MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, November 17, 2016

KURUDISHA MOYO WA UPENDO KWA MWANAUME

Wakati Mungu alimuumbwa mwanaume👷 alimpa moyo💖 wa kupenda💑 na mwanamke alipewa moyo wa kushauri ( Rejea somo la Kirudisha nafasi ya Mwanamke iliyopotea) . Mwanamke anaweza kumshauri mtu yeyote, lakini kama anamshauri mwanaume na upendo  haupo kwake elewa dhahiri kwamba hatayashika mashauri ya mtu asiyempenda💔. Ndiyo maana leo tunataka kurudisha moyo wa upendo, ili kile atakacho shauri mwanamke kiweze kuwa na faida ndani ya familia na maisha ya ndoa kwa ujumla.

Ufunuo 2:4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.

Efeso 5:25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Unaposoma ufunuo Biblia inasema nina neno juu yako, kumbuka upendo wa kwanza(First love), katika familia au mfumo wa kawaida wa wanadamu Mwanaume ndiyo wa kwanza kumpenda mwanamke💞 ndiyo maana ufunuo inasema kumbuka upendo wa kwanza. Kama ungekuwa na uhalisia ulionao sahii na ndio ulimfuata nao mwenzako uliyenaye kwenye ndoa  katu asingekubali.❌

Mimi nakumbuka wakati namchumbia mke wangu nilikuwa nikimsubiri sehemu masaa manne bila kuchoka, upendo usiopimika lakini kuna wengine wamefanya zaidi yangu lakini leo ndiyo hao wanaowaita wake zao majina yasiyofaa🐆🐒🐈🐐👺 huko wapi upendo wa kwanza?

1Wakorintho 13:8 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

Unapoona Biblia inasema upendo uvumilia niliposema nilikuwa nikimsubiri mama masaa manne, sikuwa mjinga ni upendo ulikuwa unavumilia . Ukiwa na moyo wa upendo hauwezi kuwa na maamuzi ya ghafla, ile hali ambayo ulikuwa ukimbebea mke wako zawadi🎉💐 vimetoka kwasababu upendo umeisha . Hata kama ilikuwa ni zawadi ndogo ilikuwa na maana sana kwake.👠
Tunapooa ndani ya familia mara nyingi atufanyi mambo au maamuzi kwa upendo, tunafanya kwa ukatili. 📖Biblia inasema katika kile kitabu cha Mithali "Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA."
MIT. 18:22 Maana yake ni nini Basi kama mwanaume ni kichwa👴 na mwanamke ni kiwiliwili👭, kichwa akiwezi kufanya kazi bila kiwiliwili. Ili baraka ziendelee kwenye ndoa💘 usijaribu kufarakana na kibali chako. Utakapo farakana na kibali chako utaondoa baraka juu ya maisha yako. Biblia inasema Adamu alipomuona Hawa akasema *"Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume"*Adamu akuambiwa na yeyote kuhusu Hawa lakini kwasababu ya upendo uliokuwa ndani yake💓 . Maandiko yanasema Enyi waume wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa🏥 lake. Angalia moyo wa upendo aliokuwa nao hata akafa kwaajili ya kanisa.Ilifika wakati walimletea Yesu kahaba na kwasababu ya sheria zilizokuwepo alistahili kufa yule kahaba na yeye akawaambia kama kuna ambaye ajatenda dhambi basi achukue mawe na ampige huo ulikuwa ni upendo na huo ndio moyo wa upendo unao hitajika kwa mwanamume kumpenda mke wake💏. Ukiwa na upendo utakuwa na chujio la kuchuja mambo ambayo yanapita kwako hata hata kama ni mabaya kiasi gani.

 Nawasihi wamama waombeni🙏 sana juu ya moyo💘 wa upendo kwa waume zao💏. Kama aukuomba wakati wa uchumba💍 na sasa unapitia mambo magumu nakusihi, rudi kwenye maombi🙏 na umuumbie moyo mpya mume wako.

Hata kama anakuambia nakupenda lakini ana uvumilivu ujue upendo hamna umeibiwa.

Wababa mkitaka amani ndani ya ndoa yako ni lazima urejeshe moyo wa upendo ndani yako

Wababa wamepoteza macho👀 ya kuona mbele kama kichwa cha Nyumba. Baba kama hauoni mbele utapoteza mwelekeo (Direction) ya familia yako. Lazima kabla ya kufanyia kazi jambo uliloletewa ulichuje.

Tunaitaji wababa wenye moyo❤ kama Elkana ambaye aliona moyo wa Hana na kuwa faraja kwake ingawa Penina alimchokoza mara kwa mara lakini Elkana kwasababau alikuwa anaona moyo wa Hana alimpenda na kumfariji

Wanaume wengi wanakuwa wapole wakati fedha zimewaishia ndipo wanashuka na kuanza kuona umuhimu wa mke wake . Mwanaume akiona hana kitu💰 hata kama alikuwa na sauti (kipezi) anakuwa mpole na kutaka kupangilia namna ya kuanza kunywa uji na mboga chuku chuku🙆 . Wanaume wakati wakiwa na fedha za kwenda Game Supermarket na kwingine kote thamani ya mke wake kwenye familia inashuka na kudhamini watu wa nje na kuwaona wao ni bora kuliko mke.

💀Shetani anageuza moyo ili Baraka isikae ndani ya familia👪, anajua wazi kama familia zikipona kanisa limepona na Taifa kwa ujumla . Sehemu kubwa shetani anayotumia ili kuvuruga Baraka (Uchumi)💱💷💶 ni mafarakano kwenye familia (Ndoa ) . Mlikuwa mkiomba🙏 kwa pamoja lakini sasa kila mtu anaomba kivyake. Mama anaomba akiwa chumbani tena kwa uchungu na majozi, na Baba anaomba akiwa Sebuleni na mara nyingine hata kwenye gari🚗 .

Moyo ukijeruhiwa utoa mabaya ya mwenzako bila hata kuangalia ni nani unamwambia. Unakuta mtu kwenye dala dala umekaa naye anaanza kuadithia mambo ya nyumba yake na kulaumu wanawake kwa maneno ambayo siyo ya maana kama "wanawake bana ni viumbe wa ajabu" " Najuta kweli kweli kuoa" ujue kabisa huyo moyo umechoka💔.

Ukiona mwanaume anasema umpikie chakula kizuri🍛🍲, wakati takribani mwaka mzima ajawahi kusema hivyo. Kila mara ukipika yeye anakosoa na kisifia chakula cha jirani. Ukiona hali hiyo wewe mama usipate shida muulize vizuri kwa unyenyekevu "Mume wangu ni chakula cha aina gani hicho na kiliwekwa viungo gani na gani?🍊🍅🍆🍇🍎" Ukipata jibu mchukue na umpeleke store na kumuonyesha kile ambacho kipo store ma muambia kwa unyenyekevu🙈 "Mume wangu niletee hivyo vyote ambavyo haviko store alafu ndo ufananishe chakula changu na cha jirani"

Usijaribu kuongeza uchovu kwenye moyo uliochoka, ondoa uchovu kwa kutumia busara na hekima . Ukiona mwanaume anakuambia Mama fulani anapendeza💅 usipate shida na kuanza kumwambia " kwa hiyo mimi sifai au mimi mbaya" cha kufanya ni kimoja tu. Mchukue mpeleke kwenye duka la nguo kisha mwambie "ninunulie halafu uone wiki moja nitakuwa nimen'gara kweli kweli" . Sasa usijaribu kumwambia kama mimi sifai basi niondoke "Utaondoka kweli!" Maana moyo wake umeshachoka . Wengi wanaanga namna hiyo wakifika mlangoni wanasema "Narudi tu kwaajili ya watoto wangu". Sikiliza usikae kwenye ndoa kwasababu ya watoto, maana ulipata ndoa kwanza kabla ya kupata zawadi ya watoto👪.

Sasa huo ndio uchovu unaokuta mama anaamishia kwa watoto na wanaupeleka mpaka kwenye ndoa zao. Wanaingia kwenye ndoa huku fikra zao zikiwa zimejengeka wanaume ni watu wabaya, wanyanyasaji. Ukiona Baba yako na mama awapatani na kwenye familia au ukoo watu kama watono au zaidi wanamigogoro ya aina hiyo hiyo, tambua jambo moja hiyo ni laana . Ingia kwenye maombi na tumia damu ya Yesu kuondoa hiyo laana isiwepo juu ya ndoa yako na familia kwa ujumla.

Kuna wanaume walikuwa wanajulikana kama mabondia💪 ndani ya ndoa kabla awajampa Yesu maisha yao, sasa wakishapata neema ya Kristo mama anaanza kuwa bondia kwaajili ya kulipiza yale mabaya aliyowahi kutendewa.

Kumpiga mke wako siyo kumfundisha bali ni kuongeza machungu zaidi. Na kufanya hivyo ni kutenda dhambi.

Sijajua ni wangapi wababa wanaomba msamaha . Lakini kile ninachofahamu ni kwamba mwanaume kuomba msamaha ni kitu cha nadra sana. Lakini tukiishiwa huwa tunaomba msamaha hapo ndipo utaona mwanaume anashuka. Mungu anaangalia kile ambacho kinakuletea kiburi na anakiondoa kama ni fedha, au jambo lolote lile, utaona mume anaanza kushuka na kunyenyekea.

Mwanamke usipange shida zako kama statment ya bank, Baba anaposhuka na moyo wake umerudi tambua neema hiyo. Nataka nikuhakikishie familia ikipona hata uwepo wa Mungu ndani ya kanisa utakuwa mkubwa.  Mara nyingi unakuta mwanaume anaondoka kwenda kanisani kwa njia yake na mwanamke kwa njia yake, na wote wanakwenda kusali, huko kwenye miyoyo wamewekana wao kwa wao. Hapo kuunakuwa hakuna ibada bali umeudhuria kanisani tu kama desturi ya wanadamu. IBADA NJEMA INAANZIA NYUMBANI.

 Unapookoka lazima misimamo uliyokuwa nayo ibadilike kabisa. Ndiyo maana nilisema kama umeokoka kwaajili ya kwenda mbinguni, hiyo ndoa uliyopewa kama dhamana unaweza usiende mbinguni kwasababu ya hiyo ndoa.

Ndoa ni utumishi, hakikisha umetumika vyema kwenye nafasi yako kwanza, bila kuangalia umefanyiwa nini timiza yakwako kwanza.

Mungu akubariki sana

No comments: