ռǟɮɨֆɦօքɖǟռӄTօռʀʊɖօʋɨCӄʀաɛɨӄɨʟǟ
Mwanzo 3:15
nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Kuna uzao wa nyoka na kuna uzao wa mwanamke. Uzao wa mwanamke unaonekana kwa macho ya mwili lakini uzao wa nyoka hauonekani katika macho ya mwili na nyama.
Uzao wa nyoka unazaliwa na uzao wa mwanamke unazaliwa. Kuna wanaozaliwa kumbe ni uzao wa nyoka unamuona kama mwanadamu wakawaida kumbe ni uzao wa nyoka.
Yesu alidhibitisha maneno haya ya uzao wa nyoka kwenye Mathayo 3:7
Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
Unaona Yesu anawaita uzao wa Joka, inamaanisha walikuwa wanaonekana kama wanadamu lakini ndani yao wanafanya mapenzi ya Ibilisi. Kwa hiyo walikuwa Kama wanadamu kumbe ni uzao wa nyoka. Yesu alikuwa anaona uzao wa joka na akawahoji nani aliwaonya kukimbia hasira ya Bwana inayokuja. Maandiko yako wazi juu ya sehemu ambayo Nyoka (Ibilisi) ameandaliwa ni jehanamu ya Moto.
Tuangalie mstari huu ili uweze kujua agano ambalo Mungu alifanya na wana wa Israeli juu ya wao kuoa na kuolewa na wenyeji wa nchi au wageni watakaoingia miongoni mwao.
Angalia agano ambalo lipo na kwanini ninasema hata ukitaka kuoa uoe mlokole au kuolewa na mlokole. Nataka uone kwanini maandiko yanasema mume mwema anatoka kwa Bwana ili uweze kujua Mungu alikuwa anamaanisha kitu gani. Tazama ukoo wa Yesu ilikuwa ni familia ile ile na wakaoana kwa mtiririko huo. Mathayo 1:1-17
Haujawahi kumuona mtu anasema nimemuona Mungu jamani akinitendea mema. Uliwahi kujiuliza alikutana wapi na Mungu akamtendea mema. Au haujawahi kusikia mtu akisema shetani ameinuka ndani ya familia yangu, uliwahi kujiuliza kwamba alimuona wapi shetani aliyeinuka ndani ya familia.
Hapa utajua ninachomaanisha unapokutana na mtu mbaya Mungu amekupa uwezo wa kutambua watu waliobeba Roho za Shetani. Na Jambo la ajabu unaweza kumbeba shetani na usijue kwamba umembeba.
Kuna watu ambao wao wanasiku ambazo wakiamka wanataka kugombana na kila mtu. Hii ni udhihirisho wa shetani kuwepo ndani yako. Ngoja niongee na wamama najua hapa watadaka kitu kuna wanawake wakishika mimba tu wanaanza kuchukia waume zao na wao wanaona Ni swala la kawaida tu. Hata mume naye anaona Ni swala la kawaida tu utasikia wakisema nikwasababu ya mimba tu atakuwa sawa baada ya miezi kadhaa. Sikiliza shetani amepanga kukutoa kwenye uwepo ili uweze kuzaa kilicho chake. Ndiyo maana unaona kawaida mpaka shetani atakapo weka ngome yake na falme zake.
Ngoja nijaribu hivi tena, wakati Esau na Yakobo wako tumboni mwa mama zao. Rebeka alipata shida mpaka akaamua kwenda kwa Bwana hakukasirika alimuuliza Bwana. Sasa jiulize wamama wa leo wanatoa wapi ile hali ya hasira ndani yao mpaka kumchukia mume kiasi cha kumsemea mabaya.
Mwanzo 25:22-23
Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Falme mbili zilishindana tangu tumboni mwa Rebeka. Ndiyo maana nasema ni muhimu sana kuombea tumbo la mama yako. Kuna hali zinaweza kuwa zilikuwepo wakati wa kuzaliwa kwako. Si Jambo lakawaida kabisa hizo hali zinamaana kwenye ulimwengu wa Roho. Yesu alikuja na kuzaliwa kama mzaliwa wa kwanza ili kwa Damu YAKE tuweze kukombolewa na kila laana ya mzaliwa wa kwanza toka tumboni. Kwa hiyo Kama kunalaana au mabaya yamepita hapo tunanyunyiza Damu ya Yesu ya agano jipya. (Waebrania 12:24).
Ndiyo maana Bwana aliwataka wazaliwa wa kwanza kwenye Madhabahu zake sasa usifikiri shetani naye alikaa kimya anajua nguvu ya tumbo la mwanamke na yeye akawataka wazaliwa wakwanza. Inawezekana kabisa umeombewa sehemu nyingi lakini haujafungunga ninao uwakika katika Damu ya Yesu kwamba laana hiyo inaondoka leo.
Ngoja nikupe mfano huu,
Kama uliwahi kuwaona wale wafungwa wa zama za kale waliokuwa wanafungwa cheni kuanzia wakwanza mpaka wamwisho, kwa hiyo ukitaka kukata cheni nikazi kidogo. Cheni inafungwa kwenye shingo, miguu na mikono. Ndivyo shetani anavyofanya kazi kwenye ulimwengu wa Roho anawafunga watu kweli kweli.
1 Yohana 3:9-10
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Unaona watoto wa Mungu nidhahiri na watoto wa Ibilisi nidhahiri. Unamuona mtu wakawaida tu lakini kumbe ndani yake amebeba ufalme wa shetani.
Nakuonyesha mitego ya adui anayotumia kupitisha mitego. Wanawake wengi ambao wakiwa wajawazito check maneno ambao waume wanawaambia wake zao. "Mtoto sina uhakika naye kama niwakwangu" Maneno mengi yasiyofaa, kama usipojua shetani atapenyeza hila zake na kukamata uzao wako. Na Hali hizi zinaenda kizazi kwa kizazi, Bibi alikuwa na hali hiyo, mama, Shangazi, Dada kizazi kwa kizazi.
No comments:
Post a Comment