MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Wednesday, March 24, 2021

KUVULIWA VAZI NA KUVIKWA VAZI

 KUVULIWA VAZI NA KUVIKWA VAZI


Na Bishop Lambart Ileta


15th March 2021. 


Kuna vitu kadhaa tunataka tuangalia katika mfungo huu wa siku 21. Tunakwenda kuvaa vazi lakini sasa kabla ya kuvaa vazi ambalo linapatikana kwenye ufalme. Haya mavazi yanapatikana kwenye ufalme na upo kwenye ulimwengu wa Roho. Sasa lazima tujue haya mambo kwa kina kidogo. 


Warumi 10:9-10


Tunataka kuangalia ulimwengu wa Roho ni kitu gani na unaingia vipi. Biblia inasema ukiamini kwa moyo na kukiri ndipo unaokoka. Unapoamini na kukiri kwamba Yesu ni Bwana unaingia kwenye ulimwengu wa Roho. Ulimwengu wa Roho upo karibu sana na sisi kuliko vile tunavyofikiri. 


Kwa hivyo hatua ya kwanza ni kukiri kwa kinywa na unapokiri unapata wokovu na haki yako na unafunguliwa geti na mlango wa kuingia kwenye ufalme na kisha utaanza kupata haki za mfalme. Sasa utapataje hizo haki ni kwa kumuamini mfalme na neno lake. Unajua unapoamini kwamba wewe ni wa ufalme wa mbinguni itakuwa hivyo usipoamini hauwezi kuwa na haki ya ufalme huo. Ukiamini tu unapata ufalme. Kile kilichotoke kwa wale wezi wawili pale msalabani ilikuwa ni kuamini kwamba Yesu ni Bwana kiuhalisia hatukuona mahali ambapo huyu ndugu aliongozwa sala ya toba lakini aliamini moyoni mwake (Luka 23:39-43). Hizo ni siri za ufalme nakupa ukiamini tu. Jinsi ya kutengeneza na kupokea ni imani uliyonayo. Tengeneza imani yako ili kuweza kutengeneza mambo makubwa najua unaamini ndiyo maana huko hapa lakini unahitaji kuzidisha imani yako (Warumi 1:17). Unahitaji kuikuza imani yako kwasababu shetani anasimama kwenye imani yako ili wewe usiweze kusimama kwenye ile haki. 


Sasa utauliza nakuzaje imani? Imani inakuzwa kwa kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Na kama imani inaweza kuja inaweza kuondoka vile vile kwasababu inaondoka kwa kusikia vile ambavyo siyo neno la Mungu. Yuda 1:3


Kukiri maneno ni jambo lingine na kuyaamini ni jambo lingine. Kuomba ni jambo lingine na kuamini kile unachoomba ni jambo lingine ndiyo maana Biblia inasema ukiomba uamini kwamba yamekuwa yako na hayo yatatokea. Marko 11:24


Efeso 3:17-20


Kristo anakaa ndani ya moyo wako kwa imani. Imani ndiyo inakufanya ujue kwamba una Mungu au hauna Mungu ndani yako. Ukiamini kwamba yupo ndani yako yupo kweli kwa imani. Ukijua upana urefu na kina na kuamini ndivyo unavyopewa. Kwa kadri ya kuamini kwako na kujua upana wake na kina chake. 


Jambo la pili ni kujua upendo wake kwamba unajua anakupenda kiasi gani? Baba yako anaweza kuwa na vingi lakini unajua upendo wake kwamba anaweza kukupa. Kama haujui upendo wake hauwezi kupata haki yako. 


Sasa sikiliza usichanganye imani na uaminifu kwamba mimi nafunga ni kweli, mimi nafagia kanisa ni kweli lakini hayo yote kama hauna imani ni bure. Uaminifu haukusaidia kutengeneza jambo kwenye ulimwengu wa Roho bali inakusaidia pale ambapo Shetani anapeleka hoja zako akakosa kile ambacho atakushtaki nacho. Tofautisha haya mambo mawili faith and Trust.

No comments: