Tunaendelea na somo letu na tunaenda kuangalia tena mapepo kadhaa katika somo hili.
Aina ya Sita Pepo wa uongo.
Huyu pepo anatenda kazi ndani ya mwili wa wanadamu. Tuliona kibiblia namna ambavyo pepo wa udhahifu unapoingia ndani ya mtu anaonekana dhahifu hata vile vitu ambavyo anavifanya, iwe kazi, biashara au masomo.
Pepo wa uongo anageuza maneno yale uliyoambiwa na kukuonyesha kama ni uongo. Kama Maandiko yanasema kwa kupigwa kwake umepona pepo wa uongo anakuambia utaponaje huo ugonjwa.
2 Mambo ya Nyakati 18:21-24
21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo. 22 Basi sasa, angalia, Bwana ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye Bwana amenena mabaya juu yako. 23 Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya Bwana ili aseme na wewe? 24 Mikaya akasema, Angalia utaona siku ile, utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche.
Huyu ni pepo lakini anaitwa pepo wa uongo. Usipoelewa haya mambo unaweza kupiga mizimu, na kila laana lakini unashangaa hauna mafanikio. Kazi ya huyu pepo ni kugeuza mtazamo halisi wa Mungu kwenye maisha yako ili uonekane muongo. Pepo wa uongo ataambiwa funga wiki nzima kwaajili ya maombi na kwasababu pepo wa uongo anajua kabisa ukitekeleza kuna hatua utavuka. Siku ya kwanza utafunga inaweza kuwa mpaka ya nne ghafla pepo la uongo linaanza kukudanganya ili uache maombi na kwenda kwenye kazi, biashara. Maandiko yanasema pepo wa uongo akawaendea manabii, na tunajua fika manabii ni watumishi wa Mungu lakini haikusababisha pepo wa uongo kutokuingia ndani yao.
Pepo wa uongo anabadilisha mawazo yako na kukufanya uingiwe na msongo wa mawazo. Wazo la Mungu linakuja ndani yako kwamba uende banki na kuchukua mkopo kwaajili ya mradi wako, lakini pepo wa uongo anakuonyesha utashindwa kulipa mkopo. Ngoja niongee na mabinti ambao wanataka kuolewa unakuta kuna watu wawili au wanne wote wanataka kukuoa. Sasa usipokuwa makini utaingia mkenge na unaanza kuomba lakini katikati ya wale kuna ambaye ametumwa kwaajili ya kuharibu maisha yako. Na wale wenye pepo wa uongo wanajali kweli kweli, nisikilize Mume mwema au mke mwema anatoka kwa Bwana. Mungu ambembelezi mtu bali anamuagiza ili haifuate njia yake lakini kwa shetani nitofauti atakubembeleza. Shetani ana kawaida ya kubembeleza ukiwa nje lakini unapoingia ndani au kuanguka katika mtego wake akubembelezi tena itakuwa kilio na kusaga meno.
Uongo ndiyo unafanya kazi sana katika maisha ya wanadamu na ndiyo maaana shetani anaitwa baba wa uongo. Ukishinda uongo utakuwa umeshinda mengi sana kwasababu unaweza usiseme uongo ila ukashiriki kufanya uongo wa kudanganywa na ukanaswa. Ujasikia wamama wakilia na kusema huu si mpango wa Mungu kuwa na wewe. Maana yake ulinasa kwenye mtego wa shetani unasema ninasema kitu gani fungua Kumbukumbu la Torati 28 utaona namna ambavyo ulinaswa.
Utakaposikia sauti ya Mungu wako na kutunza, ukisikia maagizo ambayo Mungu ameyaachilia kwako kwa wiki nzima maana yake ndipo utakapofanikiwa. Lakini shetani anakuletea mawazo mengine tofauti kabisa, tofauti na yale Bwana alikupa wiki nzima. Mungu anakuambia ushike maangizo yake lakini pepo wa uongo anakudanganya na unasikia sauti yake. Tunayo vita na wala haitakaa kuisha kwasababu pepo wa uongo anatokea kwenye mawazo yako na hakuna wakati utaacha kuwaza. Kumbuka jambo moja muhimu sana pepo wa uongo akitoka hautasikia kelele bali mawazo yako yanabadilika na kuanza kusema kweli. Uovu hauwezi kuingia ndani yako pasipo kuwa na wazo la uovu. Kama hauna wazo la uovu na uovu ukaja kwako utaukimbiza haraka. Kuna msema wa kilugha cha nyumbani kwetu unasema “wakodwe kare waigimira mwire” Maana yake unasukuma mtu anakoelekea huko. Kama wazo la uovu lilikuwa ndani yako na akatokea mtu analikamilisha. Ujawahi kuona mdada analipiwa nauli anaanza kujiweka vizuri anajua tayari amependwa, maana yake alikuwa na wazo la uovu ndani yake.
Hakuna mtu ambaye hauongozwi na mawazo yake kila kitu kinaanza kama wazo, hata Tanzania tunatawaliwa na mawazo ya watu. Waliweka sera zao mbele na tukazikubali na kuwachagua kwa hiyo tunayoyapata ni yale ambayo yako kwenye sera. Ndivyo ilivyo kwa sisi wakristo tunaongozwa na sera za mbinguni ukitaka gari unaangalia sera inasemaje, ukitaka afya njema unaangalia sera inasemaje. Shida kubwa ambayo tunayo ni kuifuata sera ya Mungu na ndipo maandiko yanasema utakapoisikia sauti yake “Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.” Hii ni sera ya Mungu maana yake anakupigania na kukutunza. Sasa pepo wa uongo anaingilia hapa anakuambia hivi unaweza kuishije bila kutenda dhambi. Muulize mwanzako unaweza kuishi pasipo dhambi, hata walokole utasikia wakisema haiwezekani. Nisikilize Bwana anahitaji uwe Matakatifu na usitende dhambi kabisa na inawezekana. Wengi hawaelewi watashindaje dhambi nisikilize ukishinda mawazo umeshinda dhambi unachotakiwa kushindana nacho ni mawazo kemea mawazo kabla ya kukeme dhambi. Ukiruhusu wazo lipite na kukutawala hautamuondoa shetani, ndiyo maana kuna watu wanamkemea shetani mpaka wanafika kwenye tukio. Unaenda kuchukua rushwa unasema kama ni Mungu na wala si mpango wake arudi nazo, Mungu hayuko namna hiyo zitaingia kwenye mikono yako na si wazo la Mungu ndani yako. Sikiliza Gidioni alimuambia Mungu kama umechagua niende vitani naomba ishara na akuomba ishara akiwa vitani. Si unakumbuka wakati anashindana na mawazo yake na anasema Mungu mimi ni mdogo na Familia yangu au kabila langu ndilo dogo. “Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu” Baada ya hapo Gidioni akamuomba Mungu ishara ili ajue kama ni Mungu anayemuagiza “Gideoni akamwambia Mungu, Ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema, tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema. Ikawa hivyo; kwa maana aliondoka asubuhi na mapema, akaikamua ile ngozi, akautoa ule umande katika ile ngozi, bakuli zima la maji. Gideoni akamwambia Mungu, Hasira yako isiwake juu yangu, nami nitasema mara hii tu; nakuomba, nijaribu kwa ngozi hii mara hii tu; sasa ngozi tu na iwe kavu, na uwe umande juu ya nchi yote. Mungu akafanya hivyo usiku ule; maana ile ngozi tu ilikuwa kavu, napo palikuwa na umande juu ya nchi yote”
Mwangalie yule mtu wa Mungu Elisha na mtumishi wake Gehazi wakati Elisha amekataa zawadi za yule Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu. Gehazi pepo la uongo lilimuingia na akatamani vile vitu baada ya bwana wake kuvikataa. Gehazi alijua kwamba Elisha atajua akaenda na kumdanganya Naamani na kuvichukua vile vitu na yakampata mabaya. 2Wafalme 5: 20-27“20 Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. 21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? 22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. 23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake. 24 Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. 25 Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. 26 Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? 27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji”
Chukua sadaka yako tuombe na usikubali pepo wa uongo hakudanganye kwamba unaponenea sadaka yako hakuna jambo litatokea. Uzima na mauti upo kwenye kinywa chako shetani hasikudanganye kwamba hiyo sadaka ni ndogo umemtania Bwana. Tamkia sadaka yako na unachokiomba ndicho kinatokea. Usitoe sadaka pasipo kuinenea sadaka yako. Ndiyo maana maandiko yanasema andaa sadaka yako hata mkono wako wa kushoto usione. Nena juu ya sadaka yako umesoma sera yako ya mbinguni na unajua namna ambavyo inasema. Tuko kwenye ulimwengu ambao tunashindana na yule mwovu ambaye ni baba wa uongo.
No comments:
Post a Comment