MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, February 07, 2019

KUPOKEA NGUVU YA KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU (KUTOKA MAHALI ULIPOKAA MUDA MREFU)



6. KUFANYA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU 

Waruni 8:26-2826 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. 28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 

Roho anakuombea kwa kuugua kusikoweza kuelezeka, na hayo hayafanyiki nje ya mwanadamu bali ndani ya mwanadamu. Kiwango ambacho usingeweza kukifikia wala kukiona Roho anaatamia moyo wako na unasikia kuugua pasipo weza kuelezeka.

Kuna namna ambayo unataka kuomba lakini hauwezi kufikia pasipo kuwa na Roho Mtakatifu ndani yako. Mwanadamu kawaida ameumbwa na aibu lakini Roho ndiye hawezaye kuomba kwa namna ambavyo mwanadamu kikawaida angeshindwa. 

Yohana 14:1616 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu

Hili Roho aweze kukaa ndani yako lazima umjue Roho Mtakatifu. Kuokoka siyo issue bali issue ni kumjua Roho Mtakatifu. Ni muhimu Roho aweze kukaa ndani yako hakusaidie katika hali unazopitia. Hali ya kukataliwa awezaye kukusaidia ni Roho Mtakatifu. Hali ya kutengwa na kunyanyapaliwa awezaye kukusaidia ni Roho Mtakatifu. Hali ya uzuni ndani yako awezaye kukusaidia ni Roho Mtakatifu. Ndiyo maana kuna watu ambao wameachilia huzuni ndani yako lakini kila siku wanakukuta na furaha kwanini? Kwasababu kuna Roho amekaa ndani yako ambaye anabeba udhahifu wako wewe na huzuni zako wewe. 

7. USALAMA UNAOTOKANA NA ROHO MTAKATIFU 

Roho Mtakatifu anakupa usalama wa ndani na si wa nje uliouzoea. Nje unaweza kuonekana huko huru lakini hauko huru. Unaweza kuonekana unafanya biashara na wakaona una mafanikio lakini ndani wamekusimamisha kimafanikio. Roho anatengeneza ndani anakupa uthamani ndani ambao mnatokeo yake yataonekana kwa nje. Watu wengi ambao kwa nje wanaonekana wako huru na wanamuonekano wa kufanikiwa Roho anaposhuka leo anaondoa vizuizi vya mafanikio yako. 

Mungu akikupa usalama wa ndani hakuna wa kukuzuia. Na leo Mungu aachilie usalama wa ndani ili uweze kufanikiwa kwa jina la Yesu. 

Kuna mtu ikimuangalia unaono kabisa anastahili kufanikiwa, lakini kumbe ndani yake ana usalama. Tunatumia gharama kubwa kulinda usalama wa nje laiti kama tungetumia gharama hiyo kulinda usalama wa ndani tungekuwa mbali sana. 

Wengi hawafunguliwi na kutoka mahali walipo kwasababu wanatamani yale ambao yamewafunga wayaone kwa macho ya nyama. Kama ambavyo unaweza kufunga mlango wa macho ya nyama ukiona hauwezi kufungua kwa macho ya Rohoni. Kama walivyokufunga kwa macho ya Rohoni nguvu itakayokuja ya Roho Mtakatifu itashuka kwa macho ya Rohoni. Nguvu ya Roho inashuka kwenye utu wako wa ndani na inaposhuka utasikia kwa nje kwamba kuna kitu kimeachiliwa kwa ndani. Utajiri mkubwa ni kuwa na Roho Mtakatifu kwasababu Roho anakila kitu. Ukisoma Biblia wakati Ibrahimu anakwenda kutoa sadaka ya Isaka Roho alimletea kondoo. Kama Roho anaweza kuleta kondoo uwe na uwakika Roho anaweza kuleta nyumba yako gari na vile vyote unavyo vitamani. 

































No comments: