MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, January 31, 2019

SABABU ZINAZOSABABISHA MTU KUTOA KIAPO



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


Ukifuta kiapo bila ya kufuta sababu zinazosababisha mtu kuapa utakuwa umefanya kazi bure na sisi hatutaki kufanya kazi bure kwa jina la Yesu. 

Mithali 6: 2Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako, 

Leo tunakwenda kijitenga na maneno ya vinywa vyetu kwa jina la Yesu 

Sasa sababu zipo nyingi sana ambazo zinaweza kumsababisha mtu kula kiapo na leo tutakwenda kutembelea jambo moja ambalo ni WIVU. 

1. WIVU

Wako watu wengi wamejaa wivu na wamepanga kupangua mawazo yako hata kama yanamanufaa kwako lakini kwasababu ya wivu wanataka kufanya mabaya juu yako. 

Matendo ya Mitume 13:45-47 45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. 46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. 

Wayahudi walijaa wivu na wakawa wanapingana na maneno waliokuwa wanayatoa. Kuna watu ni lazima wawe matajiri pinga unavyoweza lazima wawe na mafanikio. Hata kama watazuia miaka mingapi lakini ni lazima uwe na mafanikio. Waliokutegea mitengo ila hauwezi kuangamia ni lazima utapita katikati yao. Kwenye mabaya waliokuandalia yupo Mungu ambaye atakuinulia watetezi wako na utapita katikati yao. Wana wa Israeli ilikuwa nilazima watoke kwenye utumwa. Farao aliwazuia lakini kwasababu ilikuwa ni lazima watoke Mungu aliachilia mapigo na wakaachiliwa. Wapende wasipende lazima waachie mwaka wako huu ni mwaka wako wa UREJESHO. 

Usikosee njia yako ni lazima upite na kutokea upande wa pili wa mafanikio ya maisha yako. Kuna watu wanajiona nafsi zao kama vile hawastahili. Kama watu hawa ambao Paulo alikuwa anawahubiria waliona kama hawastahili vile walikuwa wanapewa. Kuna watu wanaona hawakustahili hata kuolewa, kuna wengi wameolewa na wanaona kama hawakustahili kuolewa na wale ambao hawako kwenye ndoa wao ndiyo wanaona walistahili kuolewa. Na ndiyo maana kinywa chako kwenye ndoa yako kiko kinyume na ndoa yako. Huko kwenye ndoa na unaona kabisa hakustahili kuolewa. Kuna watu wanabiashara lakini wanajiona kama hawakustahili kuwa na biashara hiyo. 

Kuna wengine wanaona kwamba hawakustahili kuzaliwa Tanzania na ndiyo maana wananungunika kuwepo. Wewe ambaye unaona ulistahili kuwepo unatafuta njia ya kupita kwasbabu unajua unastahili. 

Muulize jirani yako ulistahili kuwepo kwenye Ibada leo? 

Biblia inasema siyo wewe uliyenichagua bali mimi ndiye niliyekuchagua. Kwa hiyo siyo wewe uliyejialika kwenye Ibada bali Bwana ndiye amekuchagua uwepo kwa neema yake. (Yohana 15:16). Na ndiyo maana unapokuja kwenye ibada kila mtu analo fungu lake. Uliwahi kuona mtu anaalikwa kama mgeni rasmi kwenye sherehe na akakosa chakula si raisi kabisa. Kwa hiyo ukiona mwingine anakula hauogopi kwasababu wewe siyo mzamiaji, jua zamu yako imekaribia. Hivyo basi unapoona mwingine kafikiwa jua zamu yako imefika una haja ya kupindua pindua bufee andaa tumbo lako. Uzima wako ulistahili kuwepo, watoto, kazi na vingine vingi ulivyonavyo na vinavyokuja vilistahili kuwepo kwako.

Biblia inasema utakula kwa jasho na wala si kwa mateso, na tena Biblia inasema utazaa kwa uchungu si kwa mateso. Kwa hiyo unaweza kuwa kwenye kinakilishi (Computer) na jasho likatoka tu kumbuka hilo, SIYO KILA ANAYETUMIA NGUVU ANATAJIRIKA. Si unakumbuka kila mahali Yusufu alikpokuwa anapita alikuwa na nafasi ya utawala. Alipokuwa gerezani alikuwa na nafasi ya kutawala kama msimamizi, na alipokwenda kwa Potifa alikuwa msimamizi juu ya nyumba yake. 

Kuna watu ambao walipeleka mawazo yao kwenye maofisi na makampuni walipokataliwa na wao wakajikataa. Sikia neno la Bwana wakikukataa kampuni hii geukia nyingine, Paulo walipomkataa aliwaambia “Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.” Kwa hiyo mwaka huu ulichonacho lazima kitokee kwa jina la Yesu. Una mawazo mazuri ya umoja lakini wengine hawataki wewe songa mbele na wale waliokubali na Mungu atakuacha kwa jina la Yesu. 

Usigeukie upande wa pili kwasababu ya wivu au ubaya, bali geuka kwasababu ya Bwana 

Tunenda kuomba maombi ya kufuta roho za wivu na Roho ya kujikataa. Sasa ubaya au wivu unaweza kuwa ndani yako au ndani ya jirani yako hivyo leo unajipiga kwanza wewe unakaa sawa ndipo unapokwenda kwa jirani yako. 

Yohana 11:1-4, 40- 1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. 3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. 4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. 

Yesu aliapisha magonjwa na kusema ugonjwa alionao lazaro si wa mauti bali kwaajili ya utukufu wa Mungu. Ni sawa na wewe kuitamkia biashara yako “wewe biashara umeleta hasara lakini hasara hii si ya mauti”. Kwa hiyo wakati Yesu anamfufua Lazaro alikuwa anatenda kwaajili ya utukufu wa Mungu. 
Ukisoma Mstari wa nne na Tano utaona namna ambavyo Yesu anaongelea kwa habari ya ugonjwa wa Lazaro. Kwenye Mstari wa 40 utaona namna ambavyo Yesu alisema “Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” Kwa hiyo Yesu alijua kuwa atafufuka kwaajili ya utukufu wa Mungu. Usiangalie ugumu ulionao kwenye maisha yako bali angalia utukufu wa Mungu. Usiangalie migogoro kwenye ndoa yako angalai utukufu wa Mungu. 
                                                                                                                                
Yesu alilia kwa sauti kuu kwaajili ya kudai haki yake kwasababu alijua Baba anamsikia. 

Ingia kwenye maombi kwaajili ya kupiga kila wenye wivu….. Omba mpaka usikie kitu kwenye ulimwengu wa Roho. 




No comments: