MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 24, 2020

HATIMA YA MTU HAIWEZI KUBADILISHWA


 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila.

 

21st June 2020.

 

Ili hatima yako iweze kwenda mahali wanafunga akili na ili hatima yako iweze kuwepo Mungu anafungulia akili.  Hatima a mtu anakwenda ana akili ya mtu kwa maana wakifunga akili yako wamefunga hatima yako.

 

Kuna mtu ambaye yuko karibu yako ambaye angeweza kusaidia ili ufike kwenye hatima yako lakini hauwezi kumuona.

 

Marko 5:2-20

Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. 11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. 12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. 14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. 16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. 17 Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. 18 Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; 19 lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. 20 Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.

 

 

Adui akigeuza hatima ya mtu na makao yake yanabadilika. Huyu ni mtu ambaye alikuwa na jamaa na ndugu lakini makao yake yalikuwa makaburini. Wanadamu wanaposhindwa ndipo Mungu uuanza kazi. Huyu jamaa alikuwa maefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo kama vile ambavyo wewe wamekushauri mara nyingi, wamekupa mtaji mara nyingi lakini wameshikilia hatima yako.

 

Walimuacha huyu jamaa kaburini na walimkuta na Yesu, waliokuacha kwenye utasa wakukute na mtoto wako, waliokuacha kwenye umasikini wakukute na utajiri wako. Waliokuacha kwenye ugomvi wakukute kwenye Amani.

 

Walipofunga akili za huyu ndugu aliingia makaburini lakini akili ziliporudi aliketi miguuni pa Yesu huku amevaa nguo. Watu wanarogwa ili wafungwe akili zao na akifungwa akili unakuwa si mtu wa kawaida kwa maana akili yako imefungwa (Wagalatia 3:1).

 

Huyu mtu amabye alikuwa anaishi makaburini ambaye alikuwa ana akili na aliishi makaburini alipotaka kwenda na Yesu akamwambia aende kuhubiri kwa maana yeye alikuwa ni chombo. Huyu muhubiri mkubwa sana lakini alikuwa tayari yupo makaburini.

 

 

 

 

 

No comments: