MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, November 15, 2016

KUNA VITU BINADAMU WANAVIONA VYA KAWAIDA ILA SIYO VIZURI

Na Bishop Dankton Ludovick Rwekila

Kuna vitu watu uchukulia ni vya kawaida kabisa ila vinamadhara kabisa tena makubwa , kwa leo angalau kwa udogo nikuambie mambo mawili

1 WIVU
 ● Wivu uleta mahasi makubwa sana , saa nyingine wivu unakusababisha uone unachodai ni haki kabisa .
  Kaini alione wivu kwa ndugu yake na kilichofuata baada ya hapo ni maasi makubwa sana .

Wivu usababisha mashindano yasiyokuwa na msingi wakati mwingine , 📖📖📖Mwanzo 30:1-2 ✏✏✏✏Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi. Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?
. Yakobo alikasirikia Raheli kwasababub tu ya wivu . Sasa unaweza ukaelewa wivu jinsi unavyoweza kusababisha mabaya

Mfano mwingine ni ambao tunausoma ni katika kile kitabu cha 1 Samweli 18 : 9 📖📖 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. Sasa unaweza kujua wivu ni mbaya kiasi gani

Kuna mifano mingi sana kwenye Biblia kiasi kwamba atutaweza kumaliza leo ngoja tusonge mbele kwenye jambo la pili

 2 TAMAA
Kutamani mambo yaliyo juu ya uwezo wako wakati speed yako iko kinyume na wewe .

Wengi wanalia leo kwasababu ya tamaa za muda mfupi .... Kaini alitamani kwanini mwenzangu abarikiwe na siyo mimi ...

🌏👉Wengi wamebadili neno tamaa na kuliita maono . Kwasababu ya aibu wanalificha neno tamaa kwenye maono .

👉✏✏Ukitaka kujua kama ni maono au tamaa angalia mwenendo wa mtu husika , Mungu uwa abadiliki badiliki . Tamaa uzaa dhambi ..

👉Wapo watumishi wa Mungu nao pia wanatamaa, wanakupa unabii kwasababu ya tamaa zake . Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maharifa  . Ukiwa na maharifa ya kutosha utaweza kutambua Neno la unabii na tamaa . Mwenye tamaa amabayo siyo maono kila mara uwa yanabadilika kulingana na mazingira .

Mungu akisema na wewe kwenye maono nilazima neno lake lidhibitike

Mara nyingi shetani atakuletea tamaa ili aweze kuuwa maono yako ya kweli .


Kwa mfano , Yesu alitokewa na shetani akamtamanisha ili aweze kuuwa maono yake lakini Yesu hali akijua ilo alingangana na maono yake . Mashujaa wengi wa Biblia walioanguka waliacha maono waliopewa na kufuata tamaa .

No comments: