MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, June 02, 2020

KURUDISHWA KWENYE NAFASI YAKO.

2nd June 2020
Image may contain: 1 person, text
Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila
Wapo watu ambao wamekutoa kwenye nfasi yako na walipokuona walikuona watu wa kawaida wakapanga mabaya kwaajili ya kile ambacho kipo ndani yako.
Waamuzi 11:1-31
1 Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. 2 Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine. 3 Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye. 4 Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli. 5 Ikatukia, hapo wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu; 6 wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni. 7 Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu? 8 Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena, ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi. 9 Basi Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi Kwamba mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele yangu, je! Mimi nitakuwa kichwa chenu? 10 Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu; hakika yetu tutafanya sawasawa na neno lako. 11 Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya Bwana huko Mispa. 12 Basi Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una nini nami, hata umenijilia kupigana juu ya nchi yangu? 13 Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea kutoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena pasipo matata. 14 Yeftha akatuma wajumbe mara ya pili waende kwa huyo mfalme wa wana wa Amoni; 15 akamwambia, Yeftha akuambia hivi; Israeli hakuitwaa nchi ya Moabu, wala nchi ya wana wa Amoni; 16 lakini hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walienenda katika bara hata kuifikilia Bahari ya Shamu, na kufikilia Kadeshi; 17 ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hakusikia. Ni vivyo wakampelekea wajumbe mfalme wa Moabu; wala yeye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi. 18 Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga marago upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu. 19 Kisha Israeli wakatuma wajumbe waende kwa Sihoni mfalme wa Waamori, mfalme wa Heshboni: Israeli wakamwambia, Twakuomba utupe ruhusa tupite katika nchi yako, mpaka mahali pangu. 20 Lakini huyo Sihoni hakuwaamini Israeli ili wapite ndani ya mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, nao wakapanga kambi katika Yahasa, wakapigana na Israeli. 21 Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawapiga; basi Israeli wakaimiliki hiyo nchi ya Waamori, wenye kukaa nchi hiyo. 22 Nao wakaumiliki mpaka wote wa Waamori, tokea Arnoni hata Yaboki, tokea hiyo bara hata Yordani. 23 Basi sasa yeye Bwana, Mungu wa Israeli, amewapokonya Waamori watoke mbele ya watu wake Israeli, na wewe wataka kuwatamalaki? 24 Je! Wewe hutakitamalaki hicho ambacho huyo Kemoshi mungu wako akupa kukitamalaki? Kadhalika, awaye yote ambaye Bwana, Mungu wetu, amemfukuza atoke mbele yetu hao ndio tutakaowatamalaki. 25 Na wewe sasa, je! U mwema kuliko Balaki mwana wa Sipori, huyo mfalme wa Moabu, kwa lo lote? Je! Yeye alishindana na Israeli, au kupigana nao? 26 Wakati Israeli waliokuwa wakikaa Heshboni na miji yake, na katika Aroeri na miji yake, na katika miji hiyo yote iliyo huko kando ya Arnoni, muda wa miaka mia tatu; mbona ninyi hamkuipata tena katika majira hayo? 27 Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye Bwana, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni. 28 Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuyasikiza hayo maneno ya Yeftha aliompelekea. 29 Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni. 30 Naye Yeftha akamwekea Bwana nadhiri, akasema, Kwamba wewe utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu kweli, 31 ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.
Ni Yeftha ambaye amezaliwa kwenye gfamilia lakini Biblia inasema alikuwa ni shujaa sana. Yeftha amezaliwa kwenye familia Fulani na wanamjua yeye ni shujaa kwa namna alivyokuwa. Kawaida ya shujaa anaanza kuzuiliwa hata kabla ya kuonyesha ushujaa. Yeftha ni shujaa na ndani yake Mungu ameweka kitu kikubwa sana lakini alizaliwa na mwanamke kahaba ambaye walikuwa wanamdharahu. Hawakujua kwenye mzoga kwamba kunaweza kutoka asali.
Walokole wengi wanaangalia historia yao na maisha yao yalivyo na wanamalizika kabisa, kumbe Bwana anawafanya wasiofaa wafae na wale ambao hawana akili Bwana anawapa akili.
Mungu anavitumia vinyonge kwaajili ya kufanya mambo makubwa, kuna watu wamesema hautaweza lakini utaweza katika jina la Yesu. Mikono yako itafunguliwa kwa jina la Yesu. Vifundo vilivyoshilkilia hatima yako vitafunguka katika jinal Yesu.
Yeftha alizaliwa na mwanamke ambaye ni kahaba lakini alizaliwa akiwa shujaa. Aijalishi umezaliwa katika mazingira ya namna gani lakini Mungu anayo makusudi ya wewe kuwepo. Kitu ambacho haujajua kwamba kuna watawala wawili hapa Duniani. Kuna Mungu ambaye aliumba vyote lakini ukimuondoa Mungu kuna shetani ambaye anatawala. Ukimuondoa Mungu shetani duniani ana nguvu kuliko mwanadamu yeyote aliyeko duniani. Lakini ukimuweka Mungu ndani ya mwanadamu maana yake shetani ana nguvu tena. Mungu akiwa ndani yako shetani wa Dunia hii anakimbia. Mwanadamu ukimuacha Mungu shetania nakukunja anavyotaka lakini ukiwa na Mungu unamkunja unavyotaka. Umepewa mamlaka ya kukanyaga ng’e na nyoka.
Ndugu zake Yeftha wanamuambia wewe umezaliwa na mwanamke kahaba hivyo hautarithi mali za Baba yetu. Ndugu zake wamemfukuza kwenye nafasi yake. Kiuhalisia ugomvi wa ndugu haukuanza leo. Hawa ndugu walichosahau kwamba Yeftha aliondoka akiwa shujaa kwa maana aliondoka na ushujaa wake.
Watu walijua kwamba wamepigwa kwasababu shujaa Yeftha hakuwepo ndiyo maana wakaona waachane na kila kitu alafu wamuendee Yeftha. Walimfukuza Yeftha akiwa wa kawaida na alirudi akiwa kichwa juu yao kwa maana ya kutawala.

Yeftha alishinda kwasababu akili zake alimpa Bwana na Moyo wake alimpa Bwana. Wewe unaweka nadhiri mbele za Bwana lakini haumpi Bwana moyo wako.

No comments: