LINAWAKILISHA HUKUMU. 

VAZI LA DR. LINAWAKILISHA HUDUMA YA AFYA, 

VAZI YA WAKILI LINAWAKILISHA UTETEZI, 

VAZI LA MWANAFUNZI LINAWAKILISHA KUJIFUNZA, 

VAZI LA SPIKA WA TANZANIA LINAWAKILISHA UONGOZI WA KITI BUNGENI, 

VAZI LA JESHI LINAWAKILISHA ULINZI NA MPIGANAJI WA VITA. 

LIPO VAZI LA NESI LINAWAKILISHA HUDUMA YA AFYA, kama jinsi ilivyo Katika ulimwengu wa Mwili ndivyo ilivyo Katika ulimwengu wa Roho. Vazi Ni symbol ya kazi. Au ni Alama ya kazi. Watu wanaokuona watakutreat kutokana vazi lako. Kibiblia kuna aina mbili za Neno vazi


1. Vazi linaloonekana mfano Mwanzo 3:21 '' BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika."


2. Vazi la kiroho ambalo halionekani kwa macho ya kawaida ila matokeo ya vazi hilo huonekana, mfano Warumi 13:14 '' Bali mvaeni Bwana YESU KRISTO, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake."


Ukiangalia tafasiri ya BHN juu ya andiko hilo Biblia inasema kwamba ‘’Bwana YESU awe vazi lenu’’


Kwa jinsi gani tumvae KRISTO?


Wagalatia 3:27 inajibu kwa kusema ‘’Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO.‘’


Tena 1 Petro 1 :15 inajibu kwa kusema ‘’ bali kama yeye(YESU) aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;‘’


Vazi la KRISTO ni vazi jema sana.


Lakini pia kuna vazi baya kiroho ambalo mtu anaweza akavikwa kutoka ulimwengu wa roho wa giza, na ndilo linahitajika kutoka kwako kwa jina la Yesu ili uvikwe vazi jipya. 


Ni damu YESU KRISTO pekee inayoweza kuliondoa vazi hilo la giza kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO.


Tutashinda leo kwa jina la YESU KRISTO kama ambavyo ROHO MTAKATIFU ametupa ufunuo huu muhimu wa maombi ya siku 21 ndani ya POWER OF GOD FIRE CHURCH CHINI YA BABA YETU BISHOP DANKTON RUDOVICK RWEIKILA. 


Kwa hiyo kipepo wachawi au majini wanaweza kumvika mtu vazi la kipepo ili limtese, unaweza kuvikwa vazi la kukataliwa, kuumwa umwa kila mara, kudharauliwa, kuwa mtu wa hofu tu , kufuatiliwa na majini kila siku, umasikini, mateso n.k


Nataka tuangalie vipengele vifuatavyo, 


1. Wenye dhambi wasiotubu kwa Bwana YESU watakwenda jehanamu kwa sababu kiroho watu hao wamevaa vazi la kigeni yaani vazi wasilotakiwa kulivaa wanadamu walioumbwa na MUNGU.


Vazi hilo la kigeni ni dhambi. 


Sefania 1:8 '' Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya Bwana, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.''


Vazi hilo hakuna anayemvalisha mtu yeyote ila ni mtu mwenyewe kwa matendo yake ya dhambi anajivalisha, kumpokea YESU na kutubu tu ndio njia pekee ya kulivua vazi hilo la kigeni liitwalo dhambi ambalo halitakiwi kuwako katika wanadamu wanaoutaka uzima wa milele. Ndugu livue vazi liitwalo dhambi ili lisiwe kamwe kwenye maisha yako maana hilo ni vazi la kigeni yaani ni vazi baya kwako.


2. Wokovu wa YESU KRISTO ni vazi wanalotakiwa kulivaa watu wote duniani. 


Isaya 61:10 '' Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika MUNGU wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.''.


Ndugu hakikisha unalivaa vazi hili muhimu sana. Usiuzoelee wokovu kabisa maana ni hatari mno walokole tumezoea hili vazi na kulifanya si kitu. 


Zaburi 132:16 '' Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia.''



3. Maisha ya haki katika KRISTO YESU ni vazi analotakiwa kulivaa kila mtu.


Ayubu 29:14 '' Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.''




4. Utakatifu katika KRISTO ni vazi la wateule wa MUNGU. 


Ufunuo 3:5-6 '' Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. ''. Ndugu hakikisha unalivaa vazi hilo bila kulivua hata siku moja. Wakolosai 3:10 ''mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. ''




5. Wito/Huduma ni vazi kwenye ulimwengu wa kiroho.


2 Wafalme 2:9-15 ''...... Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani.14 Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. .......'''


Kama MUNGU amekupa wito au huduma kwa ajili ya kazi yake katika Kanisa la MUNGU hakikisha unatimiza wito wako na huduma yako. 


Usikatae kufanya kazi ya MUNGU. Usilivue vazi hilo wanalovaliswa na MUNGU wateule wake waliookoka.


6. Nguvu za ROHO MTAKATIFU ni vazi la wateule wa KRISTO. 


Luka 24:49 ''Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.''


7. Vazi safi la utakaso wa damu ya YESU KRISTO.


Zakaria 3:4 '' Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi''.


Ndugu hakikisha unamkimbilia Bwana YESU kwa ajili ya kutubu na baada ya kutubu atakuvika vazi jipya la utakaso, hivyo utaanza kuwa mtoto wa MUNGU na vazi la kwanza la dhambi malaika wataliondoa kwako maana sasa utakuwa safi mbele za MUNGU.


Katika kitabu cha Ayubu tunafahamu kwamba kwa kibali cha MUNGU na kwa sababu Maalumu MUNGU alimpa kibali shetani amshambulie Ayubu(Hiyo ilikuwa kwa Ayubu tu hivyo usijenge Imani yako kwamba unateseka kwa sababu MUNGU ametaka uteseke) Katika Maandiko anayemshambulia Ayubu ni shetani na shetani alimshambulia Ayubu kwa magonjwa mabaya . Nataka ujifunze kitu kwamba Ugonjwa unaopigana nao kipepo ni vazi.


Ayubu 7:5-6 ''Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini. '' Ayubu anakiri kwamba amevikwa vazi la ugonjwa.


Kuna watu wamevikwa mavazi machafu. 


Zakaria 3:3 ''Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.''


Kuna watu watu wamevikwa vazi la aibu,kudharauliwa, kuonewa, magonjwa, madeni, umasikini,ajali, matatizo na kila uonevu.


Kuna watu kila akijaribu kuomba kazi hapati lakini wengine wanajaribu tu na kupata kazi, ndugu livue vazi la kipepo ulilovalishwa kwa kutamkiwa kichawi na mawakala wa shetani.


Kuna waliovikwa kichawi vazi la laana, kukataliwa, kuabishwa na kufeli katika maisha.


Kuna watu wamevikwa vazi la kipepo la kuwafanya wawe chini tu.


Zaburi 109:18-29 ''Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake. Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima.''


Vua mavazi ya kipepo, yavue kwa damu ya YESU KRISTO.


Pia katika maisha yako yote usikubali tena usikubali haswaa vazi lako la Wokovu likachakaa, 


Ufunuo 7:14 ''Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.''


Hakikisha unalifua kila siku vazi lako la Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana. Fua vazi lako la Wokovu kwa wewe kuishi maisha matakatifu kila siku, Kufanya maombi kila mara, kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kulisoma na kulitafarakri Neno la MUNGU.


Omba MUNGU akuvike vazi la furaha 


Zaburi 30:11 '' Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.''


Omba MUNGU kwamba majira yako ya baraka yavikwe wema.


Zaburi 65:11 '' Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono.''


Omba MUNGU awavike fedheha wote waliokuonea kipepo.


Zaburi 109:29 '' Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho.''.


Endelea kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU ili siku ya mwisho uvikwe mwili mpya usioharibika wala kuzeeka.


1 Kor 15:53-54 '' Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. ''


Maombi ya leo.


1. Vua mavazi yote ya kipepo uliyovalishwa na mawakala wa shetani kwenye ulimwengu wa roho. Yataje mavazi hayo kupitia vifungo unavyoona umefungwa mfano magonjwa, kuteswa n.k


2. Choma moto kwa damu ya YESU KRISTO kila vazi la kipepo ulilovalishwa na mawakala wa shetani.


3. Omba MUNGU awavike fedheha maadui zako.


4. Omba MUNGU ili majira yako ya baraka yavikwe wema


5. Omba MUNGU kwamba vazi la haki alilokuvika likupe baraka


6. Omba MUNGU akuvike vazi la furaha.



Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa. Bwana akuviahw vazi jipya leo kwa jina la Yesu.

No comments: