MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, February 07, 2019

NINI MATARAJIO YA MUNGU KWA VIJANA



Na Shemasi Anold Lema

1Yohana 2:14
“Nimewaandikia ninyi, akina baba,kwa sababu mmemjua yeye aliyetangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi,vijana, kwa sababu mna nguvu, naneno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi mmemshinda yule mwovu”

Mungu anao mtazamo wake binafsi juu ya kila kundi la watu chini ya jua,. Na kila kundi mfano wa wamama, wajane,watoto,vijana kuna mambo fulani ambayo Mungu anatarajia kila kundi litatekekleza. Mungu anazungumza na vijana na kusema nimewaandikia ninyi vijana moja mna nguvu, mbili neno la Mungu linakaa ndani yenu, na tatu yule mwovu. Mungu anazungumza na vijana na kusema nimewaandikia ninyi vijana kwa sababu

Moja
mna nguvu

Mbili
Neno la Mungu linakaa ndani yenu,

Tatu
mmemshinda yule mwovu.

Nguvu zinazozungumziwa hapa ni nguvu, uweza wa Mungu wa kukusaidia kutekeleza maagizo yake.
Na kwa sababu hiyo basi kuna matarajio ya Mungu kwa hao vijana.

Sasa lengo la ujumbe huu mfupi ni kukueleza nini Mungu anatarajia/anategemea kwamba utafanya sawasawa na nafasi aliyokupa mbele zake na uwezo aliokupa. Matarajio ya Mungu kwa vijana ni kama ifuatavyo:

Vijana wauteke ufalme wake.

Mathayo 11:12 
“Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.

Biblia inapozungumzia ufalme wa Mungu inazungumzia habari za utawala wa Mungu. Hivyo ni matarajio ya Mungu kwamba popote pale vijana walipo basi watatengeneza mzazingira ya Mungu kutawala katika maeneno waliyopo iwe
darasani,
Chuoni,
Kazini,
Kanisani nk na hii ni kwa sababu wana nguvu.

Sikiliza vijana wana nguvu na ufalme unapatikana kwa nguvu, maana yake Mungu anatarajia vijana watumie nguvu zao kuuteka ufalme wake na kuurusu uchukue utawala duniani.

2. Vijana warejeshe urithi na mali za wana wa Mungu zilizotekwa.

Mwanzo 14:13-16
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.14 Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.16 Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.

Hizi ni habari za Ibrahamu aliyeenda kumuokoa nduguye Lutu baada ya kuwa ametekwa. Ili kurejesha urithi wao na mali zao ilimbidi Ibrahimu atumie nguvu kazi ya vijana. Na hivyo hata leo Mungu anatarajia kwamba vijana wasimame kwenye nafasi zao na kupambana kwa ajili ya afya, ulinzi, uchumi,uponyaji,mafanikio ya watu wake. Hebu jipe dakika moja halafu tazama jinsi shetani anavyotesa watu na kudhulumu
afya zao,
ujana wao,
ndoa zao ,
uchumi wao nk.
Ni nani watakaorejesha hali nzuri, urithi huu kwa wana wa Mungu , ni Mungu kupitia Vijana.

3 Vijana wasikosee katika kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa.

Mithali 5:18
“Chemchemi yako ibarikiwe;Nawe umfurahie mke waujana wako”

Sikiliza Mungu anataka ndoa yako iwe ni ndoa ya mafanikio na ya furaha, maana yake ni ndoa ambayo hautaijutia kwamba kwa nini nilimuoa au kuolewa na huyu mtu. Sasa ili ndoa yako iwe ni ya furaha na amani, ni lazima huyo mwenzi wako umpate kwa uongozi wa Mungu mwenyewe. Sasa mtazamo wa Mungu kwa vijana ni huu vijana hawatakosea kufanya haya maamuzi kwa sababu tayari Neno la Kristo limejaa kwa wingi ndani yao. Kumbuka neno la Kristo ni taa ya miguu yangu.

4 Vijana wawe wasuluhishi wa matatizo katika jamii na taifa.

Mithali 1:4
Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari;”

Leo ndani ya kanisa, jamii tunayoishi na katika taifa kwa ujumla yapo matatizo mbalimbali ya kiroho,
kiuchumi
kijamii
kiafya
kimwili
kibiashara
kindoa nk.
Sasa Mungu anatarajia vijana ndio watumike kusuluhisha matatizo haya mbalimbali katika jamii kwa sababu ya wingi wa neno la Kristo ndani yao. Hii ina maana mtu mwenye neno la Kristo kwa wingi ndani yake basi maana yake ana upeo mkubwa wa kuelewa mipango na njia za Mungu za kuwatoa watu wake kwenye matatizo yanayowakabili. Hivyo tumia fursa hiyo kutatua matatizo hayo na kusuluhisha kwa sababu ya Kujua mawazo na njia za Mungu za kuwatoa watu wake kwenye shida walizonazo.

5 Vijana walitumikie kusudi lake la kuhubiri habari njema.

Mathayo 28:19 
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza  kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”

Sikiliza kwa sababu ya nguvu ambayo Mungu amewekeza kwa vijana basi ni matarajio yake kwamba wewe kama kijana utatumika kuwaeleza watu wengine habari njema za Yesu Kristo ziletazo amani.Ni matarajio yake kwamba vijana watapita nyumba kwa nyumba , mtaa hadi mtaa   wawaambie wengine kuhusu huyu Yesu, wakiwafungua waliofungwa na kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika. Naamini haya matarajio matano ya Mungu kwako kama kijana mwenzangu basi yatakusaidi sasa kukaa kwenye nafasi yako ili Mungu ajivunie kuwa na kijana kama wewe.

AINA YA MAOMBI YANAYOFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO KWA VIJANA

1.     Jiombee Hekima na Maarifa

2 Nyakati 1:7-12 

Hekima ni uwezo wa kukusaidia kuweza kufanya vitu muhimu kwa uweza wa Mungu kwa ajili yake na uweza wa wake.
-kama unahitaji utajiri jifunze kwanza kuomba hekima kwa maana ukiwa na hekima Mungu ndio ataleta na utajiri.

-Kuna umuhimu mkubwa sana wa sadaka katikamaombi yako.Mstari wa 6 alitoa sadakaMstari wa 7 Mungu akamwambia aombe atakalo

-Hekima ndio itakufanya uombe au ufanyevitu/maamuzi kwa usahihi.

2.     Mungu akuepushe na majaribu

Mathayo 26: 36-46
Dawa mojawapo ya majaribu ni maombi, kwahiyo usiombe tu pale upatapo majaribu. Ili kuipa nguvu roho yako jinsi ya kushinda majaribu basi jifunze kuomba. Si kila tatizo ni jaribu, jaribu ni lile ambalo linakufikisha njia panda kwamba ufuate mapenzi ya Mungu au la. Kama halikufikishi hapo basi hilo ni tatizo tu

Mungu hawezi kukupa jaribu ambalo sio size ya kwako na kama litakuzidia ni lazima atakupa na mlango wa kutokea.

3.    Maombi ya kuchuja watu wa kuwakaribu nawewe

Mungu hakumleta mtu duniani ili atafute marafiki. Usikubali marafiki wakuchague ila wewe ndio uwachague Na usichague bila ya kuwa na muda mzuri na mwingi wa kuomba ili usije chagua na wakina Yuda Na itafika mahali lazima utakutana na akina Yuda maana nao pia wana umuhimu wake. Moja ya jambo linaloponza vijana ni kuwa na marafiki kutokana na mazingira fulani yaliyokubana, kumbuka wengine si marafiki ni majirani tu.

-Watu wengi huwa wanasubiri hadi umri uende ndio waombe juu yawenza wao mke/mme. Ukijifunza kuombea hilo mapema ujananiMungu atakukumbuka na kukuepushia watu ambao sio kwa ajili yako.Yesu alipanda kuomba usiku na alipoamka alipata uwezo wa kuchaguawanafunzi.
Ni hatari sana kuzoeana tu bila ya kusudi na kama mkizoeana basimuheshimiane.

Zaburi 1:1

Si kila mtu unatakiwa ukae nae.

4.     Ombea mafanikio ya mji unaokaa

Yeremia 29:7,11-19
Mungu anajua mipango anayotuwazia na ni mipango ya kutufanikisha

Daniel 1
Ombea miji au mahali ambapo Mungu anakupeleka hata kama ni kwa muda mfupi.


5.     Omba upate kumjua Mungu na uweza wake

Waefeso 1:17-23
Unaweza ukageuza maombi haya yakawa yakwako ukijisemea wewe. Mungu anaangalia maombi ya aina yoyote hata kama unayasoma kwenye karatasi (uliyaandika), cha msingi yawe ni kutoka moyoni Wokovu ni _investiment_ Mungua anayoifanya kwa ajili ya _kudeposit_ uzima wa milele na baraka na mafanikio yake kwako.
Unapookoka mapema na ndivyo Mungu ana deposit mambo mengi kwako na kuwa baraka kwa wengine. Yesu hakufa kwa kila mtu ila alikufa kwa kila aaminiye, kwahiyo msalaba hauwezi kukusaidia kama hauamini kile kilichofanyika msalabani.-Unapookoka Mungu anaongeza thamani katika maisha yako. Mungu atanyanyua watu kwa kila hatua ambayo unapita ili ufanikiwe. Atanyanyua wakina Barnaba kwa Paulo. Tukiendelea kukua katika Bwana tutatengeneza kitu ambacho kitaendelea kuleta na kuzidisha utukufu wa Mungu zaidi.

6.    Ombea wengine, usiombe maombi ya kichoyo
Ayubu 42:10
Ayubu alipoombea wenzake na ndipo Bwana akampa mara mbili zaidi. Hata mbinguni kuna account pia na sio benki tu. Mbinguni kuna account ya Fedha pia. Na ndio mana alisema leteni zaka kamili Ghalani Mbinguni pia kuna account ya Maombi. Jinsi ya kufungua account mbinguni ni kukubali na kusaini kitabu cha sala ya toba ambapo details zako utaziweka mbinguni.

Ku *deposit* au *kuweka* kumojawapo katika akaunti ya maombi ni kuwaombea wengine.
Ku *withdraw* au *kutoa* kumojawapo ni kujiombea au kutumia ile akiba iliyotokana na kuombea wengine. Kumbuka na ujihadhari, usije ukawa unachukua tu kwenye akaunti ya maombi hadi ikaisha
kila kitu na bila ya kuweka. Ukipata nafasi ya kuombea wengine itumie vizuri maana una *deposit* kitu kwenye akaunti yako itakayokusaidia kwa ule muda ambao utakuwa na uhitaji (maombi ya akiba)
Wekeza maombi yako kwa wenzako kama kijana, haijalishi wao wakoje we waombee tu
kila siku. Usimalize siku bila ya kuwaombea wengine. Unapoombea wengine Mungu anaangalia hitaji lako na kukutimizia. 

Vya Kuzingatia
Tenga muda kwa ajili ya kuomba hata kama muda ni kidogo. Na kama huwezi kuomba basi anza kwa
kusoma Neno lake.

Kama huna hata cha kuomba ukiamka asubuhi basi unaweza hata kumsalimia tu _shikamoo Bwana Mungu
-Huwezi jua ni jinsi gani Mungu anatamani kukusikia kila siku ukimuomba au ukiongea nae japo kwa sekunde kadhaa.

Jazwa na Roho Mtakatifu ili akusaidie kuomba ili upate nafasi ya kunena hata dakika chache Usikubali kukata tamaa
Luka 18:1-8









No comments: