MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 19, 2019

PEPO WA UAGUZI


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


Pepo wa uaguzi anakuunganisha na mashetani, na kutokana na tatizo lako pepo wa uaguzi anakutuma ili kuleta vitu fulani fulani ili kukuungamanisha na mashetani. Kama ambavyo unakuja kwa Yesu na kusema nataka kuokoka kwa maana ya kumjua Bwana kama mwokozi wa maisha yako, hivyo tunatumia Damu ya Yesu ili kukuunganisha na kiti cha enzi cha Mungu Baba. 

Usipojua milango unaweza kuomba muda mrefu sana bila tatizo kuondoka. Unatumia damu ya Yesu ni kweli lakini kufungua nini? Unatumia nguvu ya Roho mtakatifu ili kufungua nini? Bwana anaachilia maarifa haya ili tuweze kupona na kuvuka kwenda hatua nyingine. Tunapoachilia Damu ya Yesu pepo wa uaguzi hawezi kuwepo, kwasababu ni damu yenye nguvu ambayo haikuwa na hatia yeyote lakini ilimwagika kwaajili yetu sote. 

Huyu pepo ndiye anatajirisha wanganga wa kienyeji kwa hiyo ukimpiga kwenye ulimwengu wa Roho kila aliyekamata cheo chako anaahia kwa jina la Yesu. 

Mwanadamu ametekwa katika sehemu tatu muhimu sana ambapo shetani akishikilia anatesa maisha yako;  
1.   Uchumi (mwanadamu uchumi wake ukishikiliwa anakosa raha na Amani)
2.   Afya (Mwanadamu hata awe na fedha lakini hakikosa afya ni bure tu) 
3.   Mahusiano (Mwanadamu hata awe na fedha na mali nyingi sana na afya kama ana mahusiano na watu ana Raha. 

Ukikomboa haya maeneo matatu ndani ya mwanadamu atakuwa mwenye furaha sana. Katika maombi yote ya mwanadamu analenga sehemu hizo tatu.

Matendo ya mitume 16:16-21


16 Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. 17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. 18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; 20 wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi; 21 tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.

No comments: