MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 31, 2019

KUFUTA KIAPO CHA KICHAWI 2


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 



Tuliposoma Waebrania inasema “Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.” Waebrania 6:16 Sasa kwa kuwa sisi tuna Mungu aliye hai maana yake yeye ni mkubwa kuliko majina yote. Kwa hiyo unapoliitia jina la Bwana wa majeshi unafuta viapo vyao. 

Wakati jana tunaangalia somo hili tuliona namna ambavyo mtu anaweza kuapa au kuapishwa. Kuna aina mbali mbali ya viapo na leo tutaangalia aina ya viapo. 

KIAPO CHA MANENO. 

Yoshua 9:1-2 1 Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo; ndipo walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao Israeli, kwa nia moja. (Soma sura nzima ya Tisa)

Hawa watu walijikusanya kwa pamoja na kwa nia moja ili kupigana na Yoshua, niliongelea kwa habari ya watu kunia kwa kitu kimoja. Watu hawa walinia jambo moja kwa moyo mmoja. Kuna watu wanaapa kwa nia moja ndani ya familia kwamba watu wote kwenye familia mtakuwa masikini. Kuna watu wanaapa kwamba majira fulani lazima ajali itatokee na ghafla kipindi hicho lazima mtu kwenye familia afe. Kuna watu wamewekwa kwenye viapo vya majira. Kama vile unavyoona mbunge anaapisha kwaajili ya jambo na anapokosea kusema inamaanisha wananchi wote walio kwenye jimbo hilo wamesema. Kama raisi ameapa kwaajili ya Tanzania inamaanisha kila anachokisema wote tumesema, akisema twende kwenye vita wote tunaenda. Ikitokea Raisi amekosea wote tumekosea na akitokea amegombana na mtu na akatangaza vita maana yake aliapa kwaajili yetu na nilazima tuende kwenye vita. Sasa kwenye ukoo mtu anaweza kuapa kwaajili ya ukoo, ndiyo maana unashangaa wanakufa kwa magonjwa ya aina moja. Ndiyo maana kiongozi wako akiongea fungua masikio yako usikie sawa sawa kwasababu neno analolinena linaweza kuwa na madhara. 

Wakati Raisi anasema niombeeni watu wakawa wanajiuliza tumuombee kitu gani, haaa sikia neno la Bwana ulipewa nafasi ya kuhakikisha kwamba kile unachotaka kitokea kinatokea. Kwa hiyo aliwekwa kwenye nafasi hiyo na kwa kuwa anamuamini Mungu wako alitaka uombe ili mapenzi ya Mungu ndiyo yatimia pale anaposema. Kwa hiyo umpende usimpende wewe omba tu kwasababu ndiyo ameshakuwa Raisi wako na hakuna njia nyingine la hasha atavisema usivyovipenda. 

Nyakati zimebadilika na wenye macho ya Rohoni wanaangalia na kujua namna ya kuomba. Kwa hiyo ni vyema usinune na uanze kupenda wale waliokula kiapo badala yako. Unajua kununa kwako kutaendelea kukuletea madhara, badilisha mtazamo wako na mawazo yako ili uanze kuwapenda viongozi wako. 

Geuza mtazamo wako umuendee Mungu wako na uanze kumpenda kwa moyo wako wote. Kumbuka Mungu anafanya kazi na wale wampendao. Warumi 8:28"Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake”

Uwezi kulinda kiapo na wala kutetea kiapo kama umelazimishwa na ndiyo maana kiapo ni hiari ya Mtu. Ndiyo maana mchawi anaambiwa utaua Baba yako anasema ndiyo, mama ndiyo maana yake upendo wake alionao kwa uchawi unazidi ule wa Baba, Mama, Mke au mtoto. Umewai kujiuliza upendo wako kwa Mungu unazidi upi wakati mwingine hata jirani unaopendo nae kuzidi hata Mungu wako na ndiyo maana jirani akikuambia usiende kanisani hauendi kweli. 

Tusome tena mistari ile ya Yoshua 9:3…..

 Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai,
4 wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyoraruka-raruka, na kutiwa viraka;
5 na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao, na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuingia koga.
6 Nao wakamwendea Yoshua hata maragoni huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. 7 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mwakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi?
8 Nao wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani? Nanyi mwatoka wapi?
9 Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,
10 na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.
11 Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu, walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari, mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi.
12 Huu mkate wetu tuliutwaa ukali moto katika nyumba zetu, siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama, umekauka, na kuingia koga;
13 na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimeraruka-raruka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana.
14 Basi hao watu wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa Bwana.
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia. 

Wenyeji wa Gibioni walienda mbele za wana wa Israeli kwa hila, walishona viatu vikuu kuu na kuvaa mavazi makuu kuu yote walifanya kwa hila. Walipokwenda ili kufanya agano na Israeli na ndiyo maana nilikuambia ombea sana kiongozi wako kwasababu akikosea na kufanya agano na watu wasio wazuri na wanaoonekana kaa msaada kumbe wana hila jua kwamba agano hilo na wewe ulikuwa miongoni mwao.  

Watu hawa walipanga hila miyoyoni mwao na njia pekee walitaka agano na wana wa Israeli ili waweze kuwa hai. Watu hao walijifanya kuwa wametoka mbali na waliyasikia matendo ya Bwana kumbe walikuwa wanasema uongo. 

Shida kubwa ya wana wa Israeli hawakutaka shauri kwa Bwana kwasababu ya namna ambavyo wale watu walikuja kwa hila hivyo Yoshua akuuliza kwa Bwana. Wengi tunapata vitu vya kufanya iwe ni kazi au chochote kile bila kutaka shauri kwa Bwana. 

Yoshua alifanya agano nao na akawaapia. Ni sawa na wewe unatoka kanisani na ukifika nyumbani tu wakwanza kukuomba pesa ni yule mchawi ambaye umetoka kupigana nae nani adui yako, bila hata kutaka shauri kutoka kwa Bwana unampatia na unashangaa kila wakati unarudi nyuma tu. Jua kwamba adui amekutenda kwa hila. 

Wiki hii inayokuja tutakuwa na maombi ya siku ishirini na moja na neno kuu kwenye maombi haya ya mfungo wa siku 21 ni Isaya 61:7 maombi ya urejesho. Tutakuwa na maombi kila siku saa kumi isipokuwa siku za mikesha. 

No comments: