MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, February 05, 2018

KUFUNGA MALANGO YA KUZIMU NA KUHARIBU JESHI LA KUZIMU SEHEMU YA SITA

  
Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

3rd February 2018 Ibada ya Jumamosi ya Maombi na Maombezi

KUKOMBOA MWILI WA MTU NASFI YA MTU ILIYOTEKWA NA KUZIMU

Zaburi 30:3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. 


Kuna watu ambao wanaweza kushuka kuzimu, nilisema kuzimu ina malango na yanafunguka kadri mtu anavyotenda uovu. Unapotenda dhambi unaruhusu malango ya kuzimu yafanyekazi juu yako na kukushusha kuzimu.

Tuliona kwamba kuzimu ina mikono na kinywa tuliangalia katika sehemu iliyopita. Mtu ana sehemu kuu tatu ambazo ni mwili, nafsi na Roho. Nafsi ina Fikra (Mind)Hisia (Emotion) Maamuzi (Will) na Roho ina Utambuzi (Intuition) Dhamira (Conscience) Madhabahu(Altar) na mwili una muunganiko wa Nyama, Damu na Mifupa. (Mwanzo 2:7)

Kwa hiyo kuzimu inaweza kushikilia maamuzi ya mtu kwa kukamata nafsi yake ili hasiweze kufanya maamuzi yaliyosahihi kwenye biashara. Utakuta mtu anayo mawazo mazuri na msukumo anao lakini nia yake imefungwa ili asiweze kufanya jambo hilo. Shetani anajua kwanini anachukua nafsi za watu kwenda kuzimu. Nataka uelewe kitu kimoja kwamba watu hawalingani kuna viwango tofauti tofauti, kuna watu wamebarikiwa kwenye, biashara, ndoa, elimu na vitu vingine vingi. Shetani anachokifanya anachukua ile nafsi na kuiweka kwenye mwili uliotekwa ili kutenda mabaya. Ndiyo maana unaweza kumuombea mtu akakuambia nafsi yake imetekwa na Bibi au Shangazi na wanaitumikisha.

Ngoja nijaribu hivi ninaposema watu wanazaliwa kwa vitu mbali mbali, kuna watu niwadogo kiumri lakini wanafanya mambo makubwa sana. Jaribu kumuangalia Samsoni alizaliwa kama mnadhiri wa Bwana kwa hiyo nafsi yake ilikuwa tayari kwaajili ya kuokoa watu wa Mungu kwenye mikono ya wafilisti. Kwa hiyo shetani anapoiba nafsi kama hiyo anakwenda kubadilisha matumizi na kumtumikisha kwingine.

Ni wengi sana wanatamani kuwa mwaminifu lakini siyo mwaminifu kwasababu nafsi zao zimetekwa na kuzimu. Unatamani kutenda mema lakini hautendi mema. Shetani akikuona umeokoka anatamani uwe silaha ambayo haina madhara, kama ni kuimba utaimba, kama ni kunena utanena kwa lugha lakini ndani hakuna kitu ndani yako. Kama ulimezwa usikimbilie manung’uniko unapoguswa bali kimbilia kukamilishwa unapoguswa. Wengi sana Mungu anaposema nao badala ya kutamani kubadilika wanaanza mang’uniko na kuendelea kutenda uovu katika malalamiko na mang’uniko hayo.

Maombolezo 4:18-22 18 Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika. 19 Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani.
20 Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tukakaa kati ya mataifa. 21 Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi. 22 Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako.

Kuna watu wanavizia hatua zako unapoinua mikono na uwepo wa Bwana ukashuka juu yako na kujaa nguvu kuna watu wanakuvizia ili huiache hiyo njia. Wanajua kabisa ukiendelea na njia hiyo wewe si wakawaida. Kuna watu nilikuwa naongea nao kwa habari ya ufalme wa mbinguni na wakasema usiangalie matendo yangu mimi naujua moyo wangu kwamba ninakwenda mbinguni. Nikawaambia jambo moja ufalme wa mbinguni umefananishwa na mtu anayetafuta fedha. Sikiliza nikuambie jambo mfanyabiashara anatafuta fedha, mbunge, Raisi, Changudoa, mfanyakazi wote hawa wanatafuta fedha. Kwa hiyo kinachojalisha ni njia ambayo unatumia kutafuta fedha kazi ambayo unaifanya ni halali au haramu. Najaua haujanielewa bado Imani yako inajegwa kwa neno la Mungu na ambalo linafundishwa kwa kweli yote. Kwa hiyo si kila njia ni sahihi kwaajili ya Imani yako kuna njia ambayo itakupeleka upotevuni. Usijaribu kusema kila njia ni halali kwamba naweza kusali kila sehemu, kumbuka shida si kusali shida ni njia yaani Imani iliyopo mahali pale inakujengea nini wewe. Haijalishi njia hiyo unaona wanapita watu wawili watatu tangu asubuhi lakini njia ikawa sahihi. Kuna mahali pengine utakutana na makutano na yamesonga kweli kweli lakini kumbe inakwenda upotevuni. Ndiyo maana njia inayokwenda upotevuni ni pana sana lakini njia inayokwenda kwenye uzima wa milele ni ndogo.

Unaweza kuchukia njia ndogo kwasababu unaona unachelewa kufika kujenga nyumba, kuwa na gari, kuwa na fedha lakini hiyo ni njia sahihi kwako. Usijaribu kutoka kwenye njia hiyo hata kama hauoni mafanikio yako kwa sasa. Wengine wanatoka kwenye njia kwaajili ya kukosa chakula cha siku moja.

Unaweza kufuatilia ushuhuda wa kijana aliyeokoka na alikuwa buguruni kimboka alipitia hali ngumu sana akiwa na miaka kumi na nane na kufikia hatua ya kuingia katika wizi wa vifaa vya magari. Ukifuatilia ushuhuda huu kwenye youtubu yetu utaelewa namna watu wanavyoibiwa nafsi zao.

Mtu anaweza kuwa na utumishi ndani yake lakini shetani akateka nafsi yako na ikatumika kwaajili ya uharibifu. Kuna wakati unafikia mwisho na unageuka na kusema yatosha haya yamefikia mwisho. Kuzimu iliyoachilia uovu wake sasa yatosha niwakati wakugeuka na kuacha uovu. Nilazima utambue majira na ifike wakati ugeuke, kuna wakati wamefikia majira yao ya kubarikiwa na usipojua ni majira yako ya kubarikiwa utaishia kupishana na Baraka zako. 

Muhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 


Unapoona majira yako lazima ujiandae kwaajili ya kupokea majira yako. Hakuna mtu ambaye anajua ni majira ya kupanda na asitayarishe shamba lake. Na inapofika majira yako ya kubarikiwa ndipo utaona mafuta ya Roho mtakatifu yakimiminika juu yako na utangara kwa jina la Yesu.

No comments: