MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Monday, June 01, 2020

KUTOKA KWENYE MASHIMO


1st June 2020
Isaya 42:22
Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
Mtu anaweza kuibiwa nafsi yake, mikono yake, kinywa chake na hata hatima ya maisha yake. Unaona mtu anaishi lakini wapo watu ambao wameshika nyota zao. Ni watu ambao wako kwenye mashimo, wanatamani kufanikiwa na kufanya jambo fulani lakini haliwezekani kwasababu ya mashimo hayo. Ndani ya mashimo Biblia inasema kuna magereza lakini wamekuwa mawindo kila wakitaka kutoka wanarudishwa.
Watu wanaweza kupoteza maisha yako, biashara yako na kuharibu kabisa ramani ya maisha yako. Kuna watu wengine wameuzwa siyo hiyari yao lakini wameuzwa mahali, lakini leo unapatikana kwa jina la Yesu.
Mtu aliyeuzwa unaonekana kama amekufa. Kuna watu walitegemea ufe lakini hautakufa na utarudishwa wiki hii kwa jina la Yesu.
MTU ANAWEZA KUUZWA.
Mwanzo 37:26-35
26 Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? 27 Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. 28 Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri. 29 Akarudi Reubeni birikani, kumbe! Yusufu hayumo katika birika, akararua nguo zake. 30 Akarudi kwa ndugu zake, akasema, Mtoto hayuko, nami niende wapi? 31 Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu. 32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. 33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. 34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. 35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.

Walitaka kumuua Yusufu na akatokea kaka yake Yuda na akawaambia hakufai kumuu ndugu yetu . Wamekaa kikao na wakakubaliana mabaya juu ya Yusufu kwa hiyo wakasema tusimuue bali tumpeleke huko hakatumikishwe.
Walikuwa wanamuuza Yusufu kwasababu ya  ndoto yale . Vita yako inakuwa ngumu sana kwasababu ya wale ambao wanakishambulia na wako sirini. Kila ukishambulia anajipanga sirini na anajua nguvu zako lakini ashukuruwe Mungu hajui uweza wa Mungu wako. Kama walikuona huko pekee lakini auko peke yako.
Chakula ambacho walikuwa wanakula waliletewa na Yusufu na wanapanga kumuua. Inawezekana kabisa yale ambayo yanakupata wanasababisha wale wa karibu yako kabisa, mlokole mwenzako, jirani yako yako kabisa lakini wamechora mchoro.

Na watesi wako wakiona kukuweka kwenye shimo haitoshi watataka kukuamishia kwenye mateso mengine. Ndiyo maana ulianza na malaria, wakaendelea kwenye biashara yako. Walifilisi biashara wakaona haitoshi wakakuweka kwenye madeni wakaona haitoshi wanataka kukudhulumu kabisa.


No comments: