MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 31, 2019

“KIAPO CHA KICHAWI”


Mungu ameaapa kwa neno lake. Mungu akiapa anaapa kwa nafsi yake, na Mungu akiapa jambo lazima litokee.
Mwanzo 22;16-25 
1Samwel 3:14
Zab 116:16
ISAYA 45:23
Mungu akiapa hakuna namna ya kukiondoa kiapo chake. Mfano taifa la Israel tangu linaanza lipo kwenye vita lakini bado lipo hadi leo kwasababu ya kiapo cha Bwana kwamba hakuna atakayeliondosha taifa la Israel katika uso wa Dunia.
Ndioo maana Elia Mtishibi alikua anaapa kwa kiapo cha Mungu kwa kusema “kama Mungu aishivyo…..”
Kiapo kinaweza kufunga.
Hesabu 30:2
Neno la Mungu ni kifungo
Hesabu 30:10 – 13
Kila neno la Mungu lafaa kwa mafundisho, neno la Mungu ni kiapo cha Bwana, lazima mtu apate kile Mungu alichosema atapata.
Hesabu 30:15
Shetani anaitwa mungu wa dunia hii, kama ambavyo Mungu anaapa shetani naye anaapa, kama ambavyo watu wa Mungu wanaapa na wakala wa shetani nao wanaapa kupitia majini na mashetani tokea kuzimu.
2Wakorintho 4:4
Matendo ya Mitume 22:12
Matendo 22:14 -20 – 21
Paulo akapelekewa taarifa kuwa kuna watu 40 wamejifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa mpaka wahakikishe Paulo amekufa.
Biblia nayo ina wasimamizi wa kiapo, ambao ni Roho Mtakatifu.
Wachawi ni wanadamu wanaofanya mapenzi ya ibilisi. Wachawi hawalogi mtu mmoja mmoja wao kama wao, wana vikosi na wana maeneo ambayo wanakutana. Wachawi wa kila mahali wana sehemu zao za kukutana. Mtu ambaye ni mchawi si rahisi kumfahamu kama unakaa naye sababu hutoka nje ya mwili na kuuacha mwili wake ndani kwenye ulimwengu wa rohoni bila kuonekana, kama mkeo ni mchawi unaweza ukabisha mpaka mwisho sababu akiwa anatoka usiku huwezi kumwona.
Wanyama wana uwezo wa kuona wachawi, Kwenye Biblia tunaona Balaam alipoitwa na Balaki kwenda kuwalaani Israeli njiani Punda aligoma kwenda sababu alimwona malaika ameziba njia lakini Balaamu akawa anampiga punda mpaka Mungu akafungua kinywa cha punda akaongea lakini aliendelea kumpiga na Mungu akafungua macho yake akamuona malaika amesimama njiani. Hii inaonyesha kuwa wanyama wanaweza kuona viumbe wa rohoni ndiomaana mbwa hutoa mlio kama wa mbweha wakati wa usiku pale wanapowaona wachawi.
Mchawi ni binadamu ambaye ndani yake kuna roho ya uchawi, wanapokwenda kuwanga wanaenda bila mwili ni (wachache tu wanaokwenda kuwanga wakiwa ndani ya miili). Ndio maana mumeo au mkeo kama ni mchawi unaweza usijue kwa kuwa akienda kuwanga anaacha mwili. Mwanadamu ni Roho inayoishi ndani ya nyumba nayo nyumba inaitwa mwili.
MADHABAHU ZA WACHAWI
Mahali ambapo wachawi wanakusanyika kwa ajili ya kuwanga viwanja hivyo vinaitwa madhababu ya wachawi. Wakikutana wanaanza kucheza ili mashetani yapande kwa maana shetani anapenda sifa na kuabudiwa. Kama vile tunavyocheza na kuabudu kanisani roho mtakatifu atawale Ibada ndivyo wachawi nao wanacheza usiku kwenye viwanja vyao ili wapandishe mapepo na majini kwaajili ya kufanya kazi.
‘KANISANI SIO MAHALI PA KUKUTANA ILI KUPEANA FARAJA, KANISANI NI MAHALI PA KUTATUA MATATIZO YALIYOSHINDIKANA KWA AKILI ZA KIBINADAMU KWA JINA LA YESU KROSTO”
Asili ya shetani: 
- Anapenda sifa
- Anakiburi
- Anapenda kuabudiwa 
Kama mtu anazoa tabia hizo hapo fahamu huyo asili yake ni kuzimu.
Wakishakutana wanapeleka mashtaka yao kwenye madhabahu zao, na mara nyini mtu anayeweza kukushtaki kwenye madhababu za kichawi huwa ni ndugu wa karibu au rafiki ama mtu anayekufahamu, au anayekujua aliyesoma na wewe. 
MTU NA NYOTA YAKE.
Kila mtu ana eneo la maisha yake ambalo nyota yake inang’aa sana.
- Wengine Baraka zao ni miguu 
- Wengine Baraka yao ni mikono 
- Wengine Baraka yao ni uso 
- Wengine Baraka yao ni tumbo la uzazi.
Wachawi wakishaona mtu ana tumbo lililobarikiwa kuzaa watoto wakuu wanapeleka mashitaka kwenye madhabahu zao ili tumbo lifungwe mtu huyo asizae. Ndipo unakuta mtu ana tatizo la uzazi kwa sababu tumbo lmefungwa au linatumika kuzaa watoto wa kijini.
Wengine wameona una uso wenye upendeleo, wanapeleka mashitaka kutaka ufunikwe uso ili ukose zile Baraka ambazo ungezipata kupitia uso wako wenye Baraka.
Mabaya yote hapa duniani yanatoka kwa shetani na mema yote yanatoka kwa Mungu, huenda leo na usiku wa jana umeshitakiwa kwenye madhabahu za kichawi na hujui lakini yupo Yesu kristo ambaye anauwezo wa kuvunja viapo vyote vya kishetani kwa mamlaka ya jina lake.
KWENYE MADHABAHU ZA KICHAWI WANAAPA. 
Kuna familia zina viapo unakuta watu wa familia moja wanagombana wao kwa wao na hakuna mafanikio. Wakati mwingine taifa linaweza viapo unakuta taifa lina kila kitu nambacho kilifanya lijulikane kama taifa masikini kwasababu ya viapo vya kichawi.
Bibilia inasema wasimamizi wa kiapo, neno la Mungu ni kiapo cha Mungu na msimamizi wa kiapo hicho ni Roho Mtakatifu, na wachawi nao wana wasimamizi wa viapo ambao ni mashetani, mapepo, miungu, majini, vibwengo n.k wanasimamia kama ni laana mpaka itimie, kama ni magonjwa mpaka yatimie, kama ni ugonjwa mpaka utimie, kama ni kifo mpaka kitimie wanasimamia lakini wanapigwa leo kwa jina la Yesu ili kila aliitiaye jina la Yesu awe mzima.
- Ndio maana kuna watu unakuta muda mrefu wapo kazini na anafanya kazi vizuri lakini hapandi cheo kumbe wamewekewa wasimamizi wa viapo wanasimamia wasipandishwe cheo.
Kama serikali inasema haiamini dini wala uchawi lakini viongozi wake ndio wanaongoza wanakwenda kwa waganga wa kienyeji na wachawi basi nchi ya namna hiyo shetani anatawala sana sababu anapenda kuabudiwa bila kujulikana.
Zakaria 3:1
2Wathesolonike 2:18-19
- Shetani anaweza kushindandana na mtu akiwa nje ya mtu 
- Shetani anaweza kugeuza maumbo 
Ufunuo 21:12
SHETANI NI MALAIKA NAYE ANAWEZA KUVAA MWILI AKAWA BINADAMU
- Malaika wa giza wanaweza kujifanya malaika ni shetani kabisa lakini anaonekana kama binadamu. 
- Mashetani wanaweza kugeuka kuwa kitu.
- Mtu anaweza kuwa ni binadamu lakini ndani yake kuna nia ya ibilisi.
- Nguo inaweza kunuiziwa maneno, Ikavaliwa na unayeivaa unakua umemvaa shetani mwenyewe bila yaw ewe kujua ambaye ndiye anayekuletea matatizo hayo.
Mashetani wakishatumwa kusimamia viapo vya kichawi wanakuja kwenye masha ya mtu sasa na kama walitumwa kusimamia asizae unakuta mtu anashindwa kutunga mimba kwasababu ya kiapo kilichotolewa asizae, kiapo kikivunjika mtu anakuwa mzima.
Wachawi wanapoapa na kutuma wasimamizi wa kiapo wanapanga na muda na saa ya uharibifu walioupanga kumpata mtu Fulani kupitia wasimamizi wa kiapo hicho.
“Kwa jina la Yesu nafuta ile saa na ule uharibifu ambao ulipangwa ukupate, na wale wasimamizi nawateketeza kwa Jina la Yesu kristo.”
Wachawi wakishaapa kwamba hatakaa upate furaha katika maisha unaweza kujikuta unapata nyumba, una gari lakini hupati furaha, kwa sababu kuna viapo vimeapwa kuwa usipate furaha, na wakatumwa wasimammizi ili kusimamia usipate furaha.
Ukivunja viapo vya kichawi, na kuwateketeza mashetani ambao ni wasimamizi wa viapo lazima maisha yako yabadilike na kua huru kwa jina la Yesu.
UKIRI:-
“Kuanzia leo mtu yeyote atakayekwenda kwenye madhabahu ya kichawi kunitaja, yote aliyoyataja juu yangu yampate yeye. Ninang’oa viapo vyote kwenye maisha yangu, viapo vilivyoapiwa kwenye biashara yangu, viapo vilivyoapiwa kwenye ndoa yangu, viapo vilivoapiwa kwenye familia yangu naving’oa kwa jina la Yesu.” Endelea kuharibi viapo vya kichawi juu yako na familia yako uwe huru kwa jina la Yesu Amen

No comments: