MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, May 24, 2020

AHADI ZA MUNGU JUU YA MAADUI ZAKO WANAOKUONEA.


 

Sunday Service 24th May 2020

 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

 

1.    KWENYE MAISHA KUNA MAADUI WENGI WALIOKUZUNGUKA WAKIWA NA KUSUDI LA KUHARIBU MAISHA YAKO, HATIMA YAKO, MAONO YAKO NA KUONA NDOTO YAKO HAITIMII.

Kila siku inayoitwa leo maadui zako ni wengi wanaokuzunguka na wapo wanaoonekana na wapo wasioonekana. Wapo anaowahisi lakini wapo ambao hauwaisi ambao ni maadui zako. Zaburi 118:12 Biblia inakuhakikishia kwamba wapo maaddui zako na Mungu anawajua hata kabla wao hawajaanza uadui na wewe. Mungu aliijua idadi ya maadui zako kabla ya wewe kuzaliwa.

 

Zaburi 118:12-14

 

12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

 

Biblia inasema maadui zako wanakuzunguka kama nyuki kwa hiyo maadui zako ni wengi hauwezi kupigana nao wewe mwenyewe ila Mungu ndiyo anaweza kupigana nao anayetambua wingi wao na silaha walizobeba kwaajili yako. Daudi anasema adui zake walimzunguka kama nyuki na unajua nyuki wankuwa wengi ambao hauwezi kujizuia. Wanashambulia kwa wakati mmoja kama nyuki na kazi ya Mungu ni kukufunika na anapokufunika anawazima kama moto wa miibani. Kiuhalisia hauwezi kupigana na nyuki mmoja mmoja utakufa kwasababu ni jeshi linalokushambulia kwa pamoja.

 

Kawaida ya adui Mungu akimgeuza anatoa asali, kwa hivyo kuna maadui zako wanapozimika utateka maadui zako


13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.

 


Kusudi la adui ni kukusukuma na kukutoa kwenye nafasi yako ili uanguke na nafasi zinazotafutwa ni zile Mungu alizozisimamisha kwako kwaajili ya kufanikiwa. Nafasi ya kazi, biashara, ndoa, uzao, utawala, utumishi na maisha matakatifu. Hizo zote ni nafasi zinazompa Mungu utukufu zinapokuwepo kwenye maisha yako. Kazi ya shetani ni kuziondoa na kutupilia kwenye nafasi zingine, kama umasikini, magonjwa kushindwa kukataliwa, mateso, dhambi kwenye mabaya anayokuwa amekuandalia. Mungu alikujua kabla y aewe kuzaliwa na ndiyo maana alikutakasa na kukuweka duniani. Maadui zako wanaijua nafasi yako ambayo Mungu alikuweka kwa ajili ya hiyo duniani. Na wanajua wasipokusukuma utastawi kwenye nafasi yako.

 

Unaona Yusufu ambaye alikuwa na ndoto na ndugu zake walijitahidi kumsukuma ili asifikie kwenye hatima yake. Wao walijua wamemtoa kwenye hatima yako kumbe walimsogeza kwenye hatima yake.

 

Ndiyo maana wanapokusukuma mimi nasema uangukie kwenye hatima yako kwa jina la Yesu kama Yusufu alivyoangukia kwenye hatima yako.

 


14 Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.

 

Mungu anakupa nguvu ya kukuimarisha ili uendelee kubaki kwenye nafasi yako Ndiyo maana nasema  wamtegemeao Bwana ni kama mlima sayuni,

Ndiyo maana nasema twayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.




















No comments: