MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, September 30, 2021

NGUVU YA MSAMAHA*



_*Na Bishop Danktin Rudovick Rweikila*_


*18th August 2021*


Mathayo 6:9-15

_*[9]Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

[10]Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.[11]Utupe leo riziki yetu [12]Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. [13]Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] [14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.[15]Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.*_


Katika maombi haya hakuna mhali Yesu alipoweka sharti isipokuwa kwenye mstaru wa kumi na mbili. Mstari hu9 ndiyo ambao una sharti la wewe kusamehe. Makosa yako yanafutwa na nguvu ya msamaha. Kama unavyoonyesha kuwasamehe waliokukosea ndivyo unapata nafasi ya msamaha. KAMA HAUNA NEEMA YA KUSAMEHE KWENYE NYAKATI HIZI ZA MWISHO MLANGO WAKO WA KWENDA MBINGUNI UMEFUGWA. 


Yesu alikuja kukomboa ulimwengu baada ya Mungu kutusamehe, huu msamaha unawahusu wale ambao wanasamehe. Kila mmmoja anatamani msamaha na tunaenda mbele za Mungu kuomba msamaha. Ni maumivu makubwa sana na hauwezi kusamehe pasipo kuondoa yale maumivu ya makosa uliyokosewa. 


Tumeacha vyote kwaajili ya Kristo ili tuweze kupata ufalme wa mbinguni. Tumepata Neema ya kuokolewa na tunapezwa usiku na mchana na kuonekana wajinga kwasababu ya kuutafuta ufalme wa mbinguni. Haya yote yamebebwa na nguvu ya msamaha. Pasipo kusamehe iwe unajitoa kwenywe kazi ya Mungu kwa nguvu sana lakini unahitaji kusamehe. 


Toba haina maana kwako kama wewe unayeomba haujasamehe waliokukosea. Ndiyo maana Biblia inasema usipowasamehe watu makosa yao Baba wa mbinguni hawezi kukusamehe. 


Sasa utajuaje umesamehewa? 


*Mathayo 7:15-20*

_*[15]Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. [16]Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? [17]Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. [18]Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. [19]Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. [20]Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.*_


Huu ndiyo udhuhirisho wa wateule siku hizi za mwisho. Si vazi la kujificha kwenye kanisa la walokole haitakusaidia ni ile hali ya kumaanisha. Kubadilishwa kwa ndani. Matunda yako yatakutambulisha. 


Ile hali ya kwamba huko kwenye kanisa la kilokole lakini ndani umejaa umbea, huzushi n.k. Wakati unakuja ambao hautaweza kuomba pasipokuwa na utakatifu. Kuna neema ilikuwa inaendelea kwetu ili tuifanye kazi ya Mungu. 


Matunda mabaya ni muonekano wako, matendo yako, tabia zako n.k, mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mema. Na Yesu anasema kila mwenye matendo mabaya anakatwa na kutupwa motoni. Tunafunga na kuomba si ili tupate pesa bali tupate ufalme wa mbinguni. 


Ni majira ya kujiandaa kwa kanisa maana Bwana harusi anakuja saa yeyote katika nyakati hizi. 



No comments: