MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, March 28, 2021

♨♨ KUSHINDANA NA ROHO YA FARAO AU ROHO YA KIMISRI ♨♨ 🆕️🔧


♨♨ KUSHINDANA NA ROHO YA FARAO AU ROHO YA KIMISRI ♨♨ 🆕️🔧

28th March 2021

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

Ni kweli umeomba na umevua vazi na unayo matarajio yako kwa Mungu, lakini usiposhindana roho ya farao hautaweza kutoka mahali. Roho ya Farao inatawala katika maeneo manne.

1️⃣Anga
2️⃣Ardhi
3️⃣Nchi
4️⃣Bahari

*Mwanzo 1:26-28*
_*[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. [27]Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. [28]Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.*_

Utaona namna ambavyo uliumbwa kwa mfano wa Mungu wako. Unayo nguvu ya kutawala ndani yako na umepewa akili. Wanyama wengi wana macho lakini akili hawana. Maeneo haya manne ndiyo ambayo Roho ya Farao inashughulika nayo. Ndiyo maana Farao alishindana na wana wa Israeli. Kumbuka wana wa Israeli walitaabika miaka mia nne na thelathini na walitoka ndani ya Nchi ya Misri kwa kufa wazaliwa wa kwanza tangu yule wa Farao mpaka yule wa kijakazi.wwliondoka kwa kumchinja pasaka na kuweka kwenye miimo ya milango yao na ndiyo maana Yesu alikuja kama sadaka ya Pasaka. *1 WAkorintho 5:7*

Kumbuka Farao ni mtu na ndani ya mtu kuna Roho ambayo inakaa ndani yake. Katika Nchi ya Misri walikuwa na Mungu wao ambayo ilikuwa ni Roho za mashetani.

*Isaya 19:3*
_*[3]Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi.Unaweza kushangaa ndani ya familia kuna watu ambao hawamtambui Mungu kwasababu wanakuwa na hii roho ya kimisri, utakutq mtu yuko tayari kwenda hata nje ya anchi kwasababu ya waganga wa kienyeji lakini kuja kanisani mtu ataki ni kwasababu ya hii roho ya kimisri. Sasa usishindane nao bali shindana na hii roho ya kimisri.*_

Roho ya Farao maana yake nini?

1️⃣ _Ni roho ya kuua kila kichanga au hatua yako ya kwanza unayoanza kwenye maisha yako._

Farao anasubiri unapata kazi na unapooanza siku ya kwanza wanaanza ugomvi na wewe na unashangaa mbona nachukiwa bila sababu, roho hii inaua nia ya kwanza na hatua ya kwanza. Wengi hii roho wanaita ya kukataliwa au ya kushindwa.

*Kutoka 1:15-16*
_*[15]Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua [16]akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.*_

Farao alipoona Waebrania wanaongezeka kwa maana wana matarajio ya kutoka Misri akainuka kinyume nao. Roho ya Farao inaanza kuona matarajio yako ambayo unayo ndani yako kwamba utaanza kutoka utumwani. Mtu anayo matarajio ya kupata kazi Faraonanaanza kuharibu kwenye chanzo na kuua mahusiano. Farao alipoona wanaongezeka akaongea na wazalisha kwamba kila mwanaume anayezaliwa hauwawe. Maana yake kila biashara inayozaliwa kwako ife, kila mtaji unaopata ufe.

Leo nimekuja na ile sauti ya Musa kwaajili ya kila mtu ambaye anateswa na Roho hii ya Farao kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.

Adui yako lazima ashirikiane na waganga wa kienyeji na wachawi sasa sikiliza ukiona hii roho inanguvu geuza wale waliotumwa ili washirikiane na madhabahu ya Mungu wako. Lazima uende kwa ufunuo geuza mioyo yao wawe wachaMungu. Wale wazalisha walipopewa agizo hawakuweza kugusa watoto wa kiebrania. Wakasema kabla ya sisi kuwazalisha tunakuta wamezaa wenyewe.

Sikia neno la Bwana waebrania siyo kama wamisri hawasubiri kupewa mitaji bali tunapoenda tunawakuta na mitaji na hatujui wametoa wapi? Walisema ikiwa ni biashara yenye faida ikiwa ni ndoa yenye amani hakikisha imeua. Ukiona mtoto wake anayo matarajio ya kuwa waziri hakikisha mmeua. Ukiona mtu anatoa sadaka na inaleta matokeo hakikisha mmeua. Waliambiwa wakiona Muebrania ni mjamzito wafuatilie kwamba ni kitu gani kitazaliwa. Wanasema haya maombi anayoomba yakufunga yanamatokeo sawa mpe usingizi, je ibada anazokwenda zinamatokeo mpe kazi nyingi na ubize ili kiroho chake kipoe na maono yapotee.

*Maombi*

Kuanzia leo ninaikataa hii roho ya kafao haitanizuia kwa jina la Yesu

Elewa jambo moja mwembrania hataelewa ni kwanini mtoto amekufa atajua ni bahati mbaya au ni kawaida tu. Yaani biashara kufa unaona kawaida tu kumbe ni hii Roho ya Farao.

*Omba maombi haya*

Bwana Yesu ninaifuta hii roho juu yangu roho ya farao ninaikataa iliyonitaabisha miaka mingi ninaondoa kwenye familia yangu kazi yangu kwenye uchumi wangu ninaondoa kuanzaia leo kwa jina la Yesu. Wewe anga achia wewe bahari achia wewe ardhi achia kwa jina la Yesu malango ya mzaliwa wa kwanza achia kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.

2️⃣ _Roho ya Farao inakutumikisha kwa kazi ngumu na yenye mateso kwa muda mrefu bila faida._

Unafanya kazi kwa nguvu tena ngumu na unachelewa kulala ukiandika mipango na Diary inajaa lakini hakuna hata mpango mmoja uliofanikiwa. Unachlewa kurudi nyumbani hata majirani hawakujui lakini jirani yako anakuja saa kumi na moja anayo matokeo chanya. Umeàjiriwa kwenye kiwanda miaka nenda rudi lakini hauna faida umebakia kuwa mtumwa tu.

*Kutoka 14:5-6*
_*[5]Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena [6]Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye;*_

Roho ya Farao haiwezi kukuruhusu kutoka tu. Walipoona wametoka walikaa kikao wakasema kwanini tumewaruhusu hawa watu kutoka. Alipigwa kwenye ibada na akatoka alafu unafika nyumbani wanasema imekuwaje tumemruhusu huyu mtu kutoka. Sasa kwasababu wamezoea kutumia akili zako, kichwa chako wataanza kuuliza kwanini tumeruhusu. Ndiyo maana unakuwa na ushindani hata kuja ibadani. Mungu alishuka na kugeuza moyo wa Farao uwe mgumu na akawafuatia *USIOGOPE WANAKUFUATIA KWA JINA LA YESU.*

Wana wa Israeli walitembea kwa miguu na walipotoka Farao akaandaa gari lake ili kuwafuatia, yaani umetaabika muda mrefu lakini siku moja tu roho hii i akuangusha. Usipomtegemea Mungu hii roho ya Farao ni siku moja itakurudisha nyuma. Roho ya Farao inakurudisha haraka chini kuliko ulivyoenda. Farao alichagua magari mia sita ili kuwafuatia na kuwarudhisha kwa siku moja.

Walipoanza kisogea wana wa Israeli wakaanza kutetemeka. Usitawaliwe na Roho ya hofu kwasababu itakurudisha utumwani. Nyuma ya Roho ya hofu kuna Roho ya Farao. Ujawahi kuona umegoma kwenda kanisani na mtu akikuuliza hauna sababu ya kusema. Roho ya Farao inakuonyesha umauti kabla ya kufa inakuonyesha umasikini kabla haujakupata inakuonyesha kushindwa kabla ya kushindana. Hii roho inakufanya uache kazi kabla ya kuandikiwa barua. Wana wa Israeli walisahau mkono wa Bwana uliowatetea kwa mapigo kumi na wakatoka misri walimnungunikia Musa lawama zikaanza kutawala. Wale walimungunikia Musa inawezekana na wewe kuna uliowalaumu kwasababu ya kushindwa kwako na ukawalaumu kweli sikiliza usiangukie mtu ukafikiri yeye ndiye amekufanya kushindwa. Kila aliyeshindwa anasababu zankushindwa lakini nakutangazia leo ukashinde katika jina la Yesu Kristo.

Wanamuambia Musa neno hili silo tulilokuambia tukiwa Misri kwamba utaondoka na Farao atatufuata, waliondoka wakiwa na matarajio ya kurudishwa lakini Musa yeye akulia wala kutarajia kurudi Misri. Musa aliwaambia watu hivi, *_Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele._*

Furaha nyingine ni hii kwamba hautatoka kwa Farao mikono mitupu

Kutoka 3:6-7

3️⃣ Roho ya Farao inakuweka utumwani muda mrefu

Biblia inasema Roho ya Farao iliwaweka miaka 430 wana wa Israeli UTUMWANI. Sijajua wewe umekaa na huo ugonjwa kwa miaka mingapi, sijajua miaka yote nini kinakutesa hiyo ni roho ya Farao lazima ugeuze maombi yako na kuanza kupiga Roho ya Farao. Kila mlango unaotokea unazuiliwa hii ni Roho ya Farao. Miaka mia nne wana wa Israeli wanalia kwa utumwa. Sijajua ninmuda gani unaomba na haujafanikiwa hiyo ni Roho ya Farao.

Maombi
Bwana Yesu kuanzia leo naikataa Rho ya Farao inayotenda kazi kupitia anga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi. Endelea kuomba kwa ajili ya kila eneo ambalo umekaa muda iwe ni biashara haina matunda muda mrefu, ndoa, kazi, magonjwa ya muda mrefu piga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi ili viachie maisha yako. Achilia moto kwenye anga, achilia moto ulao kwenye ardhi baharini mimina moto wa damu ya Yesu.

*Kutoka 12:40-42*

_*[40]Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. [41]Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri. [42]Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.*_

Walitumikishwa miaka 430 na Bwana alikaa kimya lakini wakati ulipofika hawakutoka watupu na wewe leo unayesoma haya na kuomba maombi haya hautatoka mtupu. Walizuianuzao wako utapata mapacha mpaka useme Bwana yatosha, walizuia amani yako utakuwa na amani mapaka wakushangae, walikuzuia usiolewa utaolewa na harusi yako itakuwa ya maajabu, walikuzuia usipande cheo utapanda mara mbilli kwa jina la Yesu. Haya si maneno yangu ni Bwana anasema _*Nami nitawapa watu hao kufadhiliwa mbele ya Wamisri; hata itakuwa, hapo mtakapokwenda zenu hamtakwenda kitupu;*_ *Kutoka 3:21* Hao waliokataa kukusaidia muda wote watageuka na kuanza kukusaidia wewe hao ambao walikutisha Bwana atawageuza kuwa msaada kwako. Kabla hawajapigwa kwanza wakusaidie alafu kisha watapigwa.

Mungu ni waajabu endelea kumtegemea na kumtafuta hata kama ni miaka kumi si wamekuona unamuimbia Yesu na wao wakashughulikia maisha yako wakati wanalia wewe utakuwa umeketi na wafalme.

Ngoja nijaribu hivi najua utaelewa

Wakati unaita nyota yako haitarudi kitupu bali itarudi na gari lako. Yule ambaye alikufunga akawa na nyumba u apofunguliwa utanunua na nyumba yake. Yule aliyechukua akili yako ukafeli na ukarudia madarasa yeye ameajiriwa na wewe ndo umemaliza elimu sasa hivi sikiliza neno la Bwana wewe unayesoma haya na kuomba utabeba cheo chake yeye. Unaweza kusema Bishop neno ili linakuwaje, Mordekai alikuwa akikaa malangoni na mtumwa tu lakini ghafla Hamani aliyekuwa anataka afe kibao kikageuka. Walikuwa wamepanga mabaya jùu ya Mordekai. Hamani wakati anaulizwa alijua ni yeye kumbe majira yalikuwa yamebadilika.

*Esta 6:1-10*
_*[1]Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme [2]Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero. [3]Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa. [4]Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari. [5]Basi watumwa wa mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme akasema, Na aingie. [6]Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiziwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi? [7]Basi Hamani akamwambia mfalme, Yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, [8]na aletewe mavazi ya kifalme ambayo mfalme amezoea kuyavaa, na farasi ambaye mfalme humpanda mwenyewe, ambaye ametiwa taji ya kifalme kichwani; [9]na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu. [10]Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote katika yote uliyoyasema.*_

Mordekai alisimamiwa na mfalme na alikupungua neno hata moja. Na leo mbingu inakusimamia alitapungua hata neno moja watarudisha vyote, kazi yako, kipawa chako, ndoa yako, mume wako, mke wako, watoto wako kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi. 

No comments: