MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, June 17, 2020

KUSHUGHULIKA NA ROHO YA YEZABELI


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

 

13th June 2020

 

Roho ya Yezabeli ni Roho ambayo inakaa ndani ya mtu, inawezekana ni ndani yako au kati ya watu wako ndani ya familia.

 

Dalili za Roho ya Yezabeli

 

1.     Kuanguka kwenye dhambi kila wakati

2.     Kuanguka kwenye roho ya uzinzi kila mara unakuwa upendi lakini mara nyingi unaanguka kwenye haliya uzinzi.

3.     Kuota kula chakula na kulishwa na watu hii ni Roho ya Yezabeli. Unakuwa unakunywa kitu lakini kichafu chafu unaona ni Juice lakini kumbe ni damu ambayo unakunywa.

4.     Kuota unapewa vitu, unaweza kuota unapewa fimbo au kitu Fulani.

5.     Kuota unavutwa miguu. Kawaida ya roho ya Yerabeli inatiwa watu hofu ndiyo maana wakati mwingine unaweza kuona kama kuna mtu anakufuata kwa nyuma.

6.     Unasikia unampenda Mungu na kumwamini lakini hauamini kile ambacho unakiomba. Kuomba unaomba na Mungu unampenda na kanisani unakuja lakini kile unachokiomba uamini kwamba kuna jambo litatokea.

7.     Kutaka kujiua, unasikia kwamba nataka kufa kwasababu kama kuomba nimeomba kama kutoa sadaka nimetoa lakini sasa sioni kitu si bora nife tu. Macho yako yanakuwa yamefungwa na wala hayaoni. Kitu ambacho kilimfanya yule mtumishi wa Elisha apate shida ilikuwa macho yake kufungwa ndiyo maan alijaa roho ya hofu.

 

Unaweza kujiuliza kwanini sfanikiwi kwanini mimi naomba lakini kama haujatambua tatizo na namna ya kutoka kwenye tatizo utabaki pale pale. Hii roho ya Yezabeli inafunika watu ili wawe na hofu ndani yao.

 

Roho ya Yezabeli inaweza kuingia ndani ya mwili wa mtu na ikamsemesha. Kwamba si umeona kwamba ulifanya kie na hiki lakini haukufanikiwa.

 

Yezabeli aliolewa na Ahabu na kipindi kile mfalme alikuwa anachaguliwa na Mungu sasa Ahabu aliwekwa na Bwana lakini sasa akaenda kuoa kule ambapo hawakuruhusiwa kuoa. Alipomuoa Yezabeli akageuza moyo wake.

 

1.     Roho ya Yezabeli inawafanya watu wamuabudu shetani na kujenga madhabahu ya shetani na kuondoa madhabahu ya Mungu aliye hai

 

1 Wafalme 16:31-32

31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.

 

 

Ahabu alipompokea Yezabeli kwenye maisha yake alianza kuharibu maisha yake. Watu wanapoingia kwenye maisha yako kuna mabadiliko yanaweza kutokea. Hakuna mtu anabadilika isipokuwa ni kupokea mtu falani au kutoka kwa maana ya kwenda mahai Fulani na kukutana na vitu Fulani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments: