MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, February 16, 2019

KUPOKEA NGUVU YA AGIZO LA BWANA YESU. (Receiving the power of the Lord's command)



 ฿h o ₧  ₦   r u o v i   r € i 

Siyo wote wanaagizwa wanaweza kubeba maagizo na kuyatimiza. Kila unapoingia kwenye ibada Roho anachilia maagizo lakini si wote wanayabeba. Si unakumbuka ule mfano wa mpanzi ambao Bwana Yesu alisema na wanafunzi wake. Kuna watu wanapata maagizo kwenye ibada lakini hawayatimizi'''

Marko 16:14-20

Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Kila aliyeokoka na akaamini maana yake ana uwezo wa kuhubiri injili. Kama haujahubiria mtu na akaacha dhambi na kumwamini Kristo haujazaa matunda. Petro akauliza sisi tumeacha vyote tutapata nini? Waliacha vyote kwaajili ya kuwafanya mataifa kuwanafunzi wake.  

Mungu anataka ufuate agizo leo lakuwafanya mataifawawe wanafunzi wake. Ukiwa unatoka nyumbani kwenda kanisani toka na wazo la kuokoa watu kwaali ya injili. 

Kati ya watu ambao wamechukia kukusanya wenye dhambi kanisani ni walokole. Haiwezekani mwaka mzima tangu Moja mapaka thelathini unashughulika na maisha nyako tu. Petro alipewa fungua za ufalme wa mbinguni na kinachojenga Jenga ufalme wa mbinguni ni watu kutubu dhambi zao. Si kazi nyepesi kugeuza akili ya mtu na kumrejea Bwana si funguo za kawaida. Ukishamfungua mtu kufungua biashara yako ni kazi ndogo tu kwasababu ni akili yako mwenyewe. 

Ukishaamini jina la Bwana wa majeshi ndipo pepo anatoka. Usipoliamini neno la Bwana hakuna ishara ambayo utaiona kwako. Mama mmoja ameshuhudia hapa alifunguliwa kupitia neno la Mungu, neno ndilo linaweza KUKUSAIDIA, siyo maombi. 

Sikiliza nikueleze naweza kukuombea na ukapona lakini usipokuwa na neno ndani yako ukifika nyumbani tu hauna neno unarudia tena hali ya kwanza. Maandiko hayasemi watu wake wanapotea kwa kukosa maarifa si kwakukosa maombi. 

Ni muhimu sana kuwa makini wakati wa neno kuliko wakati wa maombi, neno litajenga imani kwako na ndipo utaweza kuomba vizuri. 

Maandiko yanasema utasema kwa LUGHA MPYA. Sasa ni aibu kwa mlokole usiponena kwa lugha. Hupo kanisani miaka mitatu wala hauneni kwa LUGHA  ni hatari. Uchanga wa mwisho ni mtu kutokunena lugha. Unaponena kwa LUGHA unaijenga nafsi yako mwenyewe. 

Ukishanena kwa LUGHA unakuwa na nguvu ya kushika nyoka kwa maana ya kushika uchawi, waganga, nyoka na kazi zote za shetani. 

Hata wakiweka matambiko yao kwenye chakula hautakufa kwa jina la Yesu. Sasa kwenye eneo hili kuna watu wanamjaribu Mungu. Roho amekuambia usile chakula hicho wewe unaanza kukitakasa kwa Damu ya Yesu sikiliza utakauka pale pale. Roho Mtakatifu yupo ndani yako kwaajili ya kuachilia maelekezo kwenye maisha yako, ni muhimu sana kusikia.

Ķώά мғάήό

Roho amesema na wewe kwamba usile chakula ndani kwako (kwenye familia) na akasikia hilo tu, leo haujala chakula siku tatu haujakula chakula lakini hautoi suluhisho ni kitu gani cha kufanya. Hapo kutakuwa na familia kweli Ni muhimu kusikia ili kufuata maelekezo sawa sawa. Kazi ya Roho ni kupatanisha na watu waishi kwa Imani.

Ni muhimu sana kushika maagizo unayoagizwa sana sana kwenye Madhabahu ya Bwana. Kama haushiki maagizo unayoagizwa unategemea kutoka vipi kwenye hatua uliyopo. Kuna faida gani kuambatana na madhabahu ambayo haushiki maagizo yake.


No comments: