ռǟɮɨֆɦօքɖǟռӄTօռʀʊɖօʋɨCӄʀաɛɨӄɨʟǟ
Leo tunaangalia namna ya kuharibu uzao wa majini kupitia ndoa za majini. Kwa wale ambao wameshasoma masomo yaliyotangulia katika vipindi vitatu utajua nazungumza kitu gani. Tuliona namna ambavyo uzao wa mwanamke Ni dhahiri na vile vile uzao wa nyoka.
Nyoka huwakilisha adui, hiyo ndio maana nyepesi ya nyoka katika ulimwengu wa roho.
Tangu Mwanzo kabisa tunaona MUNGU akitangaza kwamba kutakuwa na uadui katika ya uzao wa Mwanamke na uzao wa nyoka
Mwanzo 3:15
nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Siwezi kurudi nilipotoka ila unaweza kupata masomo yaliyopita maana tulipo toka ni mbali kidogo.
Watu wengi hawaelewi kwanini Wafalme wa kale walikuwa wanaoa mabinti bikira. Kuna namna ambavyo mtu anaungamanishwa anapozini na mwanaume. Ndiyo maana Yesu alizaliwa na Bikira ambaye bado hakuungamanishwa na mtu yeyote. Check yule uliyemuoa kapita kwa John, Yakobo, Yusufu, na wewe unayeishi naye, inawezekana kabisa umeoa mwili tu lakini yeye alichukuliwa na John kitambo. Najua vijana mnanisikia mjiandae kwa nyundo zakutosha ijumaa ya wiki hii.
Kama apataye mke anapata kibali sasa Kama huyu alizini na watu 20 Ni yupi mwenye kibali maana wote umeungamanishwa nao. Sasa ngoja nikuambie jambo kama ulikutana na mganga wa kienyeji na ukaishi naye alibeba sehemu yake. Kama ni Mchungaji mke wangu anaitwa Mama Mchungaji maana yake ana sehemu yangu, ndani yake. Angalia mtu ambaye alipita kwenye mikataba ya aina hii ni kitu gani kinatokea kwao, hata amani ya ndoa inakuwa yashida sana, kwanini kwasababu tayari wapo watu wawili wanakumiliki.
2 Wakorintho 11:14
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Shetani anajigeuza kuwa kama mwanadamu lakini si nwanadamu. Kwa hiyo unaweza kuishi na mume au mke kumbe ni uzao wa joka. Kitakachokufanya kumjua nimatendo yake ya uovu.
1 Wakorintho 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Wengi wamekutana na majini mahaba na wanawatokea kwenye ndoto na wanajikuta Ni mambo halisi kabisa. Unaota unazini na mtu na unapoamka asubuhi unakuta hali hiyo ilikuwa halisi kabisa.
Unaona unapoingia kwenye mahusiano na uzao wa joka unakuwa mwili mmoja naye. Na wengi wamepitia haya wanakutana na watu na kuanza mahusiano bila hata kujua huyu ni
mchawi au la hasha. Utashangaa wakati watu wanafunguliwa namna walivyoungamanishwa na ndoa hizi.
Umewahi kuona wakati watu wanataka kuoana wanakuwa na kamati za sherehe na ndani yake kamati mbali mbali, lakini hakuna kamati ya maombi kwaajili ya ndoa. Check baada ya kufunga ndoa inakuwaje wanashindwa kuendelea mbele muda mrefu wanaanza kupigana ngumi.
Kama kibali chako kimepotea na umasikini umekujia leo kataa na kibali chako kitarudi kwa jina la Yesu.
No comments:
Post a Comment