MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, February 19, 2019

NAMNA YA KUOMBA


Maombi ya toba na Moyo wa Toba.

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila 


U
naweza kuomba toba na moyo wako usiombe toba au mawazo yako yasiombe toba. Unaweza kuomba toba lakini usiwe na mawasiliano sawa sawa na Mungu. Elewa kitu kimoja mawasiliano tunayotafuta ni kama yale ya simu, unaweza kuwa na simu ya gharama lakini kama hauna laini ya mtandao ni kitu bure, na unaweza kuwa na line lakini kama hakuna network ni kazi bure tu. Unaweza kujipamba kwa nje lakini ukiingia kukamata mawasiliano ya kimbingu haupati mawasiliano kabisa. Uko kwenye maombi lakini ni mkavu kweli kweli hauna mawasiliano japo umejipamba kwa nje vizuri. Lakini mwingine yupo kawaida tu lakini netwok ipo wakati wowote mpaka unamshangaa huo uwepo anapata wapi. 

Line ndiyo moyo wako na simu ni kama mwili wako, line yako ikikosa network hata ukikaa kwenye mtandao hauwezi kupata mtandao. Kwa hiyo hata kama ukiwa karibu na Mchungaji au ukashikana na Mchungaji lakini hauna network kabisa. Hata ningekubeba mgongoni au kukupa koti langu uvae bado network itakosekana. Kuna watu ambao wapo mbali na mnara lakini network inakamata kweli kweli. Kwa hiyo shida si network ni laini (Moyo) uliyonayo. Unaweza kutoa sadaka ili ujiungamanishe na madhabahu lakini kama laini yako haiko sawa hata ulale madhamahuni utakuwa mtupu tu. 

Kuna watu ambao wakiinua mikono kwenye madhabahu ya Bwana anasikia uwepo wa hali ya juu. Maana yake moyo wake huko sawa na Mungu wake. Unaweza kufunga siku tatu au nne lakini bado ukaona uwepo haupo maana yake laini yako iko kwenye simu lakini haipo sawa. Kwa hiyo usijaribu kupiga simu kama haujahakiki kama network iko sawa. Unaweza kupiga simu lakini kama hakuna network hautaona mawasiliano. Unaweza kuomba kweli lakini je nguvu ya Mungu ndani yako ilikuwepo. 

Inawezekana kila mmoja anakwenda kanisani na ukiuliza kwanini unaenda kanisani jibu ni moja tu nimeenda kanisani ili kuabudu. Sasa si wote wanaingia kanisani kwaajili ya kuabudu la hasha! Kuna wengine wameingia kanisani kwaajili ya kuangalia watu wamevaa nini? Wanapigaje makofi na vitu kama hivyo, hawajaandaa miyoyo yao na mawazo yao kwaajili ya kupokea kwa Bwana kwa hiyo network erro. SASA USIJE UKANICHUKIA NI ROHO ANASEMA NDANI YANGU WEWE ZUNGUMZA NAYE NA UREKEBISHE NAYE UWE SAWA MBELE ZA BWANA KWAAJILI YA MAWASILIANO. 

Isaya 29:13
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; 

Waebrania 9:14
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

 Isaya 55:7
 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. 

  1 Wakorintho 3:9
 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. 

Shida si kumkaribia Mungu na kumuheshimu kwa kinywa chako. Unaweza kuingia kanisani na kumtukuza Mungu kwa kinywa chako kweli lakini shida iliyopo hapo moyo wa kupokea umefarakana na Mungu. Ukitumia akili yako wakati huko mbele Bwana lazima kuna vitu vitagoma ndani yako. Ukitumia akili inakutadhimini namna ulivyo, lakini Imani haikuonyeshi hayo. Ndiyo maana walimuambia Paulo hana akili kwasababu tayari alikuwa hatumii akili yake bali Imani. Ukitumia Imani unaonekana hauna akili kwasababu akili ikifika mhali inakataa kabisa. Warumi 1:28Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasaMuombe Mungu akupe Imani maana pasipo Imani hauwezi kumpendeza Mungu. Akili inapingana na chochote ambacho kinatokana na Imani. Ndiyo maana akili inafikia kipindi mtu anasema ana akili sana kwasababu amerithi kwa baba yake lakini siyo Imani. Imani haurithi bali unaipata kwa Bwana. 

Walokole wengi wanatumia akili kuliko Imani, Imani inapokea lakini akili haipokei. Ukitaka akili ifanye kazi unaangalia yule unayemuheshimu mbele yako lakini Imani inamtizama Mungu peke yake. Mungu alivyomuumba mwanadamu alimuwekea akili ili ujue nani umuheshimu. Na akili imeachiliwa ili uweze kujua namna ya kuishi na watu kwenye jamii. Wengi wanaomba kwa akilli na wala si kwa Imani. Akili haina matunda lakini Imani inayo matunda. 



Waebrania 10:22 
na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi. 

Kukaribia na moyo wa kweli si kwa akili. Haujawahi kuona mtu anakosea na yupo radhi alipie fedha yeyote lakini si kuomba msamaha. Mtu anaona fedha ni bora kuliko chochote. Akili ipo kwaajili ya mambo ya Duniani, kwa hiyo tumepewa ili kutumia Duniani na tunahitaji kutumia akili zetu kwa Imani. Ndiyo maana tunasikia kuna watu walifanya maamuzi ya haraka na matokeo yake ni ya hatari. Dhamira safi mawazo yako unayowaza mbele za Bwana yawe safi, kuna wengine wanakuja na dhamira mbaya mbele za Bwana. Unaomba tuba mbele za Bwana ili usamehewe na ufanikiwe kwenye biashara yako, si kwamba anaomba toba kwaajili ya kuwa msafi mbele za Bwana. Asilimia kubwa ya watu wanaookoka wana dhamira tofauti tofauti. Kuna wengine wamekuja kanisani wakiwa wanajua kwamba watapata fedha na alipokuja ghafla Yesu amemuokoa na anabadilisha dhamira ya ndani. Ukija mbele za Bwana usiwe na dhamira ya kutafuta vitu kupitia Mungu kwasababu Mungu autampata wala fedha hautaipata. 
Unapotoka kwenye toba ya namna hii inayofaa mbele za Bwana akili inaweza kukuambia Biashara yako haiwezekani leo lakini Imani yako inakuambai inawezekana kabisa. Hiyo ndiyo toba ya kweli mbele za Bwana. Unapotoka kwenye toba ya namna hii utakuwa safi na kuna hali itakusukuma ndani yako, tupa kile tupa hichi ili utakatifu uwepo ndani yako. Imani inageuza utaratibu ambao umewekwa na wanadamu, Imani peke yake ndiyo inaweza kugeuza utaratibu wa yale yanayoshindikana kwa akili yako. Akili zikibadilisha yale ambayo yamewekwa kiutaratibu huo inaitwa utapeli na kuna madhara ya utapeli. Imani inabadilisha utaratibu uliowekwa mbele zako na aliyeweka naye inabadilishwa na kukubaliana na yale unayoyosema. Wengi wanatumia akili wanasingizia Imani, nisikilize Imani hautajutia lakini akili kuna majuto mbele yako. AngaliaDanieli alipotumia imani na kuwabadilisha wote waliotumia wamuabudu Mungu wake. 


No comments: