MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 05, 2019

ADUI ANAYETAKA KUHARIBU MIPANGO YAKO INAVYOISEMESHA NAFSI YAKO



Unaweza kuomba na kama ni kibali ukapata lakini Baraka zako usizione. Wapo adui wavizihao njiani na wana mbinu nyingi kweli kweli. Adui hawa wanacheza na taharifa za mtu na wanazo njia mbali mbali za kupata taharifa za mtu. Huyu adui anaweza kuja kwa njia nyingi anaweza kuja kama rafiki ili apate taharifa na kukwamisha mchakato wako. Mara nyingi kuzimu inatumia mtu wa karibu yako kuchukua taharifa zako. Zipo njia nyingi ambazo adui wanazitumia na leo tunakwenda kutizama chache. 

Utashangaa umelala na mipango mizuri baada ya siku mbili imeharibika na ndipo utasikia mtu fulani ana mawazo mazuri lakini hafanikiwi. Aina hii ya maadui ni wabaya sana kwasababu wanavizia wakati mpango wako unakaribia kuiva. Adui anapoona hawezi kukuzuia wewe anamzuia yule ambaye alikuwa akufanikishe. Ndipo hapo utamsikia mtu akisema rafiki mipango yako imefikia wapi. Sasa leo tuangalie chanzo kimoja cha mtu kutoa taharifa ambacho ni WEWE MWENYEWE. Kujua mtu anawaza nini amepanga nini adui anaweza kujua na unaweza kujiuliza anajuaje? Wachawi wanaweza kusemesha nafsi ya mtu na ukasema yale yote uliyowaza na kupanga akajua na kukuvizia njiani. 

Unakuta na mtu na mipango mingi mizuri na una bidii lakini mipango yako haitekelezeki. Najua wapo wengi sana ambao wana mipango na haitimii. Biblia inajua wapo wachawi wa aina hiyo na wanaitwa wapandisha pepo. Nafsi yako inaweza kuvutwa na kupelekwa mahali fulani kwenye kikao na wakaoji na kujua kile ambacho unakiwaza. 

1Samweli 28:6-

Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. 9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? 10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. 13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. 


Mtu anapopandisha nafsi ya mtu anataka kujua ni kitu gani ambacho mtu anawaza au amepanga. Sauli anakwenda kwa mwanamke mmoja ambaye ni mpunga pepo na kuuambia ampandishie Samweli ili kujua kwamba aende vitani au asiende vitani. 

Mwanamke aliuliza ni nafsi ya mtu gani ambayo inatakiwa kupandishwa, Mwanamke alitaka kujua usalama wake ndiyo maana aliuliza. Samweli alikuwa nabii wa Mungu ambaye alikuwa kama kinywa cha Mungu juu ya mfalme. Wakati huu Samweli alikuwa amekufa hivyo wakati nafsi yake inapandishwa yeye alikuwa amekufa. Sauli alipoona kuwa ni Samweli amepandishwa akainama chini akasujudi kwasababu Samweli alikuwa si wa kawaida. 

Leo tunakwenda kuwapiga wapunga pepo kwa jina la Yesu na wanaozipandisha nafsi za watu. 

Kumbukumbu 18:10-14 
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo. 

Maandiko yanasema asionekane mtu atazamaye bao, wala atazamaye nyakati mbaya, hapa ndo utakutana na wale ambao wanasema nina yota ya nge, simba, n.k. Maandiko yanasema watu kama hao wasionekane. Na kutokuonekana kuna maana moja kubwa sana kwamba kutokuwepo mahali fulani kabisa kwa hiyo mtu wa namna hii hatakiwi kuonekana na kama uliwahi kushiriki mambo kama haya ni muhimu sana kuomba toba. Kwasababu si rahisi kupigana vita hii kama Mungu hayupo upande wako. 


No comments: