MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, June 11, 2020

ROHO ZA WAFU AU ROHO ZA MIUNGU ZA WATU WALIOKUFA NDANI YA FAMILIA.



11th June 2020

Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila,

Kwanini roho za wafu zinatokea?

Kuna wafu wa aina mbili: -

1.     Wafu waliokufa katika dhambi ambao hawakumuamini Mungu wala awakuokoka. Watu hawa wanakuwa kuzimu kwenye utawala wa shetani huku wakisubiri hukumu ya mwisho kwenye utawala wa shetani.

2.     Wanaokufa katika Bwana. Hawa wanakuwepo kwenye utawala wa Mungu na utukufu wake ingawa Mungu anaweza kuwatumia vile vile.

Roho za wafu zinazokutokea ni Roho amabzo zinatumwa na shetani ili kutawala watu ambao wako hai. Shetani anahitaji kuondoka na watu wengi kwenda Jehanamu kwasababu iliandaliwa kwaajili yako.

Hawa watu wanatawala Roho za wanadamu walio hai lakini zimetumwa na shetani lakini hawa waliokufa katika Bwana Mungu anaweza kuwatumia anavyotaka. Tunaona Yesu akiwa mlimani anatokewa na Musa na aliye na wote walikuwa wamekufa na akasema nao na wanafunzi wake wakauona utukufu wake. Hawa watu walipomtokea Yesu ni watu muhimu kwenye Biblia kwa maana Musa alipewa sharia na Eliya alikuwa kwa upande wa manabii na Yesu alikuja kutimiliza yale yaliyoandikwa na manabii.

1 Samweli 28:1-20 1 Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako. 2 Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima. 3 Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. 4 Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. 5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. 6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. 9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? 10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. 11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. 12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. 13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. 15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje. 16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? 17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. 18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. 19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. 20 Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.

Hii roho za wafu ndizo ambazo utakuta mtu akitembea nazo anaanza kutembea na tabia za mababu kama ni ugonjwa utakuta ni ule ambao ulimuua Babu. Ndiyo maana unapta kisukari wanauliza nani kwenye ukoo ana ugonjwa wa aina hiyo unakuta ni Babu au Bibi ambaye alikwisha kufa lakini uliridhi magonjwa hayo ambayo uliridhishwa.

Inatokea tabia Fulani ndani ya familia kwamba hii ni tabia ya nani na unakutana na tabia ya namna hiyo alikuwa nayo shangazi hivyo watoto wameridhia au watu Fulani kwenye familia sikiliza leo tunafuta kwa damu ya Yesu…. Leo tunaanza maisha mapya kwasababu tumekombolewa kwa damu ya Yesu na tumebarikiwa na leo kwa damu ya Yesu kuanzia wewe unaanza uzao mpya na maisha mapya ndani ya Damu ya Yesu.

Lakini hauwezi kuanza maisha mapya bila kukataa hizi Roho za wale waliokufa na wanakumiliki. Haujalewa kwanini Yesu hakufia msalabani na kuishia hapo bila kuingia kwenye kaburi, ilimpasa kuingia nay ale magonjwa yako kaburini, laana za ukoo na kisha akafufuka na uzima wetu, Baraka zetu. Ndiyo maana Biblia inasema tulikufa na kufufuka pamoja na Yesu.

Wakati wa vita ndipo mtu anatafuta msaada, vita ilitokea na Sauli alitakiwa kwenda vitani lakini alipomuita Bwana na yeye alikaa kimya. Ni hatari kwenye maisha yako unapita siku mbili Mungu akakaa kimya.

Mungu akumjibu Sauli kwenye ndoto, kumbe unaposema na Bwana wakati ukiwa kwenye shida anaweza kukujibu kwenye ndoto.
Unapokuwa kwenye changamoto lazima uwe makini sana kwasababu unaweza kufanya maamuzi mabaya ya kukupelekea kuharibikiwa. Sauli anauliza kwa Bwana na kwasababu ya makossa yake Mungu akumjibu na hivyo akaamua kwenda kwa wanganga wa kienyeji.

Watu wengi waliokwenda kwa wanganga wa kienyeji ni wale ambao waliingia kwenye shida na majaribu ya aina mbali mbali na wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji.

Sauli alipouliza apate wapi mganga wa kienyeji kulikuwepo na watumishi wake ambao nao walikuwa watumishi lakini wakienda kwa wanganga wakampeleka kwa mganga. Kuna walokole ukiwa kwenye changamoto watakupeleka kwa wanganga wa kienyeji. Hivyo kuwa makini kwasababu wale ambao wanakusaidia ni wale ambao wako karibu na wewe.

Unapopita mahali kuna marafiki wa aina nyingi ambao watakushauri lazima uwe makini Sauli aliangaika mpaka kwa watu wake wa karibu kwasababu ya changamoto ambazo alikuwa nazo.

Kazi za roho za wafu ni kugeuza mtu zinakutokea kwenye ndoto na wanakulisha chakula na kuongea na wewe. Unapokula chakula hicho cha wafu kinaanza kuzuia nguvu za Mungu na unajikuta anaanza kutenda dhambi.

Mungu anapokaa kimya kwenye maisha yako shetani anakunyemelea aweze kukugeuza na kukupelekea kwenye ubaya. Shetani kila wakati anatafuta nafasi ya kukugeuza. Moyo wa mtu ukigeuzwa viungo vyake vyote vinakuwa vimeshageuzwa.

Sauli alikuwa na kumbukumbu ya mtu aliyekufa na yeye alijua akimuita Fulani atampa msaada. Mwanamke alikuwa anamjua Sauli lakini alibojibadilisha hakuweza kumtambua. Sauli aliwakatilia mbali waganga na wachawi katika Nchi ya Israeli.

Samweli alikuwa amekufa na mganga alijua kabisa kwamba anaweza kumpandisha aliyekufa kwa maana ya Roho za wafu. Na ndiyo maana alimpandisha Samweli.

Ndiyo maana tunapoombea watu utasikia akisema mimi ni Bibi wakati alishakufa miaka mingi na anakuwa na uhalali wa kumiliki walio hai. Kwa hivyo kwasababu shetani anakua kwamba mwanadamu anakawaida ya kukata tamaa hivyo basi wanashikilia kazi yako, mikono yako na kila kitu chako. Hivyo anavyokamata unapoenda kwenye makaburi ya Babu anaachia na wewe unaona umepata unafuu kumbe ndiyo anazidi kukuunganisha kuzimu.

Samweli alikufa na aliyekuwa anamtumikia Mungu, na yule mwanamke alijua Samweli ni mwanadamu hivyo basi akimuita atakuja kama mwanadamu wa kawaida. Kumbuka aliyeokoka ni MUNGU KAMILI HIVYO WANAVYOFANAY VITA NA WEWE WANAKUTANA NA MUNGU KAMILI. Ukielewa jambo ili utakuwa unajua namna ambavyo ukiomba inakuwa kwasababu unao uwakika, unapoomba kwa kutumia kinywa kinageuzwa kuwa ni moto mikono yako inageuka kuwa ni upanga ukatao kuwili.

Mganga anaita Samweli lakini kwasababu alikuwa akimtumikia Mungu hakumuona Samweli bali mungu ambaye alitoka katiak Nchi. Samweli ingawa alikuwa amekufa lakini alianza kuongea na Sauli. Tambau kwamba mfu anaweza kuitwa na akaongea ndani ya mtu ingawa alishakufa. Kumbe Mungu akikuacha hauna mahusiano na mtumishi wa Mungu.

No comments: