MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, March 24, 2021

 ⓂⒶⓉⒶⓇⒶⒿⒾⓄ ⓎⒶⓀⓄ ② *MATARAJIO YAKO* 2 

 ⓂⒶⓉⒶⓇⒶⒿⒾⓄ ⓎⒶⓀⓄ ② *MATARAJIO YAKO* 2 


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


24𝓽𝓱 𝓜𝓪𝓻𝓬𝓱 2021

*_Ufanye nini ili mztarajio yako yapate kutimia au yaendelee kuwepo_*❓

Mungu anataka vitu unavyotarajia vidhihirike.

1️⃣ Kinachoweza kuondoa matarajio yako yasitimie ni Dhambi

*Mithali 10:28*
_*[28]Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.*_

Kinachomuondoa MUNGU kwenye matarajio yako ni dhambi. Matarajio ya mwenye haki yatatimia na inakuwa furaha. Mungu anapokutendea kuna furaha inatokea kwasababu wewe ni mwenye haki. Kuna mtu moja kwenye Biblia ambaye akujali na aliuza uzaliwa wake wa kwanza. Esau alipofika wakati wa kubarikiwa akubarikiwa kwasababu ya mambo mawili uasherati na kutokujali.

*Waebrania 12:16-17*

*_[16]Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja.[17]Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi._*

Esau alipopewa ile nafasi hakuithamini na ndiyo maana alipotaka kubarikiwa hata kwa machozi hakupata baraka ile. Kuna nafasi umechezea kwenye ulimwengu wa Roho kuna madhara kiasi gani? Unapokula fungu la kumi unaweza usione madhara yake lakini kuna wakati wa kubarikiwa hautapata baraka na utatafuta hiyo nafasi hata kwa machozi.

Ni rahisi kufanya biashara ukifikiri kesho utakuwa na hiyo nafasi tena na ikipotea hauwezi kuipata tena hata kwa machozi dhambi inaua matarajio ya mtu. Esau alifikiri kupewa neema ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya kawaida ndiyo maana akadharau uzaliwa wa kwanza. Toba yenyewe ni neema kwasasababu Esau alitafuta lakini hakuweza. Wakati Baba yake anamtuma kwenda kuwinda ili ampikie Baba yake na kubarikiwa alikwenda akiwa na matarajio ya kupata baraka. Hakukumbuka kwamba aliuuza uzaliwa wake na hakuwahi kutubu akaona anaenda kufaulu. Lakini muda ule ule ambao alikwenda ndipo matarajio yake yaliibiwa.

Njaa ya Esau aikuwa ya kawaida bali ilikuwa ni kipimo cha yeye kumuheshimu Mungu wake. Changamoto uliyonayo ni kipimo chako cha kumuheshimu Mungu wako. Sijajua umepewa nini ndani yako lakini usidharau nafasi uliyopewa na Mungu, ukipotea utatafuta kwa machozi.

2️⃣ *_Hakikikisha unanena maneno mazuri kwa kila tukio linalotokea mbele yako._*

Maneno ni roho *( Yohana 6:63)* kwa hivyo ili kitu kife inategemeana na maneno yako. Shetani anasikiliza manenk yako na Mungu naye anasikiliza maneno yako, unaposema ndipo shetani anapata mlango wa kuyatekeleza kadhalika unaposema Mungu anaumba kupitia maneno yako. *Waebrania 11:3*

Unapotamka vyema ndipo unaachilia nuru kwa vile unavyotarajia. Ulichopewa ni faida hivyo hakikisha unatamka mema hata kama hasara inatokea wewe endelea kudai faida yako. Usigeuze matukio yasiyo ya kawaida kuwa sehemu yako. Wewe hauogozwi ma matukio bali neno la Bwana na ndilo linagengeneza picha ndani yako. Imani ni kuwa na uwakika na mambo yatarajiwayo, usiangalie mazigira au adui anayekuzunguka bali kile unafhotarajia kikupe neema ya kushinda.

*Hesabu 14:28*
_*[28]Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;*_

Kama ulivyosema ndivyo Bwana atakufanyia kama ukiongozwa na matukio maana yake utaongea na kunena sawa sawa na matukio ambayo yanaweza kuwa siyo matarajio yako. Unawezekana umekwama leo lakini si amarajio yako. Unapotamka kwa woga na kubeba udhahifu wa tukio ilo unalifanya liwepo.

Unapokutana na shimo siyo tukio la kukufanya ufe lakini unapotamka mabaya yataimarisha kile ulichosema kwenye kinywa chao. Mabaya hayana nguvu kama utashinda hofu ya matukio.

Changamoto zipo haijalishi huko kwenye ngazi ipi lakini changamoto ipo, mpaka utakapokwenda kwenye mji mpya na kuvumilia mpaka mwisho wake. Haushindi changamoto kwasababu umeomba leo bali ukiwa na kanuni ya Mungu utashinda changamoto. Mahesabu yanabadilika number lakini kanuni ni ile ile. Changamoto zinabadilika lakini ukijua kanuni ya Kimungu ya kutatua changamoto utashinda. Kanuni ya kwanza ya kutatua changamoto lazima umsikilize Roho Mtakatifu, yeye ndiye anajua matamanio ya Mungu wako. Yule Mama mshunami akukiri kwa kinywa chake kwamba mtoto wake amekufa na ndiyo maana Gehazi alimpomuuliza mtoto hajambo alisema hajambo *2 Wafalme 4:17-37*







No comments: