MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 24, 2020

KUSHUGHULIKA NA ROHO YA YEZABELI-3


 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

16th June 2020

 

1 Wafalme 19-2-10 

Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.

 

1.     ROHO YA YEZABELI HUACHILIA VITISHO KWA WATUMISHI WA MUNGU ILI WAACHE KUSUD LA MUNGU.

 

Nilikuambia kwenye jambo lolote ambalo unakutana nalo kama changamoto usijiombee kufa hata mara moja. Tuliona mifano ya watu ambao walijiombea kufa kwasababu ya kukata tamaa, tuliona Samsoni namna ambavyo alipata shida nah ii Roho ya Yezabeli na hatimaye akajiombea kufa yeye na wale watu.

 

Elia alikaa chini ya mretemu na akijiombea Roho yake ili haweze kufa kwasababu ya Roho ya Yezabeli. Kikawaida Yezabeli anakutia woga ili uache kusudi la Mungu na kukimbia. Elia alipokuwa chini ya Mretemu Mungu alituma kunguru wakamletea chakula pamoja na maji.

 

Kuna wakati Mungu atatuma kunguru kwaajili ya kukusaidia maisha yako, kuna mahali ambapo umekwama na Mungu atakutumia msaada kwako ambao haukutarajia. Mungu akishindwa kukupa watu atakutumia wazo, umasikini ni hali ya kukosa wazo ndani yako. Kwa hivyo ukiwa na wazo ndani yako linakusadia kwenda mahali Fulani. Wazo ambalo Mungu anaachilia kwenye maisha yako ndilo linakupa utajiri, kwenye wazo la Mungu ndipo anaweka utajiri, kwenye wazo la mungu ndipo anaweka maghorofa yako. Mungu atakusaidia kwa namna yeyote ili ili uweze kumshinda Yezabeli.

 

Elia aliomba kufa lakini alikuwa ameifanya kazi ya Bwana, na anasema yeye si mwema kuliko Baba zake na hivyo ajiombea kufa.

 

Ukipata ujasii kwenye maisha yako utatoka lakini ukiwa muoga utakufa, na sisi hapa hakuna kufa wala hakuna umasikini kati yetu. Bwana anatupa njia ya kutoka kwa jina la Yesu.

 

Elia akupunguziwa nguvu ile aliyekuwa nayo ya kuwaua manabii wa bahari bali Yezabeli tu alimtisha na nguvu ndani yake ikapungua. Unapopitia magumu unatishwa na ghafla nguvu ya Mungu inapungua ndani yako. Eliya alikuwa na nguvu na akiita moto unashuka kitu gani kilitokea mpaka akatishwa na Yezabeli mpaka akaishiwa na stamina. Eliaya alipotishwa nguvu ikaisha ndani yake na akawa mwanadamu wa kawaida.

 

Ni wewe ulikuwa unaomba na maajabu yanatokea lakini Roho ya Yezabeli inakutisha na ghafla nguvu inaisha ndani yako. Kuna nguvu ambayo itaachiliwa ndani yako na utatembea nayo siku arubaini na Mungu atakutia nguvu mpaka ufike Mahalia mbapo umekusudiwa.

 

Yezabeli anaiona mbele yako ndiyo maana anakutishia kuwa atakuua. Kila unachogusa unakutana na ugumu lakini leo Malaika wa Bwana akutokee leo kwa jina la Yesu.

 

Huyu mtu ambaye alijilaza kwenye mretemu ndiyo yule ambaye alimwambia mfalme Ahabu kwamba hakutakuwa na mvua juu ya Israeli bila neno lake. Yezabeli alikuwepo na manabii wake wa uongo wapo lakini mvua haikunyesha na hawakuwa na uwezo wowote.

 

Eliya amefika HOREBU kwenye mlima wa Mungu amejilaza kwenye pango Mungu anamuuliza kwanini huko hapa? Mungu alikuwa anajua kwamba Yezabeli alimfukuza lakini alianzisha mazungumzo kwanini alikuwa pale. Mungu anakuuliza kwanini umekwama? Ni kweli yeye anajua umekwama lakini anakuuliza swali hilo? Mungu aliweka kila kitu ndani yako kwa hivyo anapokuuliza lazima umuambie Bwana kuna adui ameinuka na unahitaji msaada wake.

 

Eliya anasema ameona wivu kwaajili ya Bwana. Umetete jina la Bwana wakaharibu biashara yako, umesimama kwenye kazi yake lakini wameharibu ndoa yako.

 

Eliya aliona miamba ikitetemeka lakini hakukuwa Mungu ndani yake, amekimbia Yezabeli ambaye hakuwa na Mungu ndani yake. Inawezekana ulikuwa na biashara ukakimbia lakini Mungu akuwemo. Anawezekana ulikuwa na kitu Fulani ukakimbia kwa uoga wa miungu yao lakini Mungu akuwemo. Mungu anaweza kuzima kila kitu na kikawa sawa hata kama milima inapasuka pasuka lakini yeye akitokea kila kitu kitakaa sawa.

 

Nilisema kuna watu ambao wako kwenye maisha yako ambao ukupewa na Bwana, Elisha alimgangania Eliya kila alipokwenda hata alipomuambia niache kaa mahali nitarudi alikataa. Lakini Gehazi yeye aliambiwa kaa hapa na akakaa, kuna watu ambao utapewa na mtanganganiana kweli kweli kwasababu umepewa na Bwana. Mtu uliyepewa na Bwana utamjua kwa namna ambavyo mtahusiana.

 

Mungu akusadie lakini kuna mambo ya kuombea

 

1.     Mungu aondoe hofu ndani yako.

2.     Jambo la pili mungu akutumie Malaika waseme na wewe.

3.     Jambo la Tatu Mungu akupe mtu sahihi kwenye maisha yako atakayekuwa rafikimwema.

Omba maombi hayo na utamuona Bwana kwenye maisha yako.

 

No comments: