MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, January 23, 2018

KUFUNGA MALANGO YA KUZIMU NA KUHARIBU JESHI LA KUZIMU



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

20TH January 2018

Tumemaliza somo la kufuta viapo na kupiga viapo vya shetani na tunaingia kwenye somo lingine la kufunga malango ya kuzimu na kuharibu jeshi la kuzimu.

Unapoharibu jeshi la kuzimu unaharibu jeshi la shetani, kuzimu ipo na inatenda kazi kwenye ulimwengu wa Roho na jeshi la kuzimu lipo na linatendakazi kwenye ulimwengu wa roho. Na kuzimu haiwezi kutenda kazi pasipo wanadamu kama vile Mungu hawezi kutenda kazi pasipo kuwa na wanadamu. (Warumi 8:28) Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Shetani yupo na ametoka mbinguni lakini alifanya uasi, na siku zote muasi awezi kushinda kwa yule anayemuhasi.

Isaya 5:13-14 13 Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.
14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. 

Mtu anapokosa maarifa anaweza kupotea, shetani anaweza kukuogopesha kwasababu haujabeba ufalme wa Mungu. Na ndiyo maana lazima ujue kuzimu umjue shetani na kazi zake ili uweze kupigana nao kwa jina la Yesu. (2 Wakorintho 2:11) Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.


Maombi
Sema kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu sintapotea kwa kukosa maarifa kwa jina la Yesu. Ewe shetani uliyeshikilia akili yangu ufahamu wangu achia kwa jina la Yesu. Napokea nguvu ya maarifa ya Mungu kwa jina la Yesu na kwa Damu ya Yesu.

Mtu akishakuwa na maarifa maana yake anakuwa na cheo (Nafasi kwenye ulimwengu wa Roho). Wachawi wana maarifa na leo tunakwenda kupata maarifa na kuharibu makao yao kwa jina la Yesu. Mchawi ana maarifa kwamba anaweza kukulogha ukiwa ulaya lakini mlokole ana maarifa kwamba anaweza kumpiga mchawi kutoka mahali alipo. Leo na sisi tunapata maarifa na kuwateka mahali walipo kwa jina la Yesu. Leo tunawafuata walipo kwa jina la Yesu.

Kama wewe ulivyo na kiu ya Neno la Mungu na watesi wako wana kiu ya uharibifu wa maisha yako.        Hujawahi kusikia mvuta sigara anaamka usiku wa manane anatafuta sigara maali ilipo. Ndivyo ilivyo kwako, kama ukikosa kiu ya Roho Mtakatifu utaikimbia hata huduma. Ukiwa na kiu ya neno la Mungu hautaambiwa kanisa liko wapi au maombi ni saa ngapi lazima utataka kushindana kwasababu unasikia kiu. Ukiwa ndani ya daladala unajikuta unaomba kila saa kwasababu ya kiu iliyondani yako.

Kuna watu wengine walikuwa na kiu ya kwenda kwa waganga wakienyeji yaani akisikia habari ya mganga kokote tu anatamani kwenda. Ninapoongelea kiu namaanisha ni uhitaji wa kitu fulani mtu anapanga asikose jambo hilo kwa gharama yeyote. Wengine wana kiu ya sherehe tu yaania asipofanya sherehe roho yake haiku sawa. Unasikia msukumo fulani ndani yako.

Tamaa ya kuzimu

Kuzimu kuna tamaa nani tamaa ya uharibifu. Kuna wakati mtu anakuwa na tamaa ndani yake ya ajabu anaona kabisa kuna aibu inaenda kumpata lakini anakuwa na tamaa ya ajabu sana. Na ndiyo maana kama unafuatilia nchi yetu kuna mambo yanatokea maeno fulani fulani utakuta watu wanatenda mambo ya ajabu KUZIMU IMEFUNUA TAMAA YAKE. Si ulisikia kipindi kuzimu ilifungua tamaa yake ghafla kila mahali wanatafuta mikono ya watu wenye ulemavu wa ngozi, hiyo ilikuwa ni tamaa ya kuzimu. Na katika hali kama hiyo watu wasipoomba kuna maangamizi makubwa sana yatatokea (Matendo 12:5).

Kuna habari tunazisikia juu ya Nchi ambayo watu wanakula watu, sasa unaweza kuona ni jambo la kawaida kama kanisa lisipokausha hiyo tamaa kuzimu itaendelea kufanya uharibifu wake. Na leo tunakausha tamaa ya kuzimu kwa DAMU YA YESU.

Kila tukio linalotokea linasababu ya kutokea, hivyo kuzimu inaandaa mpango na kutupia wanadamu na wanaonekana wanadamu wanatenda kumbe ni kuzimu imeandaa mpango huo na wanaotekeleza ni wanadamu. Ngoja nikuambie Mbingu ikitaka kufanya jambo zuri lazima mwanadamu hatumike kufanya jambo hilo na ndiyo maana hata wakati wa ukombozi wetu wanadamu kikao kilifanyika juu mbinguni. Mungu akamtuma mwanae wa pekee akazaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu kama mwanadamu wa kawaida na akatukomboa na dhambi zote.

Kwa hiyo wakati haya mambo yanatokea siyo kwamba Mungu atakaa kimya kuna watu wataambiwa mambo hayo. Kama kuna jambo paya limepangwa kuzimu kuna watu wataoteshwa ndoto ili kujua kile ambacho kimepangwa. Wakati Yusufu aliyekuwa Baba yake Yesu anataka kumuacha mchumba wake Mariamu, Mungu alisema naye kwa njia ya ndoto na ndipo Yusufu akakubali kumchukua Mariamu (Mathayo 1:20). Hata Mbingu ikitaka kusema na wewe kuna ndoto Bwana atakuonyesha. Kwa hiyo hata wewe ndoto uliyoota si kwa bahati mbaya Mungu ametaka kusema na wewe kwa habari ya mambo mabaya yaliyopo kwenye maisha yako au yaliyozuia maisha yako.

Usiombe wakati mabaya yametokea, ukianza kuona unapata hasara kidogo kidogo jua kuna madhara yatatokea hivyo ni muhimu kuomba ili jambo hilo lisitokee. Kila changamoto inayokuja kwako usiizoe kwasababu siyo yako. Shetani anakamata akili yako ili uone ni kawaida tu. Kwa hiyo isifikie mpaka umetoka kwenye biashara kabisa ndo unakuja kwa Mchungaji. Kuna dalili za mwanzo kabisa za wewe kuanza kupata changamoto yeyote kwa hiyo tunataka wakati changamoto inaanza ikiwa ya moto hapo hapo ndo tunaanza kushughulikia changamoto ikiwa ya motomoto.

Sema kwa jina la Yesu ninarejesha maarifa yangu kuanzia leo…..

Ukishanyanganywa maarifa kuzimu inaachia tamaa, na kama hauna maarifa jambo lolote unaweza kufanya. Kuzimu inaweza kuachilia tamaa lakini isikupate wewe kwasababu una maarifa kwa jina la Yesu. Kuzimu ikashakuwa na tamaa tu unafungua kinywa chake kwa maana inataka kumeza.

Unapokuwa na tamaa kinywa cha kuzimu kinafunguka kwaajili ya kumeza wale wanaoifuata hiyo tamaa ya kuzimu. Na wale wanaofuata tamaa za kuzimu wanaanza kufurahia uovu. Mtu anaona mabaya kama ni utukufu wake. Ukisikiliza shuhuda za watu mbali mbali waliookoka utakuta wengi wao walivutwa na tamaa ya kuzimu, anatamani utajiri ambao mtu anauona kwa mganga wa kienyeji hiyo ni tamaa na kuzimu imefungua kinywa chake.

Mathayo 16:18 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 

Kuzimu ipo lakini unayo mamlaka ya fungua na leo tunahitaji kuzitumia kuifunga kuzimu kwa jina la Yesu. Kukemea kiburi, mashindano n.k bila kufunga malango ya kuzimu bado mabaya yataendelea kutokea. Hapa tumefika kwenye kiini cha kumpiga shetani mwenyewe na ni saa yake ya kumpiga shetani na tunamuendea mahali akaapo kwa jina la Yesu.

Ngoja nitoe matangazo yafuatayo kabla ya kwenda kwenye maombi

Siku ya Jumatano wiki ijayo ni siku ya wamama wale walio kwenye ndoa na tutakutana saa nane kamili. Tutakuwa na maombi ya kawaida vile vile.

Na siku ya ijumaa itakuwa ni siku ya Wababa ambao wako kwenye ndoa na tutakutana muda wasaa nane vile vile.

Na baada ya hapo tutapanga ratiba ya kuwa na semina ya pamoja ili tuwe na semina ya pamoja na familia zetu ziwe mpya kwa jina la Yesu. Na sijasahau vijana na wao tutakuwa na semina yao ambayo tutapanga hapo baadae.

Tuingie kwenye maombi

Sema kwa jina la yesu kwa damu ya Yesu napokea funguo za mamlaka kwa jina la Yesu, ninapokea funguo kwenye kinywa changu kwa jina la Yesu.

Kila nitakachokifunga leo kinafungika kwa mamlaka ya Damu ya Yesu. Ninaiendea kuzimu isiyoonekana kwa macho ya nyama ninayateka nyara malango ya kuzimu kwa jina la Yesu.

Ninakamata walinzi wa kuzimu walio kwenye malango kwa jina la Yesu. Ninawakusanya wakala wote wa kuzimu na kuwatupa kuzimu ninawafungia hawatatoka tena kwa jina la Yesu. Enyi majini mahaba ninawakusanya na kuwatupa kuzimu kwa jina la Yesu.

Ewe Roho ya Tamaa ninaikusanya na kutupa kuzimu kwa jina la Yesu. Roho ya kiburi, majivuno, kujisikia ninazikusanya na kutupa kuzimu kwa jina la Yesu. Roho za uharibifu, roho za ubaya, maumbo ya kuzimu ya wanadamu, nyoka, wanyama waliotoka kuzimu leo ninayakusanya na kuyanfungia kuzimu kwa jina la Yesu leo ninateka maumbo yote yaliyotoka kuzimu kwa Damu ya Yesu. Ninashambulia kuzimu, nateka wajumbe wake, serikali yake ninapiga vyeo vyao kwa damu ya Mwana kondoo. Ninaitawanya kuzimu kwa damu ya Yesu. Ninapiga jeshi lake kwa jina la Yesu. Ninashambulia mitaa yote ya kuzimu kwa Damu ya Mwana kondoo. Imeandikwa nao wakamshinda shetani kwa damu ya mwanakondoo. Leo ninawapiga kwa Damu ya Yesu.

Ninakamata leo mfalme wa kuzimu Abadoni sawa sawa na Ufunuo 9:11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake ApolioniLeo ninakamata vyumba vyote vya kuzimu vinavyotenda kazi kwenye ulimwengu wa roho kwa jina la Yesu. Ninalipua kuzimu kwa jiana la Yesu kwa Damu ya Yesu.

Leo kuzimu yote ninaiteka kwa moto, ninaagiza malaika wenye moto leo wafunge malango ya kuzimu kwa jina la Yesu. Ninafunga leo waliachilia mitengo mbele yangu ili ininase kwa jina la Yesu. Ninategua mitego walionitegea ili ininase kwa damu ya Yesu.

Kila mtego kwenye mazingira yangu ninaitegua kwa jina la Yesu. Ewe mitego ya umasikini, magonjwa, chuma ulete, nategua kwa jina la Yesu. Mitego iliyotegwa kwenye anga, ardhi ninategua kwa jina la Yesu. Ewe mtego wa kuchukua fedha yangu leo ninategua kwa jina la Yesu. Ninategua kila mitego iliyotegwa kwenye njia zangu kwa jina la Yesu. Kila mitego walioweka kwenye biashara yangu, kazi yangu, ndoa yangu, watoto wangu ninategua hiyo mitego kwa jina la Yesu.

Hiyo mitego iliyowekwa ili nifilisike na kurudi nyuma kiroho ninaitegua kwa jina la Yesu. Hiyo mitego ya kufilisika waliyotegesha kwenye mikono yangu ili wanase faida yangu ninaitegua kwa jina la Yesu. Hiyo mitego waliotega kwa watoto wangu ili wakose elimu ninaitegegua kwa ina la Yesu. Ninaitegua kila mitego ya majini mahaba kwa jina la Yesu.

Ninakamata kila mtego wa umasikini kwa jina la Yesu. Ewe kuzimu iliyefungua kinywa chako kwaajili ya tamaa leo ninakamata kinywa chako kwa jina la Yesu Kristo. Ninaachilia Malaika wa Bwana washuke mpaka kuzimu leo washuke kwa moto na kukamata kinywa cha kuzimu na nguvu zao. Leo tunalipua kwa moto wa Bwana. Ewe kuzimu uliyeamsha tamaa ninakulipua kwa jina la Yesu.

Mungu wangu akubariki na kukuifadhi kwa jina la Yesu usisahau kesho kuwahi kwenye ibada itakayoanza saa tatu za asubuhi njoo na mtu mmoja na Mungu atakubariki.










No comments: