Na Pastor Lambart Ileta
Uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka siku zote wanapigana na usiogope vita kwasababu utashinda hiyo vita kwa jina la Yesu. Mbingu imewekwa kwajili yako na lazima ushinde kwa sina la Yesu.
Unaweza kuchanganyikiwa pale unapoambiwa uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka. Unaweza kudhani uzao wa nyoka ni wale walio porini hapana. Uzao wa mwanamke na uzao wa Joka vinatenda kazi ndani ya mtu. Utakutana na mwanadamu huyu wa kawaida unayemuona lakini ndani yake amebeba joka. Ni wanadamu hawa hawa tunaoishi nao duniani lakini ndani kuna uzao wa mwanamke au uzao wa nyoka. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema yule ambaye amekubali kuokoka na kumkubali Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Uzao wa nyoka unaweza kubadilika na kuwa uzao wa mwanamke.
Ukiwa uzao wa mwanamke unapewa mamlaka ya kukanyaga nguvu ya nyoka na ng’e. Uzao wa mwamake haukulaaniwa bali aliyelaaniwa ni joka na ndiye anayesambaza laana.
Tuangalie neema ambayo iko juu ya mwanamke na uzao wake dhiki ya uzao wa nyoka. Ufunuo 12:1-61 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. 2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. 3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. 4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. 6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
Huyu mwanamke kabla ya kuzaa tunaona neema ilikuwa juu yake, tunaona ana jua juu yake na mwezi chini yake kwa maana amepewa utawala wa kushinda giza na kazi zake. Vile vile huyu mwanamke alikuwa na nyoka kumi na mbili. Nini maana ya nyota? Ni malaika waliokuwa wanamlinda huyu mwanamke usiku na mchana. Tunapoongelea uzao silazima uwe uzao wa tumbo la mwanamke tu hapana kuna uzao wa Baraka vile vile.
No comments:
Post a Comment