MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 24, 2020

IDARA ZA MASHETANI ZINAZOSABABISHA KUZUIA HATIMA YA MTU


 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila.

 

23rd June 2020.



Upo kwaajii ya kutimiza kusudi la Mungu la kuumbwa kwako na kwasababu hiyo shetani na yeye anataka kuzuia hatima yako hili isiweze kutimia. Hivyo basi zipo idara ambazo anazitumia kwaajili ya kuzuia hatima ya maisha yako. Na tutatembea idara hizo kwaajili ya kuziangamiza kwa jina la Yesu. 

 

Biblia inasema watu wa Mungu wanaangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6) hivyo basi shetani anazo mbinu nyingi sana ambazo anatumia kwaajili ya kushindana na wewe. Kwa hivyo kila unapoongeza maarifa maana yake kuna kitu kinaongezeka ndani yako kwaajili ya kumshinda shetani. Shetani haumshindi tu kwa kuomba bali kwa maarifa unayoyapata na kutembelea pale ambapo ameshikilia kwenye maisha yako. Ukijua ni wapi ambapo shetani ameshikilia kwenye maisha yako jua kwamba ni rahisi kutoka hapo.

 

IDARA YA KWANZA

idara ya mateso

 

Kawaida shetani uwa anaachilia mateso kwa mwanadamu akiwa anaamini kwamba mwanadamu hawezi kuvumilia mateso kwa muda mrefu. Mwanadamu akuumbiwa kuvumilia mateso na yameingia tu au ameyabeba kwasababu ya dhambi. Jukumu ambalo limeingia kwenye maisha ya mwanadamu si la kwake na wala mwanadamu hakuumbiwa kuyabeba mateso wala maumivu kwenye maisha yake.

 

Ni kawaida kwamba kila jambo lina matumizi yake kama vile kuna magari ya kubeba mizigo na kuna ya kubeba abiria (yapo kwaajili hiyo kazi tu). Vile vile na mwanadamu hakuumbiwa kubeba mateso na ukibeba kwa muda mrefu lazima uangamie au kupotea. Idara hii anaitumia shetani kuzuia watu wasikifike kwenye hatima: -

ü  Mateso ya umasikini

ü  Mateso ya kukataliwa

ü  Mateso ya magonjwa

ü  Mateso ya njaa.

 

Mahali ambapo umefikia na kuona kwamba moyo wako umelemewa ndiyo mateso ambayo tunaongelea.

 

Kutoka 3:7-8

Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

 

 

Mungu anajua maumivu yako na mateso yako. Wana wa Israeli walimuuza Yusufu na wao wakabaki misri lakini hawakujua kwamba walipomuuza na kumpelekea Yusufu utumwani walikuwa wanajipeleka na wao. Walimpeleka Yusufu utumwani na akawa waziri mkuu na ikatokea njaa hivyo Yusufu ambaye alikuwa waziri mkuu akawapokea ndugu zake waliokwenda kufuata chakula. Walikwenda utumwani na walipokelewa kwa furaha ambayo ilikuwa ni furaha ya muda na walipokelewa na Farao ambaye alimjua Yusufu. Yusufu alipokufa akaibuka asiyemjua na ghafla maisha ya wana wa Israeli yakabadilika na kuwa mateso.

 

Farao alipoinuka akasema tuwatende watu hawa kwa hila na wakafikia hatua ya kuua watoto wa kiume. Lakini ashukuruwe Mungu kwasababu ya Mama yake Musa mbaye alimficha Musa kwa ujasiri ambaye alikuja kuwaokoa wana wa Israeli. Hatima ya musa haikuzuiliwa na hata alipokuwa kidogo mama yake alimuweka kwenye kisafina na kumpeleka mto Nile ambapo Binti Farao alimuona na akasema atafutiwe mwanamke wa kiebrania ili amyonyeshe. Walipomtafuta wakampata mama yake Musa ambaye alikwenda kumyonyesha mtoto wake bila wao kujua.

 

Mungu aliyaona mateso ya wana wa Israeli hivyo aliandaa mkakati wa Musa ambaye anatakiwa kuwaokoa wana wa Israeli. Wakati wa kutengeneza safina walijua kwamba Musa aingeishi kwasababu tayari tangazo la kuua watoto wa kiume lilishapita.

 

Musa yuko kwenye ikulu na anayonyeshwa na mama yake na anaweza kujua kwamba mama yake alivyokuwa anaongea na Musa kwamba wewe ni Muebrania siyo mmisri. Wamama wanajua namna ambavyo wanaongea na wa watoto wao wakati wa kunyonyesha au wakati wa kuwapembeleza. Na wewe ni ukoo wa Ibrahimu wewe siyo mmisri bali ni muebrania ambaye unatembea na ahadi na agano la Bwana. Muebrania unaweza kumtesa lakini hauwezi kumuua.

 

Inawezekana wamekutisha na ukoo uliozaliwa ukoo wa babu yako, lakini leo waambie mimi ni ukoo wa Isaka na Ibrahimu na mzaliwa wa kwanza ni Yesu. Musa alikuwa kwenye Ikulu ya Farao na alipofikia umri Fulani alikutana mmsiri na mwembrania wanapigana na akamkamata mmisri akamua. Ndiyo maana nasema wewe siyo wa kwanza kuombea mtaa mzima ukitaka wawe salama. Kawaida ya mwembrania yeye aangalii maisha yake bali anatetea ndugu zake. Musa akaanza kuishi pale na akaanza kusikia habaroi zake kwamba ameua ameua akakimbia na Mungu alimuandalia mtu wa kumpokea ambaye alilinda maono yake.

 

Musa akatokewa na Mungu kwenye maono katika kijiti ambacho kilikuwa kinawaka akiteketei moto. Na Bwana anamuambia arudi kwa Farao kwaajili ya kuokoa wana wa Israeli. Aliondoka akiwa mkimbizi na anarudi kama mkombozi.

 

2 Thethalonike 1:6 -7

Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; 7 na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake

 

Wale walioandaa mateso kwenye maisha yako ni haki yakow ewe kuwalipa mateso. Unaposhughulikia hii idara ya mateso usiogope kuwarudishia wao ni haki yako kabisa. Ni haki kuwalipa mateso wale wanaokutesa. Kwenye idara hizi Mungu anakwenda kugeuza maisha yako lakini pia atakwenda kugeuza maisha ya adui zako. Mungu anakuja kwa majira yake kwenye majira ya kuokoa utuma neno la kuokoa, kwenye majira ya kubariki utuma neno la kubariki.

 

Kuna wakati umetesw ana maadui zako walifurahia lakini kuna wakati wao wanapokuwa wanalipwa mateso yao wewe utakuwa na furaha hasiye kuwa na heshima ataheshimika na aliyekuwa na heshima atashushwa. Kila mtu anapata haki yake kwenye kushughulikia hili swala la Idara. Adui zako watapata haki yao na wewe utapata haki yako. Usishangae utakapoona kila mlango unafunguka ni Mungu amekupa haki yako.

 

 

 

 

 

 

 

No comments: