MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, May 24, 2020

NAMNA YA KUTEMBEA NA AHADI ZA MUNGU ILI ZIPATE KUTIMIA KWENYE MAISHA YAKO.


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

Image may contain: 1 person

16th May 2020

 

1.    . Ahadi za Mungu kuhusu Utajiri na Mafanikio ya Wana wa Mungu

3Yohana 1:2; 2Timotheo 2:7; Kumbukumbu 28:1-13; Zaburi 1:1-3; Yoshua 1:7-8

2Wakorintho 8:9; 2Wakorintho 9:11; Wafilipi 4:19; Kumbukumbu 15:4; Isaya 45:1-3 Malaki 3:10-12; Warumi 10:12 , Kumbukumbu 8:28 , 1 Nyakati 19:22

 

Umasikini ni nguvu ya mawazo ambayo unaamka nayo na kulala nayo. Unaposikia mawazo ya kuanzisha kitu fulani au kwenda mahali fulani nikanunua bidhaa fulani na kuuza kwa mtu hilo ni wazo na unapolitekeleza linakuletea fedha.

 

Hatua ya utajiri ni kwamba kila siku unapata fedha au baraka lakini sasa kuondoka kwenye umasikini ni kupata fedha inayozidi matumizi yako na ukubakiwa na akiba. Kwanini Mungu anazuia umasikini? kwasababu Mungu anaweza kuondoa mabaya ambayo yanakuletea matumizi mabaya.

 

Kwa mfano kama unatumia elfu tano na ukapata elfu kumi na tano maana yake umeanza hatua ya utajiri. Masikini ni yule ambaye anapata vyote na kutumia vyote kwamba hakuna kilichobaki. Umasikini uongezeka kila siku na umasikininao uongezeka kila siku. Ile akiba inayobaki kama hauwezi kuitumia vizuri utarudi kwenye umasikini. Na kumbuka kanuni ya Mungu ni kumuinua mtu mavumbini na kumketisha na wafalme.

 

Hakuna wakati utakaoweza kuona fedha ni nyingi, fedha ni mipango na fedha ni malengo. Kuna watu wana mawazo potofu kwamba kufanya mambo makubwa unahitaji fedha nyingi hapana ni mpangilio wa fedha ambao unapita kwenye mikono yako.

 

Kumbuka kwamba utajiri ni ahadi za MUNGU za wewe kuwa tajiri.

 

1 Samweli 2:7-8Image may contain: 1 person, closeup

Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.

 

 Mungu anaweza kukufanya kuwa masikini na Mungu anaweza kukufanya tajiri, chochote ulichonacho leo ni Bwana. Mungu akiongeza mawazo na akili njema ulivyonavyo vyote vitaongezeka. Mwanadamu akipataa wamawazo ya Mungu ametoka kwenye umasikini na ukikosa mawazo ya Mungu maana yake umekuwa masikini.

 

Shetani alipokuwa anamshitaki Ayubu alisema ni kwasababu umembariki na kumzungushia ulinzi pande zote. Unajifunza kwamba Mungu akikupa kumbe na ulinzi unakuwa juu yako. Shetani alipomshitaki Ayubu, Mungu aliondoa tu ulinzi wake kwenye mali za Ayubu na kuondoa ile akili ya kuzalisha na akawa na uchungu wa yale yanayompata ingawa alikuwa na Bwana.

 

Biblia inasema imani bila matendo imekufa kwa maana una wazo na imani ya kuwa tajiri lakini hauchukui hatua jua kwamba hiyo imani imekufa. Wewe ni tajiri shida yako kubwa una mashaka ndani yako. Imani unakuja kwa kusikia na ndiyo maana shetani anajua utakapopewa neno na kuliamini yeye anatuma wajumbe wake ili wakupe neno na unapoliamini tu umekuwa masikini.

 

Shetani anajua kwamba wawili wasipopatana hawawezi kwenda pamoja ndiyo maana mnaweza kukopa bank na akawafarakanisha mpaka fedha zinaishia ndipo mnapatana.

 

Mtu ambaye ameachiliwa Roho ya uharibifu hata iweje hawezi kukupa matumizi yake hata kama alipata milioni hamsini. Mwanadamu anaishi kwa huzuni pasipo yeye kutegemea na ndiyo maana unakuta mtu anajuta kweli baada ya kumaliza fedha aliyokuwanayo. Na ili uharibifu ukupate ni pale unapoanza kuwekwa BUSY na shetani. Unakuwa busy kiasi ya kwamba haupati muda wa kwenda kanisani, shughuli nyingi za dunia zinakuvaa na taratibu shetani anapata nafasi kwako.

 

Kumbukumbu 28:1 1takuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

 

Kusikia na kuyashika maagizo ya Bwana ndipo utaona mpenyo kwenye maisha yako. Sasa tulikuwa na semina ya watendakazi na tuliangalia kwamba moja ya agizo tulilopewa ni kumpenda jirani yako. Na wengi wetu hatukuwa tumeshika maagizo haya ya Mungu. Lakini tuliona vilevile agizo la kutoa sadaka kwa maana ya kumtumikia MUNGU na mali zetu. Tuliagizwa kutoa fungu la kumi na hii tukaona wengi tunamuibia Mungu.

 

Agizo la Mungu kwa sisi wanaume tumeambiwa tuwapende wake zetu na Bblia inasema asiyetunza wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko asiye amini. Sasa jaribu kuangalia umeshika maagizo hayo.

 

Wengi wameacha kusikiliza maagizo ya Mungu na usiposikiliza jua kwamba hauwezi kuaga umasikini. Hatutafuti Mungu anataka nini bali tunatafuta kwamba sisi tunataka nini? Ni muhimu sana kutafuta Mungu anatakani nini kwenye miradi yako, mahusiano yako, kazi yako lazima utafute Mungu anataka nini? Tumetaabika kwasababu tunaangalia kile tunachokitaka sisi siyo kile anachotaka BWANA. Ni muhimu sana kujua kwamba Mungu anataka nini? Kila siku tafuta Mungu anataka nini? Au kwa lugha nyingine tafuta kuyajua mapenzi ya Mungu (Zaburi 143:10)

 

 

Sulemani alipomwambia Mungu naomba maarifa na hekima yako, alijua ukiwa na hekima ya Mungu utayafanya yaliyo ya Mungu, Mungu akasikia na akamwambia kwa kuwa haukujitakia mali wala haukutaka ushinde vita katika kukubariki nitakubariki na hapatakuwako na mtawala yeyote duniani isipokuwa wewe. 1 Wafalme 3:5-28

 

Baraka ni kusikia sauti ya Bwana,

 

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Unapoisikia sauti ya Mungu na kuishika utabarikiwa, mjini, mashambani, uzao wako.

Unapoamka asubuhi kwenye maisha yako jifunze kumwuliza Mugu unataka nini? Nataka niende kwenye biashara lakini unataka nini kwenye biashara yangu? Unataka nini kwenye elimu ya watoto wangu? Natamani mtoto wangu awe mtumishi ila unataka nini kwenye utumishi wa mtoto wangu, naomba umpe hekima. Uone vile uweza wa Mungu unatembea.

 

Mungu anajua kila baraka kuna adui atatokea, ila Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako wapigwe. Unaposikia sauti ya Mungu Bwana atawapiga maadui zako wanaoinuka mbele yako.

 

Unapoona adui wanaanza kusema jina lako angalia kiwango chako cha Mungu na uwepo unaotembea nao.

 

Baraka inaamriwa, na kama inaamriwa maana yake inasikia na inaenda,  Sulemani alikuwa mtu wa kawaida lakini akaambiwa nimekubariki, nimeiamuru baraka ije juu yako. Ibrahim alikuwa mtu wa kawaida lakini baraka iliamriwa, Daudi alikuwa mtu wa kawaida lakini baraka iliamriwa.

 

Baraka ina masikio, unapofika uakiamuru kwa mume wako, mke wako, watoto wako, kwenye biashara yako baraka inaingia. Unapoiauru baraka inainiga inakaa mahali kwa hiyo nguvu hiyo inatua mahali. Unaweza ukaiamuru iingie kwenye ardhi yako.

 

Pasipo imani kuingia kwenye amtendo haiwezekani kwa hiyo unapotoka na nguvu ya baraka kanisani na ukagusa kwenye eneo lako, duka lako hayo ni matendo na nguvu ya baraka inaingia.

 

Na uchawi bala matendo haupo, ndio maana anaambiwa kavunje nazi anaenda, kabebe hirizi anaenda  sasa wewe mlikole ukiambiwa mbebe Roho Mtakatifu unasema nimemwacha nyumbani wakati yeye mchawi anatembea na hirizi lake analisikilizia linavyo hema na bosi akiwa mkali analitikisa akizidi kuwa mkali anaendelea kulitikisa utasikia bosi anamwambia jirekebishe, sasa wewe mlokole umemtikisa Roho Mtakatifu mara ngapi?.

No comments: