MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, December 14, 2010

BSS 2010 TAREHE 17 DECEMBER KUFANYA KWELI



Meneja wa Bia za Kilimanjaro George Kavishe na Madamu Rita  
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika hotel ya Paradise city   alisema fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika Ijumaa hii tarehe 17 Dec 2010 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.


Ticket za shindano hili zimegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni kundi la viti maalum (VIP) ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu Arobaini na tano (45,000/=) na kundi la pili ni kundi la viti vya kawaida ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu ishirini (20,000/=).

Milango itafunguliwa kuanzia saa moja kamili jion na tiketi zinapatikana katika maduka yote ya shear Illusions, Biggy Respect, Ofisi za Benchmark Productions na katika ukumbi wwa mikutano wa Mlimani city ambapo fainali hizi zitafanyika.
 

 Tano Bora wakiwa wameshilia Hundi ya Million Thelathini ambayo itakuwa kama zawadi kwa mshindi wa BSS 2010






 Lema one akiwa na Bella wa star search



Mwalimu wa Bongo star search akinena kitu na mratibu wa BASATA Vicky Temu


















No comments: