MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 31, 2019

VIAPO VYA KICHAWI



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 



Ninapoongelea kiapo ni ile hali ya mtu kudhamiria ndani ya moyo wake. Na anapofaya hivyo anafunga nafsi ya yule mtu aliyemnenea. 

Mathayo 26:69-74 

69 Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. 70 Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo.
71 Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti. 72 Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. 73 Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.
74 Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo. 



Maandiko yanasema Pero aliapa na kusema simjui mtu huyu, kumbe hata mtu anaweza kuapa na hata kama ni ukweli. Petro alimjua Yesu lakini walipomuoji alisema hamjui mtu huyo. Shetani anaweza kugeuza kinywa chako na ukajinenea mabaya na ukaapa kwamba maisha yamekushinda. Kumbuka kiapo maana yake ni maneno unayojinenea kukuhusu wewe. 

Maombi 
Sema kwa jina la Yesu kwa damu  Yesu ee Bwana Yesu naomba unisamehe kiapo chochote nilichoapa na kujitamkia kwamba nitashindwa kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu. 

Wakati tulikamata wachawi na kuwahoji wakasema wamewafungia watu kwenye vinywa na wanaapa kushindwa wenyewe. Kwa hiyo wanakamata vinywa vya watu bila wao kujua na kuanza kutamka mabaya. Kumbuka uzima na mauti upo ndani ya kinywa chako. Kila mlokole unayekutana naye unapomuuliza unaendeleaje utasikia majibu yao si ya mema bali yamejaa ubaya na kushindwa. 

Waebrania 6:16 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. 

Kiapo chochote unachoapa unapokea adhabu na ndiyo maana hakuna mtu anaapa kwa mdogo wake bali kwa mkuu. Na ndiyo maana hata wachawi wanapishwa na si rahisi wao kuacha uchawi kirahisi kwasababu ya kiapo. Wengine wanaapishwa wakiacha uchawi watakufa. 





Maombi 
Yeyote kwenye familia aliyeapishwa kwaajili ya mauti, kwaajili ya mabaya ndani ya familia ninafuta hicho kiapo kwa Damu ya Yesu kwa jina la Yesu. Mkuu yeyote aliyemuapisha ninaondoa hicho kiapo kwa jina la Yesu. 

Sikiliza wengine wanaapishwa kwamba ukiacha uchawi mama au Baba au Mtoto wako anakufa, kwa hiyo mtu anafanya uchawi kwasababu ya kiapo alichoapishwa. Madhara yanatokea kwenye maisha yako kwasababu ya mtu ambaye aliapishwa kwamba akikosea anakuwa masikini au kwenye hali yeyote ya uharibifu. 

Maombi 
Leo ninafuta kila kiapo ambacho mtu ameapa kwa miungu yao kwaajili yangu ndani ya familia yangu kwa jina la Yesu. Leo ninafuta kila kiapo cha kipepo kwa damu ya Yesu. Ninakataa kila kiapo cha kichawi kwa jina la Yesu na kwa Damu ya Yesu. 

Waadamu wanaapa kwa mkubwa wao ili anapokosewa adhabu inatolewa, lakini leo tunaapa kwa Mungu wetu. Unapookoka maana yake na wewe umeapa kwa Mungu wako. Kama vile mchawi navyoapa na kupanda mabaya na wewe umeapa ili kupanda mema. Shetani anapojua una nguvu anakuchafulia kinywa chako ili utamke mabaya kweye maisha yako Na ndiyo maana ni mloole lakini unatamka mabaya kwa watoto wako, mke wako na hata kwajili ya afya wako. Uzima na mauti upo kwenye kinywa chako. Walokole wengi wanapoamka wanaanza kujinenea kushindwa na wanaanza kujinenea mabaya ndani ya maisha yako. 

Wakati tunamuhoji mtu mmoja aliyekuwa na uchawi alisema wao wakikosea kunena wanapewa adhabu. Lakini kwa mlokole anashindwa kuelewa namna ambavyo akinena madhara yanatokea juu yake, kwa kila neno unalosema kumbuka uzima na mauti upo kwenye kinywa chako. Unaposoma kitabu cha Ayubu Mungu anasubiri neno litoke ndani ya Ayubu la kukufuru lakini maandiko yanasema Ayubu akakataa kukufuru. Hati ya kifo cha Ayubu ilikuwa ndani ya kinywa chake. Sikiliza nikuambie hati ya uzima na mauti ipo kwenye kinywa chako. 


Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo (Mithali 23:7a)

Ukiona uzima ndivyo ulivyo, ukiona magonjwa ndivyo ulivyo. Hati ya mafanikio ipo ndani ya kinywa chako 

Maombi 
Nakataa mazingira yote niliyoandaliwa na wajumbe kutoka kuzimu kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu.

Ni rahisi sana kupangiwa wajumbe kutoka kuzimu, unashangaa kila aliyekuzunguka anachangamoto ya umasikini na wewe unajikuta unachangamoto hiyo hiyo, kama wana changamoto ya kukataliwa na wewe unajikuta hivyo hivyo. Ujawahi kusikia watu wakisema wanaume wa siku hizi hawaeleweki ghafla na wewe unajikuta hauwaelewi hata kama wanaeleweka. Imani uja kwa kusikia tena kwa kusikia NENO. Sasa unaweza kusikia neno la Bwana au la watu wabaya. Si kila mtu ni mzuri kwako wengine ni wajumbe kutoka kuzimu.

Ujawahi kuwaona wajumbe kutoka kuzimu namna wanavyoweza kukatisha mtu tamaa kwa vinywa vyao. Utawakuta wakisema nimeomba sana, nimebisha sana lakini sijaona matokea sasa jiulize baada ya hapo unaelekea wapi?. Sikiliza maandiko yanasema ombeni bila kuchoka na kuomba kwake mwenye haki kunafaa sana akiomba kwa bidii (1Wathesalonike 5:17-18 Yakobo 5:16). Ulikuwa mtu wa Imani na unapoona changamoto unajua kuna ushindi ndani yako lakini ghafla Imani yako unabadilishwa na wajumbe wataabishaji waliotumwa kukurudisha nyuma. 

Niliwauliza wale wachawi swali moja, kati ya dawa na maneno ni kipi chenye nguvu akasema hakuna dawa ambayo inafanya kazi bila kuinenea. Nikajua kitu kimoja uchawi si majani wala vitu vinavyotumika bali uchawi ni maneno. Uchawi si majani au kucha zilizofungwa bila kutamkiwa maneno. 

Shetani au wachawi wanaweza kukuchafulia kinywa chako sadaka unatoa lakini aumaanishi, kanisani unaenda lakini hauwezi kumaanisha, lakini mwenye kiapo analazimisha kumaanisha. Ukimaanisha kutumika tumika kwa uaminifu sehemu yako ndani ya mwili wa Kristo. 

Maombi 

Kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu yeyote aliyebadilisha kinywa changu nikajilaani ninabatilisha kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu.  

Wachawi wakikutana na mtu na kumsalimia, huwa hawabaki kimya moyoni wanatamka maneno ya kushindana. Hivyo mchawi akiwa anakusalimia tu jua kwamba Rohoni anachukua Baraka zako, yota yako. We unaweza kudhania kwamba unasalimiwa tu kumbe kuna maneno yanatamkwa kwenye ulimwengu wa Roho. Sikiliza hata wewe ni jeshi la Bwana ukiwapa salama hakikisha na wewe unawapiga kwa jina la Yesu. 




MAOMBI 

Tunaomba maombi ya kupigana na wachawi na kuna hatua kumi za kichawi.
1.    Uchawi wa mtu mwenyewe. 
-->
Ukitoka kuwa uchawi wa mtu unaanza kuwa uchawi wa familia, kisha ukoo, mtaa na hata kabila kwa ujumla 

No comments: