MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, March 24, 2021

NGUVU YA KUGEUZWA NA KURUDISHWA KWENYE ASILI YAKO

 NGUVU YA KUGEUZWA NA KURUDISHWA KWENYE ASILI YAKO


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila


14th March 2021


NENO HILO LIMEBEBA MAMBO MANNE 


YEREMIA 2:21


Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?


》Unachosikia


》Kadri unavyoona ndivyo unatamani kusikia ( Unavyoona)


》Imani


》Mazingira


Mwanadamu aliumbwa mzabibu mwema na Mungu anauliza alipanda mzabibu mwema imekuwaje kugeuka na kuwa mzabibu mwitu. Sasa ili kujua kwamba mwanadamu anabadilikaje na aligeukaje lazima turudi kwa Adamu. 


Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu lakini aliporuhusu kusikia kutoka kwa ibilisi ndipo akaona tunda lifaa kuliwa na ghafla mazigira yakabadilika na wakajificha kujiona wako uchi. Mungu alipomtembelea Adamu alimkimbia Baba yake hivyo akategemea mabaya wakati alikuwa anamkimbilia Baba yake hapo awali. Imani yake ikageuzwa na mazingira yakageuka tena. 


Ndiyo maana mtu anapookoka anakuwa kwenye hali nzuri sana kiroho lakini ghafla anapoaanza kusikia maneno ya walokole ndipo uharibifu unatokea kwake na kuanza kushuka kiroho. Utasikia mtu akisema mimi nilifunga mara nyingi sikufanikiwa anakukatisha tamaa kwa kusudi kabisa. Hii si kwa habari ya kuokoka tu unapokwenda madhabahuni kwa mara ya kwanza utashangaa bidii utakayokuwanayo. Lakini ukianza kusikiliza maneno ya watu ndipo utakapopata shida. 


Kwa kadri moyo wako unavyobadilika ndivyo mahusiano yako na Mungu yanabadilika. Yule mwana mpotevu alipopoteza mahusiano na Baba yake ndipo Huduma nyingine ziliisha (Luka 15:11-32)


Shahuku ya ndani ikishageuzwa unaanza kwenda mahali kimazoea. Kwamba ni kwasababu jumapili kuna ibada lakini siyo kwasababu unashahuku na Baba yako. Nehemia aliposikia kuta zimebomolewa akasikia huzuni ndani yake. 


Baba yako ni wa vyote na ukutakiwa kuwa hivyo, kile ambacho kimekufanya uone ibada ya kawaida, maombi ya kawaida, mifungo ya kawaida kuna jambo alimekugeuza. Mahusiano yakifa hata kwenye ulimwengu wa kiroho yanakufa, ndiyo maana angalia yule mtu ambaye unamchukia hauwezi kuona akikubariki bali utaona anakukaba na kukufanyia mabaya. Hivyo ndivyo ulivyo ukimpenda Mungu wako utaona namna ambavyo utaona kwenye ulimwengu wa roho, utaanza kuona muda wa ibada ni mfupi, muda wa maombi kama hautoshi. Ukiona hayo jua moyoni mwako ibada hiyo haikuhusu. 


Mungu wako hawezi kukusahau wewe rudisha tu mahusiano na Mungu wako. Yeye amechora jina lako kwenye viganja vya mikono yake wala si kwenye viganja vya Malaika. 


Mabaya si sehemu yako unapokuwa na Bwana yatakuwa ya muda tu . Ayubu alipita kwenye jaribu hata wale rafiki zake wakina Bildadi, Sofari na Elifazi wakasema ni nani atakayevumilia kwa haya yaliyokupata na walijua ni mtu mwenye haki. Sikiliza dhiki hiyo ilikuwa ya kitambo tu ( 2 Wakorintho 4:17) na baada ya muda utangaa. 


Luka 5:1-11


Petro alisema kwa neno lako tutashusha nyavu. Petro alisikiliza neno la Bwana na hata alipoiangia kwenye chomba hawakumdai kutumia chombo chake. KWA NENO LAKE UNAWEZA KUFANYA MAKUU SANA. 


Kesho tunaanza maombi ya siku 21 masaa kumi na mawili kufunga na kuomba na tunakutana saa kumi kumi kamili jioni ibada itakuwa imeanza. Walete wagonjwa na wenye shida mbali mbali Bwana atawahudumia katika siku hizi ishirini na moja. 


Bishop Dankton Rudovick Rweikila

Power of God Fire Church

Chanika Buyuni

Simu +255  753 230 680 +255 717 538 499

Youtubu Chanel https://youtu.be/mJSqGrFBd4 inc

Facebook link.POwer of God Fire Church https://www.facebook.com/Power-of-God-Fire-Church-965783380111414/

Or 

Bishop Dankton Rudovick Rweki 

https://www.facebook.com/profile.php?id=100010423302719

www.powerofgodfirechurch.blogspot.com

No comments: