MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 24, 2020

KUSHUGHULIKA NA ROHO YA YEZABELI- 2


 

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

13th June 2020

 

Tuliangalia katika kipindi kilichopita dalili hizi za Roho ya Yezabeli na nataka tuangalie katika sehemu hii ya pili hii Roho ya Yezabeli tena. Moja kati ya Dalili ambayo nataka tushughulike nayo ni ile ambayo tulisema Unasikia unampenda Mungu na kumwamini lakini hauamini kile ambacho unakiomba. Kuomba unaomba na Mungu unampenda na kanisani unakuja lakini kile unachokiomba uamini kwamba kuna jambo litatokea. Biblia inasema lolote unaloliomba uamini kwamba limekuwa la kwako na lenyewe litatokea. Tena maandiko yanasema mtu anayeomba ni sawa na mtu anayepanda shamba tena kwa uchungu akitarajia kuvuna kwa furaha.

 

Biblia inasema paispo Imani hauwezi kumpendeza Mungu kwa hivyo unapoomba lazima uwe na Imani yay ale uliyoomba kwamba yatatokea. Ni sawa sawa na mtu yupo chuko kikuu huku akiamini kwamba hatafanikiwa na mwingine anasoma lakini hana Imani ya kufanikiwa, unafanya biashara lakini hauna Imani ya kufanikiwa katika hiyo biashara.

 

Nataka tuendelee kwenye point ya pili ambayo tuangalie hii roho ya Yezabeli.

 

1.     Yezabeli huua Roho za watumishi wa Mungu na kuinua wakwakwe.

Hii Roho inaua kile ambacho kipo ndani yako na kupanda roho ya Shetani. Na kama tulivyoona hii Roho inakufaya uanguke na kuinuka mara kwa mara. Unakuwa mtu wa kutenda dhambi nakuinuka tena hauwezi kusimama hii ndiyo Roho ya Yezabeli uua vipawa ndani ya mtu na karama.

 

1 Wafalme 18:4

kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa Bwana, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).

 

Yezabeli ameua manabii wa Bwana lakini alitokea Obadia ambaye aliwaficha manabii wa Bwana ili wasije kuuwawa na Yezabeli. Obadia aliwaficha manabii wa Bwana akawaweka kwenye mapango na kuwapa chakula na maji. Kuna watu wako kwenye maisha yako lakini wanayo Roho ya Yezabeli, kabla ya kukutana nao ulikuwa unaomba lakini hauobi tena, ulikuwa unamtumikia Mungu lakini hautumiki tena maana yake mtu huyo ana Roho ya Yezabeli ambayo inakuwepo kwaajili ya kuharibu kusudi la Mungu.

 

Kuna watu ambao wameolewa na kuoa lakini hawajaolewa na Eva wao wala Adamu wao. Unaishi na mke lakini siyo yule ambayo amekusudiwa kwenye maisha yako. Roho ya Yezabeli ina kawaida ya kutangulia mbele ya Mtu na kuweka kizuizi kwaajili ya hatima yako. Yezabeli anaweza kukufanya ukutane na mtu ambaye wewe ulikuwa ujukusudiwa kuwa naye ili haweze kuwa kuzuizi kwenye maisha yako. Anaweza kutanguliza biashara Fulani ili kuua mtaji wako usifanikiwe.

 

Samsoni alikuwa mnadhiri wa Mungu na aliandaliwa kama mnadhiri wa Mungu lakini Delila akaingia kwenye maisha yake na yule ambaye alikuwa mnadhiri wa Mungu nguvu yake ilitekwa. Samsoni ambaye alikuwa na nguvu alipokamatwa na delila maisha yake yakaharibika. Samsoni ambaye alikuwa manadhiri wa Bwana hata Nywele zilipoanza kuota akaomkba nguvu ili afe na maadui zake. Kawaida ya hii Roho nilisema inakufanya utake kufa, kwa kawaida mtu wa Mungu anaomba nguvu siyo ili haweze kufa na maadui zake bali awaue maadui zake. Hii Roho inapofusha macho yako.

 

Tuliona namna ambavyo Gehazi macho yake yalikuwa yamefumba wala hakuweza kuona msaada ambao ulikuwa upande wao. Mpaka pale Elisha alipoomba macho yake yafumbuliwe kisha akaona msaada ambao ulitoka kwa Bwana.

 

Watoto wa Isaka ambao walikuwa mapach akwa maana ya Esau na Yakobo wapo ndani ya tumbo la mama yao Rebeka. Mmoja alikuwa na kusudi la Mungu na mwingine ni mwanadamu wa kawaida.

 

Mwanzo 25:20 -25

25 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. 26 Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino.  Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa. 27 Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani. 28 Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo. 29 Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. 30 Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.

 

Kuna mambo yanaendelea kwenye ulimwengu wa Roho na kuna watu ambao mnafarakana lakini hata vita naye hauna. Utakapoonza kuinuliwa kuna watu utafarakana nao, utakapooanza kazi yako kuna watu ambao utafarakana nayeo. Yezabeli alitaka kuzuia mafanikio ya Yakobo lakini hakuweza kuzuia. Hawa watoto bado walikuwa hawajazaliwa lakini Mungu anasema kwa habari ya maisha yao kabla ya wao kuzaliwa. Kimsingi mtu anapozaa anaumba mwili tu lakini Roho inatoka kwa Bwana. Roho inatpoka kwa Mungu na ndiyo iliyotumwa kazi kutoka mbinguni. Vita uliyonayo ni lile kusudi ambalo umetumwa kulitenda toka mbinguni maana yake kuna mtu ametumwa na wengine wapo wanaomzuia kufanya kile alichotumwa.

 

Yakobo alikuwa na akili kuliko Esau, na kawaida ya mtu mwenye akili anamtawala mtu mwenye nguvu kwasababu ya akili zake. Yezabeli hawezi kuzuia akili ya mtu wa Mungu katika jina la Yesu.

 

Yakobo alipofika kwa Labani alimpenda mtoto mdogo wa Labani na nimekuambia kawaida ya Yezabeli ni kukuandali mtu ambaye siyo. Yakobo aligeuziwa mchumba wake kwasababu alijua kweney familia ya Yakobo kuna mtu atatokea anaitwa Yusufu hivyo walimbadilishia ili Yusufu asipatikane. Yakobo akasema mimi nilimtala mdogo na Labani akamwambia huku kwetu havifanyiki hivi kama unataka na huyu mdogo basi tumika tena miaka saba.

 

Mwanzo 29:18

Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.

 

Sijajua wewe ulimpenda nani sijui ilipenda Biashara ipi? Inawezekana unafanya kazi lakini siyo ndoto yako, inawezekana umeajiriwa lakini siyo kile ambacho ni cha kwako. Yakobo aliona miaka saba kama siku chache kwasababu ya kumpenda. Yakobo alitumiaka miaka saba kwasababu ya Raheli sijajua wewe utatumika miaka mingapi kwaajili ya yule wakwako.

 

Yakobo alipompata Raheli tumbo lake lilifungwa, usishangae Biashara ambayo umetaka kwa muda mrefu ikawa na changamoto. Yakobo alipompata Yusufu ndipo alimwambia Labani nataka kuondoka kwenda kwenye nchi yake mwenyewe (Mwanzo 30:25).

 

No comments: