Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila
Somo lililopita nilisema kwamba hizi ndoto zinakuja kwa sura ya mwanamke au mwanaume. Na wanazini na wewe kabisa ukiamka ni uhalisia kabisa. Wengi wameishi katika hali hiyo na kuona kwamba ni kawaida tu. Katika hatua ya pili tutaona namna ambavyo wengine wameishi na mapepo ndani yao na wanaona kawaida tu na aina za mapepo hayo. Mapepo yanayo majina yake na kwenye Biblia yapo kabisa na ndiyo maana leo tunakwenda kuyatembelea kwa jina la Yesu.
Tumepewa mamlaka juu ya pepo wachafu na leo wanaondoka kwa jina la Yesu.
Walawi 20:6
Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.
Hawa ni wanadamu lakini ndani wana uchawi na wewe umekwenda na kuzini naye maana yake ile Roho yake umeibeba na maandiko yanasema ile Roho yake utaibeba. Zamani walikuwa wanatengwa lakini sasa tupo nao pamoja na wanakuja hata makanisani, usipokuwa na Roho mtakatifu ndani yako unaweza kuangamia katika mitego yao.
Maombi
Sema kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu pepo lolote nililolipata kwa njia ya kuzini na wachawi toka kwa jina la Yesu. Achia mwili wangu kwa Damu ya Yesu, ninakutoa ndani yangu na kila uharibifu ulioufanya ninaachilia Damu ya Yesu. Amen
Unaweza kujua kwamba wewe unamtumikia Mungu na kumuamini Mungu lakini kumbe kuna mahali uliungamanishwa na haya mapepo. Agano la kale mtu mwenye pepo au uchawi alikuwa anatengwa na watu au kupigwa mawe hadi kufa. Lakini Bwana Yesu alipokuja haupigwi mawe tena bali pepo anatoka kwa jina la Yesu. Neema ya msalaba umeturudishia uhai tena kwa jina la Yesu.
Tulipewa mamlaka kwenye Marko 6:7
Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
Ndiyo maana shetani akisikia Damu ya Yesu anatetemeka maana anajua anaharibiwa kwa Damu ya Yesu. Mapepo haya tunayoyapiga leo lazima uone matokeo kwenye maisha yako kwa jina la Yesu.
Maombi
Kwa jina la Yesu ninayo amri juu ya mapepo wachafu kwenye ulimwengu wa Roho kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu, pepo mchafu toka kwenye maisha yangu, ndoa yangu, uzao wangu, kazi yangu, karama yangu, shamba langu, ajira yangu kwa jina la Yesu.
Pepo mchafu anapokuwa ndani ya mtu unaonekana haufai, lakini anapotoka utafaa, kazi yako itafaa, kwa jina la Yesu.
Hii ni aina ya kwanza ya pepo anayetesa maisha ya wanadamu anaitwa pepo mchafu.
Aina ya pili ni pepo Bubu Marko 9: 17-18, 25
17 Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 18 na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. 25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
Pepo Bubu kazi yake ni kukufanya usifae mbele za watu kuwa na kauli mbaya mbele za watu. Anakamata kinywa chako mbele za watu ili usionekane unajua kitu. Anaweza kufunga kinywa chako usiongee kabisa au kama unaongea usiongee maneno yanayofaa mbele za watu. Utasikia wakisema huyu naye kaongea nini. Kama ni kwenye biashara yako utashangaa mtu anaanza kuuliza za siku nyingi badala ya kufanya biashara pepo huyu anapoteza muda wako.
Pepo huyu akiwa kwa wanandoa ndiyo hatari zaidi, mwenzako hajasema utasikia ukisema umenidharau, umenitukana huyo ni pepo bubu yupo kazini kwaajili ya uharibifu.
Aina ya Tatu pepo kiziwiMarko 9:25
Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
Pepo huyu anashughulika na masikio, anaweza kufunga ili usisikie au kubadilisha kile ulichokisikia. Kuna watu wanabadilishiwa habari anasikia lakini ukimuuliza hanabadilisha na kusema kingine. Kuna wengine wanasikia kelele tu maana yake pepo kiziwi amebadilisha masikio. Ndiyo maana maandiko yanasema wana masikio lakini hawasikii, kwanini kwasababu yupo pepo kiziwi aliyeziba masikio yako usisikie neno la Mungu. Kama usipojua mapepo haya yataendelea kukaa kwako na utashangaa unagombana na watu kila mara.
Aina ya nne ni pepo wabaya.
Luka 7:21
Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.
Hawa pepo wakiinga ndani ya mtu wanamgeuza awe mbaya, unaonekana mbaya tu. Hawa pepo wameandikwa ndani ya Biblia ili wewe uweze kuushinda huu ufalme wa mapepo ya aina hizi. Elewe kitu kimoja kila mtu analo jina lake na hauitwi kila jina kuna jina lako maalumu na ndiyo maana tunajua aina hizi za mapepo kwa majina yao ili unapoomba moto unawafikia moja kwa moja kwa jina la Yesu.
Wakati Yesu alikuwa anaomba alikuwa anataja kabisa aina hizi za mapepo hakuwa anakemea jumla jumla tu kwamba pepo toka la hasha! Kama ni pepo mchafu alisema kama ni pepo wa udhahifu alisema na wakatoka kwasababu alitaja majina yao, maana yake aliwajua.
Aina ya tano pepo wa kuvua nguo Luka 8:27
Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini.
Aina hii ya pepo inawatembelea wadada sana na wanavaa nguo zinazo muweka nusu uchi. Wengine mnamuuliza kwani haoni aibu yule pepo amemfunika ili haone yuko sawa. Huyu pepo wa aibu anaaibisha sana wadada kwasababu akitulia utashangaa mtu anaanza kuvuta nguo kujifunika ili asiaibike wakati alivaa mwenyewe nguo hiyo. Unaweza kukutana na picha ya mtu ukaanza kujiuliza huyu ni mwanadamu au myama. Aibu ikiondoka ndani ya mtu anakuwa kama myama kabisa. Aibu hii ilianza kwenye bustani ya Edeni, Mungu aliachilia hofu kwetu wala si aibu. Kama Mungu asingeachilia aibu watu duniani wengetembea uchi na kwasababu ya aibu hii ndipo unakuta wamama wanaongea, wazee wanaongea, serikali inaongea.
Aina ya sita Pepo wa udhahifuLuka 13: 11
Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.
Pepo huyu ni waajabu sana akiingia kwenye maisha yako. Unaweza kuwa mgonjwa na wala si mgonjwa. Kuna watu ambao hawawezi kutibiwa mahali popote, unaenda hospitalini mwili unauma, mifupa inauma lakini ugonjwa hauonekani. Pepo ili likihama ndani ya mwili wako linaingia kwenye kazi yako, unashangaa unafanya kitu lakini watu hawakione unaulizwa saa yote unafanya kazi hii tu. Lakini akifanya mtu mwingine akaonekana na kusifiwa sana tena ndani ya dakika chache. Unaweza kupiga makata na akaitika lakini pepo wa udhahifu unaweza kuishi naye miaka yote lakini yakanyamaza kimya.
Unaposoma Luka 13:12-13 maandiko yanasema hivi “12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. 13 Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.”
Unaona namna pepo wa udhahifu alivyo, aliondoka kimya kimya bila kupiga kelele kwa hiyo kuna mapepo wanaondoka kimya kimya bila kupiga kelele. Kwa mfano pepo wa uongo hawezi kupiga kelele bali mtu anabadilika na kuanza kusema ukweli. Kwa hiyo usidhani kutokuanguka nisababu ya kutokuwa na pepo linaweza kuwepo na kuondoka bila wewe kujua, utakachokiona nimabadiliko ya tabia fulani ndani ya mtu.
Ukiwa na nguvu ya Mungu ndani yako unaweza kuingia kwenye ofisi ya mtu ukashangaa wanashindwa kuimili ile nguvu uliyobeba na mapepo wanaanza kupata shida.
Ngoja niishie hapo nitaendelea na aina nyingine za mapepo kwenye kipindi kingine kaa mkao wa kupata maarifa yakutosha ili kuweza kupigana na aina hizi za mapepo. Maana ukijua na kupiga mapepo haya kuna hatua kubwa sana utavuka kwenye maisha yako.
No comments:
Post a Comment