MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, March 25, 2021

ⓂⒶⓉⒶⓇⒶⒿⒾⓄ ⓎⒶⓀⓄ 3 *MATARAJIO YAKO* 3

 


ⓂⒶⓉⒶⓇⒶⒿⒾⓄ ⓎⒶⓀⓄ 3 *MATARAJIO YAKO* 3

25𝓽𝓱 𝓜𝓪𝓻𝓬𝓱 2021

Tunaendelea katika hatua ambazo tulianza jana za _Ufanye nini ili matarajio yako yapate kutimia au yaendelee kuwepo_*❓

3️⃣ MALANGO

Nilisema unaweza kuwa mtumishi lakini usiweze kuingia kwenye malango ya utumishi, Biblia inasema anasimama mlangoni na anabisha hodi. Unapoona unamatarajio ambayo hayatimii tazama lango lako la Baraka ili uweze kuingia.

Sasa ninaenda kwenye somo ili kwa mtiririko ufuatao,

*Jambo la kwanza*

_Shukrani_

Shukurani maana yake ni kuamini umetendewa na ni vyakako. Unapokuwa kwenye maombi elewa unachoomba kwasababu malango yanaweza kuwa wazi. Kwenye Biblia utaona watu walifunga na kuomba lakini hawakuwa na matarajio kwamba wanaweza kupata walichoomba. Mungu anaweza kukupa kile ulichoomba na ukakataa.

*Matendo ya Mitume 12:12-17*

*_[12]Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. [13]Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza. [14]Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. [15]Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake [16]Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. [17]Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine._*

Unaweza kufurahi lakini usifungue malango yako na muujiza wako ukabaki nje ingawa unausikia.

Wakati kijakazi anafurahi tuchukulie kwamba maaskari wangemkuta nje na Roda alikuwa ajafungua mlango. Angalia huu ni muujiza wako umetokea na umeuacha nje tu kwasababu umefurahia. Usiishie kufurahi bali fungua malango ili muujiza wako usipotee. Kumbuka wale wanafunzi walirudi wakifurahi na Yesu aliwaambia msifurahie utumishi huo lakini wafurahi kama majina yao yameandikwa mbinguni.

Walimuambia kijakazi ana wazimu kwa maana walikuwa hawana imani na kile walichokuwa wanaomba. Ndiyo maana walimuambia Kijakazi unawazimu wewe. Umeomba kupata mtaji na unapopata unasema sina biashara uliomba lakini haukuwa na matarajio ya kupata. Huyu ni Petro amekataliwa na bado amengangana mlangoni je muujiza wako utaendelea kugonga mlangoni. Unasikia kuombq kwaajili yq huduma yako lakini Mungu anapoachilia wingu la kwenda mahali unakataa sasa uliomba ya nini ?. Unaomba moto wa maombi unasikia mfungo wa siku 40 alafu unanuna sasa uliomba nini maana Mungu anataka ndani ya siku 40 moto ukamate.

Yule kijakazi walimuita mwendewazimu sasa kati ya wao na kijakazi nani alikuwa mwendewazimu. Kijakazi alipokaza kusema wakasema ni malaika wa Petro ni kweli malaikq wa Petro alimtoa gerezani lakini akuendelea kuonekana bali Petro ndo alionekana. Sijajua ni wangapi umefukuza na kuwaita wendewazimu. Hawa ndugu wamejifungia na wanaomba lakini imani ya kiwa yatakuwa yao haikuwepo. Kijakazi mwenyewe anaanza kushuhudia kabla ya kifungua mlango jaribu kufikiri wangefika pale wale askari ushuhuda ungepotea wa Roda. Ndivyo walokole walivyo wanaanZa kutangaza mafanikio yao kabla ya kufungua malango. Walianza kugeuza matarajio yake wakasema uu mwendewazimu kwasababu haujui kutofautisha kati ya Petro na Malaika wake.

Petro alifululiza kupiga kelele mlangoni hata walipokuwa wakishauriana ndani. Sikiliza muujiza wako hata wasemeje utaendelea kupiga kelele mlangoni.

Walistaajabu !!!!!!

Kwanini hawa ndugu walistaajabu ni baada ya kumuona Petro aliyekuwa mlangoni. Sikia watakapoona unainuliwa acha wastaajabu walikuona mjinga na mwendewaZimu lakini Bwana atakapoinuka na kuanza kukubariki wacha wastaajabu. Katika siku nilizotamka 90 wacha maadui zako wastaajabu, walikuona wakawaida na ukadhalilika lakini natangaza miezi mitatu wastaajabu na neema ya Bwana iwe juu yako. Uwe mtu mwingine kama ambavyo Farao alistaajabu kwa Waebrania wakati wakiondoka Misri wakiwa na vitu.

Tukimaliza hili somo nitakuonyesha hii Roho ya Farao na utaona viti ambavyo vimebebwa na hii roho ya Farao. Roho ya kutokumcha Bwana ni roho ya kimisri, nitakuja kukuonyesha. Wana wa Israeli walikuwa na matarajio yao lakini walipoingia misri wakawa watumwa na Mungu aliwaokoa kwenye malango ya Farao. Roho ya Farao inatumikisha Waebrani na Wamisri. Umeokoka lakini Roho ya mateso iko juu yako. Ndiyo maana aliwaambia atawaokoa na magonjwa ya Misri.

*Zaburi 100:4*

_[4]Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Ingia malangoni kwa kushukuri_




No comments: