MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, February 05, 2018

KUFUNGA MALANGO YA KUZIMU NA KUHARIBU JESHI LA KUZIMU SEHEMU YA SABA



Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

4th February 2018

KUPIGA KUZIMU INAYOACHILIA WATU WA KUZUIA HATMA YAKO


Wakati tunaelekea mwisho wa Somo hili tunakwenda kuangalia kipengele cha mwisho kwenye somo ambalo tulikuwa tunaenda nalo kwa muda sasa. Na katika kipengele hichi cha mwisho tutaangalia namna ambavyo kuzimu inaweza kuona hatima ya mtu na kuzuia mapema.

Kuzimu inaweza kujua hatma yako kabla ya wewe kufika kwenye hatima yako. Kuzimu inaweza kujua wewe ni Mchungaji kabla haujaitwa kuwa Mchungaji ndiyo maana utakuta unavita bila kujua kwamba kuzimu inajua hatima yako. Kwa hiyo naongea na mtu ambaye hajawa tajiri lakini kesho ni tajiri naongea na wale ambao siyo watumishi leo lakini kesho watakuwa watumishi.

Maandiko yanasema Herode akapigana na mtoto Yesu, kwanini anataka kumuangamiza kwasababu kuzimu ilijua Yesu ni nani? Walimtafuta Musa akiwa mchanga na kutaka kumuua kwa sheria iliyokuwa imewekwa ya watoto wote wa kiume wa Waebrania watakaozaliwa kuuwawa.

Ni saa ya Kanisa la Bwana kuonekana na wala hawatakuona kwa jina la Yesu, ni majira yako sasa ya kuonekana ni majira yako ya kuinuliwa.

Saa ya mtoto kuzaliwa imefika, wapende wasipende lazima uzaliwe, hawana namna ya kuzuia kazi yako isizaliwe, miezi ya kazi yako kuzaliwa umefika lazima huduma yako, kazi, biashara, kampuni lazima jambo lako lizaliwe. Wapange operation lazima hazaliwe, waloge wasiloge lazima uzaliwe na mimi nimekuja kukutangazia lazima kazi yako, elimu, biashara izaliwe. Hakuna namna nyingine na kuzimu inajua na ndiyo maana tulianza kwa kuifunga kuzimu ili utakapozaliwa wasikusumbue.

Wale waliopanga mabaya juu yako Bwana amewatokea usiogope hauwaye mwili na akaacha Roho bali muogope yeye ambaye anaweza kuua mwili na Roho. Bwana amewatokea wanaozuia kazi yako, maandiko yanasema Yusufu aliazimia kumuacha Mariamu kwa siri na Bwana akamtokea kwenye ndoto. Huu si wakati wako wa kusema kwasababu Bwana atasema badala yako siyo wakati wako wa kujitetea ni wakati wa Bwana kusema badala yako.

Ninababa Yangu asiyeshindwa kamwe…..... embu tuimbe wote wimbo huu….....

Hesabu 22:1-14 (nitanukuu mistari michache na mengine unaweza kusoma ili kupata somo kamili) Basi, njoo wewe, nakusihi UNILAANIE WATU HAWA; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa. Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua UJIRA WA UGANGA mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA ATAKAVYONIAMBIA; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu. 

Usishangae Biblia kuandika Bwana atakavyoniambia kumbuka mstari wa saba umeandika wakachukua ujira wa uganga. Angalia mstari wa 12 Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa. Hilo ndiyo neno lako ambalo nataka ulijue siyo kwamba hawatakupeleka kwa waganga watafanya hivyo lakini Mungu anasema usilaaniwe kwasababu wewe umebarikiwa. Wakati huu hata Baraka za wana wa Israeli zilikuwa hazijaonekana. Nilisema kuzimu inaweza kuona masomo yako kabla hata wewe haujaenda kusoma na ndiyo maana wanasoma nyota za watu wanaweza kujua kwamba hii ni ya utumishi au ni mtu wa namna gani kuzimu inaweza kuona. Wakati wa Yesu Mamajusi waliona Nyota ya mashariki na wakajua yupo Mfalme amezaliwa na wakaiendea ile nyota na wakumuendea Yesu na wakamsujudia. Mamajusi hawa hawakuambiwa kwamba Yesu ni mfalme walijua kwasababu ya yota yake ndivyo ilivyo kwako kuzimu ilijua wewe ni mfanyabiashara, mtumishi kwasababu ya yota yako.

Balaki alipoliona jeshi la Bwana kwambali akalichungulia na hakaona utiisho juu ya jeshi la Bwana kwa hiyo anaita mjumbe wa kuzimu Balaamu ili haweze kuwalaani waisraeli waliobarikiwa. Ndivyo ilivyo kwako leo wapo wajumbe wametumwa kutoka kuzimu ambao wameona Baraka zako. Walibeba ujira wa uganga kama watu wanavyowaendea waganga wakisema kwamba nataka huyo asinishinde kwenye biashara. Kuna watu wanaona cheo chako hivyo wanatoa ujira wa uganga ili usiweze kupanda cheo chako maana wanajua ukipanda cheo wewe si wa kawaida. Balaki haliiona hatima ya wana wa Israeli na akataka kuizuia kabla haijatimia na mimi leo natangaza aliyezuia Biashara yako hawatazuia kwa jina la Yesu.

Angalia Mstari wa kumi na Tano 15 Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza. Mchawi hachoki kutuma watu kwaajili ya kufunga maisha yako. Kwa hiyo na wewe usichoke kuomba bila kuchoka. Balaki aliwatuma watu wengine wakubwa na wenye vyeo kuliko wale wakwanza.

Maombi
Sema kwa jina la Yesu kwa Damu ya Yesu yeyote aliyetumwa kwangu ninawaharibu kwa Damu ya Yesu imeandikwa Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo. Ninateketeza ushirikina wa mashetani kwa jina la Yesu. Matunguri yao nayateketeza kwa Damu ya Yesu. Amen

Nataka uelewe kitu kimoja unapoomba siyo kwamba hautaona vita mbele yako kwa hiyo kama zamani ulikuwa unapigwa na uwajui sasa hivi unapoomba Mungu anafungua adui yako unaanza kumuona kabla hajakukaribia. Mungu anakuonyesha adui yako ili upigane kabla hajakushinda na kwanini nayasema haya kwasababu wiki ijayo ni yaajabu sana Mungu anakwenda kuwaleta maadui zako uwaone kwa macho ya nyama kwa jina la Yesu. Mungu anaweza kuyafunua kwenye ndoto lakini vile vile anaweza akamleta adui yako mbele yako, ndipo unakutana na mtu anakuambia maombi yako yanatuchosha. Kuomba unaomba wewe lakini wao wanapata shida na maombi yako. Na Mungu anaweza kumfunua kwa kutumia Rafiki yako watakwenda kwao na kuanza kusema sikuizi Fulani simpendi kwasababu anaringa kwaajili ya kazi, ndoa au chochote kile jua kwamba unapoomba kwaajili ya kazi yako yeye anapigwa.  Kwa hiyo wengi tunaomba kanisani na tunao ndugu huko na marafiki wanaofuga majini na wanaologa kwa hiyo usizani kwamba watafurahia maombi yako watakuchekea tu lakini ndani wamejaa hila.

Hakikisha unaomba bila kukoma.

Mungu akubariki sana kuanzia jumatatu tutakuwa na maombi ya familia na kila mtu atomba ndani ya Familia yake yale ambayo anataka Bwana ayafanye. Tutaungana kwenye maombi saa nne usiku kila siku kasoro siku za mikesha yaani Jumanne na Alhamisi kwasababu tutakuwa kanisani.

Mungu akubariki sana    






No comments: