MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, May 24, 2020

AHADI ZA MUNGU JUU YA MAADUI ZAKO WANAOKUONEA

Sunday Service 24th May 2020   


Overnight Prayer 


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


1.    ADUI UJIKUSANYA KILA IITWAPO LEO WAKIPANGA MABAYA JUU YAKO LAKINI MUNGU UHARIBU MIPANGO YAO KILA IITWAPO LEO.

Kuna wapelelezi waliotumwa juu ya maisha yako wakipeleleza mipango yako, ngvu yako kila iitwapo leo.

ISAYA 54:14-17

14 Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.

 

15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.

 

16 Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.

 

17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.

 

 

2.    ADUI UANDAA SILAHA KILA IITWAPO LEO KWAAJILI YA KUANGAMIZA MAISHA YAKO NA MIPANGO YAKO NA MAONO YAKO, NA KAZI YA MUNGU NI KUZUIA AU KUHARIBU KILA SILAHA INAYOKUWA IMEANDALIWA KWAAJILI YAKO.

 

Adui uandaa silaha kupitia watu wake ambao kazi yao kubwa ni kukushambulia kupitia silaha zao lakini Mungu anaachilia silaha zake kwa watu wake hili kushinda watumishi wa shetani. Ndiyo maana tunaomba ili kupata silaha za Bwana kwaajili ya kupatilisha kila silaha za shetani.

 

ISAYA 54:17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.

 

3.    MUNGU ANAPOSIMAMA KUKUPIGANIA LAZIMA UMPE NAFASI ILI YEYE AWEZE KUPIGANA NA ADUI ZAKO UKIWA KATIKA HALI YA KUMTUKUZA MUNGU WAKO.

 

KUTOKA 14:14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

 

 

4.     ADUI HUWA ANAONA HASIRA PALE UNAPOENDELEA KUSTAWI NA KUONGEZEKA NA WAO UANDAA MIKAKATI YA KUKUSHAMBULIA.

Mungu anapowafanikisha watoto wake na kuingia kwenye hatua ya mafanikio mara nyingi wanasahau kuomba na wanasahau kumtumikia Mungu. Kumbe adui anaona hasira pale unapokuwa kwenye mafanikio. Walokole wengi wanatamani kulia wanapoingia kwenye changamoto na wanapofanikiwa wanamsahau Mungu.

 

ISAYA 41:11 Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.

 

Wote wanaoona hasira juu yako hawawezi kutawanyika pasipo Mungu kuwa juu yako. Usipokuwa na Mungu maana yake adui zako wanaoona hasira juu yako hawataweza kutawanyika kwasababu hayupo wa kuwatawanya.

No comments: