MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 31, 2019

KUTENGUA VIAPO VYA WATU WALIO APA PASIPOKUJUA WAMEAPA NINI AU AMEAPISHWA PASIPOKUJUA MADHARA YA KIAPO HICHO.



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 

Kuna watu ambao waliingia kwenye maagano ya kichawi bila kujua madhara ambayo yapo mbele yao. Wengine walienda kwa waganga wa kienyeji bila kujua kwamba kuna wakati ungefika na akadaiwa damu ya Mama yake au ndugu yake. Waganga wengi huwa hawasemi mambo yote zaidi wanasema tu huko tayari kufuata masharti yote. Kwa hiyo linapokuja swala la kuanza kutoa Damu kwasababu ulisema huko tayari inabidi ufanye hivyo kwasababu ya kiapo ulichokiapa. 

Unakuta ni ndugu yako au mama yako lakini anataka kukuua kwasababu ya aina ya kiapo alichoapizwa. Hivi viapo vinatokea hata kwa wana ndoa siku ya kuolewa au kuoana. Utasikia mtu anaulizwa Utamtunza na kumlinda kwenye shida na Raha unajibu tu ndivyo na Mungu anisaidie. Sasa wengine hawajui shida ni ipi, sikiliza uzizi si shida sasa kwanini unataka kukimbia kwenye ndoa kwaajili ya shida kidogo. Lazima ujue yale uliyoyanena kwa kinywa chako pasipokujua. Kuna wengi ambao wameshakwenda kinyume na kiapo chao cha ndoa ingawa wengi tunaapa kwenye shida na Raha. Wengine wanajua shida ni mtu kuumwa hapana ugonjwa ni ugonjwa wala si shida. 

Mathayo 14:1-9

Herode alikuwa anataka kumuua Yohana lakini kila anapotaka kumuua anaogopa watu. Kama hakuna kiapo hakuna ambaye anaweza kukuua kwa jina la Yesu. Inawezekana kabisa wapo ambao walitaka kukua lakini Damu ya Yesu inayosimama kukutetea autakufa kwa jina la Yesu. Shetani anatamani usisikie mafundisho haya kwasababu anajua aina ya viapo ambavyo walikuapiza na namna ambavyo vinakwenda kutenguliwa na damu ya Yesu. 

Nilisema usiwe msemaji sana ukifurahi au kuwa na huzuni. Herode alipofurahi baada ya binti Herodia kucheza mbele zake aliamua kuapa na kumuambia aseme chochote. Herode anamuapia Binti Herodia kwamba chochote atakachokitaka atampa. Kwa hali ya kawaida alifikiri akilini mwake kwamba ataomba mali lakini aikuwa hivyo. Herode pamoja na kumtafuta Yohana lakini maandiko yanasema “Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;” Kuwa makini sana unapokuwa na furaha usije kuapa na kiapo hicho kikafunga nafsi yako usiwe na maamuziNdiyo mchawi au mganga anakuambia huko tayari kufuata masharti yote na mara nyingi jibu linakuwa ndiyo.  

Naye, huku akichochewa na mamaye Binti Herodia aliomba kichwa cha Yohana, kwasababu alijua kwa kiapo hicho lazima kile anachoomba kitatekelezwa. Ndivyo ilivyo kwa wachawi kwenye familia na kwasababu ya kiapo walichoapiana kwenye familia utekelezaji unatokea. Kiapo chochote kina wapambe, wachochezi na wale wanaokumbusha juu ya kiapo ulichoapa. 

Mfalme aliumia sana kwa ombi la Herodia, ndiyo maana kwenye misiba ya namna hii ambayo watu wanashiriki siyo kwamba wale waliohusika hawaumii tena wanaumia sana ila wametekeleza kwasababu ya mkataba ambao mtu aliingia na kuapa. Kwa kuwa mchawi anajua kifo kipo anachukua kifo cha kutengeneza na kukifanya kuwa kifo halali. Wengi sana wamechukuliwa kwa kifo cha namna hii tunaishia kuzika migomba kumbe watu wamechukuliwa kichawi.  

Hawezaye kutengua kiapo ni Mungu peke yake, si unakumbuka waliapa kwaajili ya Danieli na mfalme akaapa na sheria ikawa. Danieli aliendelea kuomba na akakamatwa kupelekwa mbele ya Mfalme. Mfalme alisikitika sana na kwasababu ya kiapo ilimpasa tu kutekeleza yale aliyosema kwasababu tayari neno lake lilikuwa sheria. Nisikilize Simba wanaua, ajali inaua, na hata magonjwa yanaua lakini vyote hivyo viapo vinafutwa na Mungu aliye hai. 

Kama vile ambavyo ulisikia habari ya mtoto aliyepata ajali kanisani na kukanyangwa na tairi kwenywe kichwa chake lakini Bwana alimuokoa. Wachawi waliapa kwaajili ya mauti juu ya mtoto huyo lakini Bwana alitengua viapo vyao kwa jina la Yesu. Pengine Mungu alifanya hivyo ili Imani yako iweze kuongezeka, pengine haya ulikuwa unayasikia tu bila kuyashuhudia kwa macho lakini leo Bwana ameyapitisha kwenye mikono yetu ili Imani yako iweze kuongezeka. Kama tusingelisoma habari za Danieli tungeweza wapi kuongeza Imani zetu, kama hatukusoma mambo ya wana wa Israeli na namna ambavyo Mungu aliwatoa kwenye shida nyingi tungesimulia kitu gani wakati huu. Kitabu cha kutoka kiliandikwa baada ya wana wa Israeli kutoka.

Kila jaribu lina mlango wake, usiangalie kufungiwa angalia mlango wa kutokea. 

No comments: