MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 24, 2020

KUSHUGHULIKA NA ROHO YA YEZABELI - 4


 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

18th June 2020

 

1 Wafalme 21:1-16 1 Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. 2 Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. 3 Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. 4 Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula. 5 Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? 6 Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. 7 Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. 8 Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi. 9 Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu, 10 mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. 11 Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. 12 Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. 13 Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa. 14 Wakampelekea Yezebeli habari, wakasema, Nabothi amepigwa kwa mawe, amekufa. 15 Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa kukupa kwa fedha, maana Nabothi hako hai, lakini amekufa. 16 Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, alitelemkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki.

 

1.     ROHO YA YEZABELI INAYOWAZULUMU WATU NA KUHAKIKISHA IMTOA UHAI WAO.

 

Roho ya Yezabeli inainatamani kukunyanganya kila kitu ulichonacho kwenye maisha yako na kukudhulumu. Roho ya Yezabeli inapanga mikakati ya uovu ili ipate kukutia hatiani na kuachilia mauti juu yako.

 

Kama ambavyo umegombana na rafiki yako lakini akaenda kwa mganga na akaambiwa usiogope nitamyanganya kila kitu. Ahabu alikuwa na njia nyingine ya kuchukua shamba kutoka kwa Nabothi ndiyo maana alikwenda kwa huzuni kweli kweli. 

 

Mfalme ana huzuni lakini me wake ambaye ni Yezabeli anamuambia usiogope kwa maana yeye angempa ilo shamba la Nabothi. Wakati mfalme amerudi nyumbani kwake amehuzunika na Yezabeli anamuambia naweza kumpa lile shamba walikaa kikao. Jaribu kuangalia kwamba ni mtu ambaye amekataa kuuza kiwanja chake tu kwa maana ya kuuza urithi wake. Yezabeli alimtia mfalme ujasiri lakini ulikuwa ni wa kuharibikiwa. Ushahuru aliopewa ndani yake haukuwa mzuri kwasababu yeye mfalme alihuzunika lakini alikuwa hana la kufanya.

 

Yezabeli ameandika nyaraka kwa jina la Ahabu. Unashangaa umegombana na jirani yako lakini aliyenunua vita ni mtu mwingine. Yezabeli alizipeleka nyaraka kwa watu wenye nguvu kwa maana wakiambiwa jambo wanalitenda.

 

Yezabeli alipanga hila na akachukua mihuri ya mfalme na kuandika nyaraka kwa hila. Kuna watu ambao wameuona unataka kutoka lakini wamepanga mabaya juu yako. Hata ndugu zako hawajui hata walio karibu na wewe hawajui kwasababu kuna watu wamepanga hila.

 

Uharibifu unataka kumpata Nabothi lakini waliandaa watu wawili ambao walitaka kumshtaki Naboti tena Biblia inasema watu wasiofaa. Walinunuliwa kutenda uovu kwa maana ya kudhuru maisha ya mtu.

 

Nabali alikuwa ni muovu na mume asiyefaa, amewajibu vibaya wajakazi wa Daudi hivyo wakapanga kumuangamiza yeye na familia yake. Sasa angalia Daudi alipanga kuua mpaka watoto ambao walikuwa hawajui chochote. Mtu mmoja tu asiyefaa amewaingiza familia nzima kwenye uovu. Alitokea mtu mmoja ambaye alisikia majibu ya Nabali na kwenda kumuambia mkewe Abigaeli na anaokoa familia na ile mauti ambayo ilisababishwa na mtu asiyefaa. (1 Samweli 25:10-25)

 

Mfalme alipewa shamba bila ya yeye kujua namna ambavyo shamba lilitokea. Waliinua watu wasiofaa ili wamnenee vibaya Nabothi. Hapa ndipo unaona umuhimu wa kuombe mke au mume wako. Unaona analeta fedha lakini haujui ametoa wapi kumbe hiyo fedha imezulumiwa mahali na kuna watu wanaomboleza. Sasa unashangaa baada ya muda magonjwa yanatokea na shida kumbe kilichoingia kimesababisha magonjwa.

 

Mfalme anapokea shamba ambalo hajui kwamba kuna damu imemwagika. Anafikiri kwamba mke wake ana akili kumbe ameua mtu na kupata shamba. Mfalme anaingia kwenye adhabu kubwa mabyo Mungu akutaka kusamehe.

 

Kwasababu ya uovu wa Yezabeli Mungu aliachilia laana ambayo ilikuwa mbaya juu ya Ahabu na Yezabeli mwenyewe akasema “Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli”  

 

Kuna watu ambao wanachochea maovu ili wewe uweze kumkosea Mungu wako kama vile Yezabeli alivyokuwa anamchochea Ahabu Biblia inasema “Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea.”

AHABU alitubu kwasababu ya yale mabaya na Bwana akasema watoto wake wataichukua adhabu ile, inawezekana kuna adhabu uliyobeba ya wazazi wako ambayo wao walitubu. Lakini leo Mungu akuokoe na kila adhabu ambayo imepangwa katika kipindi chako katika jina la Yesu.

 

No comments: