MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, November 15, 2016

HAKI INAYOLETA KIBALI KWA MTU

Na Bishol Dankton Rudovick Rweikila

  Je ? Unapataje haki ili ikuletee kibali.

Wagalatia 2:16 “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.”

👪Mwanadamu awezi kutimiza ambacho Mungu anakitaka kwake . Kila Mwanadamu ni mdhahifu mbele za Mungu, lakini kwa Imani tunahesabiwa haki kwa njia ya Yesu Kristo . Hivyo hakuna anayehesabiwa haki kwa matendo yake mwenyewe. Wagatia 3:11 "Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani."

Hakuna mtu anayeweza kuhesabiwa haki kwa sharia za Mungu alizoweka bila neema ya Damu ya Yesu Kristo. Biblia inasema mwenye haki anaishi kwa Imani maana yake kwa kumuamini Yesu Kristo . Unakaa ndani ya Yesu na Yeye anakaa ndani yako ndipo unahesabiwa haki kwa neema yake Yesu Kristo. (Yohana 15:4)

Je ? Kama neema ya Damu ya Yesu inanikomboa kwanini ni hesabiwe dhambi ?

Yesu ni wakili (Advocate) wako na wewe ndiye muamuzi wa kipi ufanye kipi usifanye (1 Yohana 2:1) . Ndiyo maana mbele yako ameweka mauti na uzima na anayechagua ni wewe , ukichagua uzima maana yake Yesu atahusika katika kukutetea. (Kumbukumbu 30:19)

Haki inaletaje Kibali ?
 Tumeshaona haki inaletwa kwa Damu ya Yesu sasa tuangalie haki inaletaje kibali .

Mithali 3:4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

Unapokea kwanza kibali kwa Mungu ( Uhalali au cheti cha kupenya kwenye ulimwengu wa Roho) Kisha ndipo unaweza kutumia kibali. Kumbuka Mungu anayo mamlaka na shetani anayo mamlaka . Shetani ana mamlaka juu yako unapokuwa na kibali kutoka kwa Mungu.

Mwanzo 37:5:4
Mungu alimpa Yusufu kibali ambacho kilimpelekea Baba yake kumpenda Yusufu. Kibali kilichokuwa juu ya Yusufu akikuweza kuzuiwa na ndugu zake ingawa kibali alichokuwa nacho Yusufu akikufanya kazi kwa ndugu zake, lakini kilifanya kazi utumwani . Shetani alitaka kukiondoa kibali kilichokuwa juu ya Yusufu lakini kibali kilimpa Yusufu nguvu ya kushinda uovu.

Wakristo wengi wanataka vibali vingine lakini kibali cha kushinda dhambi awataki. Ukiona mtu anasema anacho kibali lakini anatenda dhambi lazima ujiulize kibali kinatoka wapi ? Yusufu hakuwa tajiri wa mali alikuwa tajiri wa kibali . Uzuri, Elimu, Utajiri unaweza kukataliwa kwenye mazingira magumu lakini siyo kibali . Kibali kinakuinuliwa watu wa wakuone ulichokibeba . Kibali kinakupa kinywa cha hekima . Kibali kinapoonekana ndipo haki inatokea .

MADHARA YANAYOTOKEA KWAKO UNAPODHARAU HAKI YAKO

Mwanzo 25:31 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.  Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa. Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.  Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo.  Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.  Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.  Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza

Kuzoea dhambi na uovu ni dalili ya kudharau haki yako iliyopatikana kwa damu ya Yesu Kristo. Sasa yapo madhara yanayopatikana unapodharau haki yako ?

Esau alipodharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza Baraka zilienda kwa Yakobo badala yake. Unaweza kudharau haki yako ya Damu ya Yesu kwasababu ya mkate wa siku moja. Maana yake unaidharau haki yako ya kuzaliwa mara ya pili, Hivyo unaweza kuuza kwasababu ya mkate ili tu usife na njaa. Inawezekana kabisa kuna mambo unakutana nayo na kuanza kujiuliza wokovu huu unanifaa nini, ni bora kuingia kwenye biashara hiyo au chochote kinachokupatia mkate . Wewe kama Mkristo uliyeokoka unazo haki zako za msingi kabisa lakini yawezekana bado ni mchanga yaani mtoto mdogo, unakuwa bado chini ya uangalizi wa Baba. Unachoitaji ukiwa katika hali kama hii, mwambie Baba naye atakupa mahitaji yako wala atakuacha uzimie na mguu wako autasogezwa kamwe. Mungu atakupa chakula. Bibli inasema wazi katika Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;”

Je?  una ahadi gani kama mwana wa Mungu


1. Mithali 10:6 Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.

2. Zaburi 5:12 Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; Bwana, utamzungushia radhi kama ngao.

3. Mithali 28:1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

4. Mithali 10:24 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.

5. Zaburi 146:8 Bwana huwafumbua macho waliopofuka; Bwana huwainua walioinama; Bwana huwapenda wenye haki;

6. Mithali 13:21 Uovu huwaandamia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema

7. Mithali 14:9 Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki.

8. Zaburi 92:12 Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni

9. Zaburi 37:39 Na wokovu wa wenye haki una Bwana; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.

10. Mithali 15:29 Bwana yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki

11. Mathayo 13:43 Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

12. Mithali 12:3 Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu; Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe.

Unastahili nini ? Kama Mwana wa Mungu.

Kumbukumbu la Torati 28:3-6

1. Unatukuzwa juu ya mataifa ya ulimwenguni.

2. Unabarikiwa mashambani na mijini.

3. Unabarikiwa uzao wa tumbo lako.

4. Unabarikwa uzao wa Nchi yako.


Kumbuka, anayetaka kuzuia kibali chako atapigwa mbele zako,. Watakuja kwa njia moja kuzuia kibali chako lakini Bwana atawatawanya kwa njia saba . Hicho ndicho unachostahili kama Mwana wa Mungu.

Wakati ukiwa kwenye maombi endelea kusoma haki zako ili ujue unachostahili kama mwenye haki, rudia na kurudia katika maombi. Amen.

Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es salaam, Tanzania
Tel: +255 753 230 680 +255 717 538 499

No comments: