MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 19, 2019

PEPO WA UTAMBUZI


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila. 

19thApril 2018 

Pepo wa utambuzi ni pepo wa ajabu sana na anatumiwa na waganga wa kienyeji lakini vile vile anaweza kukaa kwa mtu hata kama si mganga wa kienyeji. Waganga wa kienyeji wanamtumia huyu pepo kwaajili ya kuagua watu. Pepo huyu anatambua mawazo ya mtu na mipango yake, kwasababu shetani ashughuliki na mahali ambapo hakuna kitu. Pepo wa utambuzi anatumwa mahali ili kutambua hatima ya mtu. Kumbuka shetani hashughuliki na mahali ambapo hapana kitu anashughulika na sehemu ambayo anajua atapata faida. Hawezi kuingia sehemu ambayo tayari anajua hakuna Amani anaingia mahali ambapo kuna Amani na anaachilia faraka hapo. 

Pepo huyu akikaa ndani ya mtu ndiye anasababisha mtu awe mchawi au mshirikina. Hauwezi kuwa mshirikina au mchawi bila kuwa na wivu ndani yako. Unapokuwa na wivu ndipo unaanza kuchukua hatua ndani yako kwamba huyu atakuwa mtu Fulani baadae. Kwa hiyo pepo wa utambuzi anakuonyesha huyu mtu baadae atakuwa nani, kwa hiyo unaenda kwa wanganga wa kienyeji ili kujua kwa mambo yako ya baadae. 

2 Wafalme 23:24 

Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana.

 1 Samweli 28:5-7

 5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. 6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 

Sauli alipoona wafilisti akaogopa na kutetemeka akaenda kumuuliza Mungu na Bwana akakaa kimya. Mtu anaposongwa lazima atauliza kwa Bwana au kwa shetani. Mungu akusema na Sauli kwa ndoto wala kwa urimu na hata kwa manabii. Ukiona Mungu asemi na wewe kwenye ndoto wala kwa kutumia manabii wake jua hapo kuna tatizo. Kama Mungu anasema na wewe utaijua Ramani yako na njia unayoelekea lakini asiposema jua kwamba utageukia uapande wa pili.  Unaona namna ambavyo Mungu alikaa kimya lakini Sauli hakukaa kimya aligeukia upande wa pili ilia pate mjibu. 

Angalia kwenye ile mistari ya chini utaona namna ambavyo yule mwanamke mwenye pepo wa utambuzi alipoambiwa ampandishe Samweli kwa namna ambavyo alipata shida. Wengi wanashangaa mahali hapa unapoomba na jirani yako anakwenda kwa wanganga wa kienyeji anapoita jina lako anashangaa moto unawaka na anajua wewe ni mchawi kuliko yeye. Waliita Samweli na wakaona Mungu anainuka. Unapoona kwenye ndoto unashindana jua kwamba Mungu amekujulisha juu ya vita inayoondelea kweye ulimwengu wa Roho. 




No comments: