MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Sunday, June 07, 2020

NAMNA YA KUTUNZA MUUJIZA WAKO.


7th June 2020
Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila
Bishop Dankton Rweikila akiwa katika vazi la Kikuhani.



Tumekuwa kwenye wiki ya maombi na kwasababu tuliomba na kunyinyenyekeza mbele za Bwana ni zamu ya kuendea yale ambayo tumeyaomba kwa Bwana ili akatimie kwenye maisha yetu.

Yohana 15:1-10
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.


Ammy Mwakitalu akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji. 
Kuna mzabibu na kuna mkulima na matawi yenyewe. Usipojua umuhimu wa shina ambao ni mzabibu tawi aliwezi kuzaa, mzabibu usipomtegemea mkulima hauwezi kuzaaa. Laziam utambue mkulima, matawi ili kuwepo na uzao wa mzabibu.

Watu wengi wanafurahia matunda ya mzabibu na kusahau kuwa kuna mkulima ambaye alilima. Matunda ni pale unapofanikiwa na Mungu anakufanikisha iwe ni gari, uzao, nyumba na vingine vingi. Ukiacha shina la mzabibu na kukimbilia kwenye matunda kutakuwa na shida kwenye mzao wa mzabibu. Ndiyo maana tumekuwa watu wa kukatwa kila iitwapo leo.

Ukiwa ndani ya Kristo umoja utaonekana, upendo utaonekana na mengine mengi kwasababu Yesu yupo ndani yako.

Kuwa mlokole maana yake si Mtakatifu, maana yake kuwa tawi la mzabibu siyo kuzaa matunda.

Tawi linazaa sawa sawa na Shina, kiwango cha mazao kwenye tawi kinatokana na nguvu ya shina. Ndiyo maana Biblia inasema kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yako. Efeso 3:20

Wengi tumeshindwa kufanikiwa kwasababu tumeacha utakatifu na tumekuwa kwenye maombi muda mrefu ni kweli lakini kufanikiwa kwako kunatokana na namna ambavyo unaishi. Kama hauishi maisha ya utakatifu alafu unasema umeokoka jua kwamba

Ili ukae kwenye shina la mzabibu au ndani ya Kristo kuna sifa kama nne:-

1.     Kumpenda Mungu kwa moyo wako Marko 12:30
Kitu unachokipebda hauwezi kukiacha wala kukisahau kwasababu unakipenda.

2.     Mpende Bwana Mungu wako kwa Roho yako yote.
Roho yako ilipo ndipo na wewe uwepo, kumpend Mungu kwa Roho yako yote maana yake utakaa ndani ya Kristo. Kitu unachokipenda uko tayaro kufa lakini ukitetee.

3.     Mpende Bwana kwa akili zako zote.
Unapompenda Mungu namna hii kila ambacho utakuwa ukiamua utaanza Mungu.

4.     Nguvu zako mpe Bwana.
Wengi sana wanapoamka asubuhi ngvu zao wanapelekea kwenye mambo yao ya kila siku kama kumpikia mume au watoto. Kumbuka unapoamka nguvu zako kabla ya kumpa yeyote unatakiwa kumpa Bwana.

Ukishamaliza kumpe Mungu sifa hizi jambo linalofuata MTUKUZE MUNGU WAKo. Mara nyingi watu wanafurahia matunda na kusahau shina ambalo limewezesha tawi kuwepo. Hakikisha kwamba unampa Mungu utukufu wake siyo tawi ambalo limetokana na shina.
Waamini wakifuatilia ibada ya leo PGFC 

Isaya 42:8
Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.

Mara nyingi kwenye maisha ya kila siku Mungu anapotenda haonekani Mungu anaonekana mwanadamu. Sasa utukufu huo unatakiwa kumpa Mungu siyo mwanadamu. Unapomtukuza mwanadamu jua kwamba anageuka kuwa sanaamu. Yote uliyotendewa kwenye maisha yako utukufu ni wa Bwana, yeye ndiye aliyekuandalia mtu afanye jambo flani juu ya aisha yako.

Utukufu utabaki ni wa Mungu, tumefanya Mungu akatishe miujiza kwa sababu tumeondoa utukufu wake tukawapa watu. Unapoupeleka utukufu wa Mungu mahali Mungu hukata. Wako waliokuwa wameinuliwa lakini wamebaki bila kitu.

Zaburi  20:7
 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.

Biblia inasema wao wanatja magari, wanataja farasi lakini sisi tunalitaja jina la bwana wa Majeshi, kumbe wao wakipata magari utukufu wanarudshi kwenya magari, wakipata watoto utkufu wanawapa watoto, wanataja vitu vyao ila sisi tutalitaja jina la Bwana wa Majeshi. Kila mahali unapokwenda litaje jina la Bwana wa Majeshi na Bwana atataja kipawa chako, karama yako.

Lazima umtaje Bwana kwenye maisha yako na lazima uelewe kwanini Mungu anataka umtaje wala si vinginevyo. Ufikie mahali useme kama isingekuwa Bwana na Israeli aseme sasa.
Bishop Dankton na Mama Bishop Charty katika ibada ya leo
Kutoka 34:14 Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.

Wivu maana yake ni kukatilia mbali mtu ambaye amekuingilia. Wengi wetu hatuelewi mengine tunayopitia yamekuwa ni mapigo ya Mungu. Ni hatari sana kwenye maisha yako kusema nimechelewa kwenye ibada kwasababu ya kuandaa chakula cha watoto. Mimi uwa namuambia mke wangu kuliko uchelewe kwenye ibada ni bora tusile icho chakula lwasababu hicho chakula ambacho unakula Mungu ndiye anakiponya.

Kumb 8:14-16
basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; 15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.

Ukiona mtu anachukia pale anapoungamanishwa na Mungu ndani ni 100% kuna pepo, maana pepo anaogoppa unapofanay mahusiani mazuri na Mungu wako, anaweza kukuondolea amani ndio maana ibada chungu huwa ni ibada ya toba maana shetani huwa anapata uchungu. Unapoanza kutengeneza mahusianno yako na Mungu dipo shetani anakuletea msiba.

Unapomtafuta Bwana moyo wako usiinuke, mtu ambaye anakumbuka anapata neema ya kuongezewa. Anapata heshima na kibali. Mungu atakapokuza jina lako na likajulikana Tanzania kwenye mkoa kwenye wilaya umsimsahau Bwana. Mungu atakapokupa chakula na kikajaa kwenye jokofu lako isimsahau Mungu wako. Mungu anataka umpe yeye nguvu zako ili hatakapokuinue useme ni kwa msaada wa Bwana.

Utakapomsahau BWANA na kumuweka mtu mwingine maana yake anageuka kuwa sanamu kwako. Mtu anasema bila wewe nisingefika hivi au bila wewe nisingefaulu Biblia inasema amtumainiye mwanadamu amelaaniwa. Kama hauwezi kumsahau Mungu kwenye maisha yako hauwezi kupungukiwa kamwe. Ndiyo maana unawaona wakina Paulo wakina Shedrack na wengine wengi ambao hawakumsahau Bwana.



No comments: