MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Tuesday, November 22, 2016

ҜURUDISHΔ MIΔҜΔ ΨΔҜΩ ILIΨΩIβIШΔ



Ną Bıʂɧơ℘ Dąŋƙɬơŋ Rųɖơѷıçƙ RῳɛƙıƖą

📖👉Yoel 2:25-27 "Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.”


Mungu alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli . Israel ilikuwa inapitia katika kipindi kigumu na akasema nao,inawezekana unapitia wakati  mgumu kama wana wa Israeli walivyokuwa wanapitia. Inawezekana mwaka unaisha katika miezi uliyoisha haujazalisha faida . Inawezekana unapitia kipindi cha majini, 💀☠chumaulete, mizimu na kila namna ya mikosi lakini 📖Biblia  inasema hautotayarika kwa jina la Yesu Kristo. Tuko katika kipindi cha maombi , na leo tunaenda kupigana na ufalme huo uliokula mazao yako🦀🦂. Siyo kwamba wana wa Israeli walikuwa ni wavivu walilima lakini mazao yao yaliliwa na wadudu🐜🐞🐌 . Inawezekana hata wewe siyo mvivu lakini wapo nzige na tunutu wamekuja ndiyo maana unafanya kazi lakini fedha💷💶💰 haionekani . Kuna nyakati ambazo Mungu anakemea watoto wake kwa habari za kufanya kazi , lakini nyakati hizi unafanya kazi lakini faida haionekani❗

🎷Wimbo Uliobora 2:15

Nilipopewa neno hili na Mungu au agizo ili sikupewa mahubiri . Mungu alinipa kama lilivyo lije kwako. Kiwango chako cha kuelewa neno hili ndicho kitakachokuvusha kwenda kwenye hatua nyingine. 🚶🏻

Katika maneno ambayo Bwana aliya nena  kutuka katika kinywa cha nabii Yoeli kuna mambo matano ambayo unatakiwa kuyajua.

1⃣KURUDISHA MIAKA YAKO

Kama kuna kurudisha basi maana yake mtu anaweza kupoteza . Maana nyingine ya kurudisha ni kile ulichostahili kuwa nacho lakini shetani ☠amekinyanganya kwako . Kuna watu ambao walistahili kuwa katika kiwango Fulani kihuduma📖,biashashara💵,elimu🎓, ajira na mengine mengi. Maana yake unapokitana na neema ya kurudisha, utaona unaongezeka kwa speed💰isiyokiwa ya kawaida.

Mtazame Yona ambaye alikuwa amemezwa na samaki aliporusishwa, alikwenda kwa speed🏃🏽katika mji wa Linawi, sehemu ya kwenda siku 3⃣ yeye alitumia siku 1⃣ hiyo siyo speed ya kawaida.

Unapoinuliwa na kurudishiwa miaka yako kiburi kisiinuke ndani yako. Tulijifunza kwamba mtu anapokosea nilazima Mungu apitishe kiboko chake. Hapo ndipo adui anaanza uharibifu wa kula miaka yako.

2⃣KULA CHAKULA TELE🍨🌯🍟🍝

Mungu amesema mtakula na kushiba lakini mtakuwa nacho tele . Mungu alijua nzige na madumadu wakija watakula mazao yako, lakini yeye amesema atakapofungua madirisha anasema utakula na kishiba na utakuwa nacho tele . Wakati nasoma neno hili Bwana akanikumbisha wakati nilipitia shida na kukosa hata kikombe cha uji🍵 na akaniambia wapo watu wa namna hiyo na yeye anawatudishia miaka yao iliyoibiwa. Bwana atafanua njia pasipo na 🛤njia .

Nilipokuwa natafakati Bwana akanionyesha habari ya wana wa Israeli kwenye bahari ya shamu🌁.Wakati Mungu anaongea na Musa na kumpa maangizo ya kuvuka bahari wana wa Israeli walishangaa😳, na wakati hii Bwana mwenyewe atakushangaza maana njia zake azichunguziki . Haijalishi kuna ugumu mkubwa kiasi gani.

3⃣KUSHIBA
Kuna kuwa na utele lakini pia kuna kishiba. Kuna watu wanakula chakula lakini miili yao na miyoyo yao aina Amani . Unakula na magonjwa yanaongezeka lakini miaka hii ambayo Mungu anakurejeshea hakutakuwa na udhaifu. Maana ya kishiba ni kuwa na Amani tele. Mtazame Daniel 1:8-15 “*Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi. Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme. Ndipo Danieli akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme*.”Sasa unaweza ukaona siyo habari ya kula chakula kizuri, je umeshiba?.

4⃣KULIHIMIDI JINA LA BWANA🙏🏼

Kuna watu wakishapata utajiri💵🎓💰 tayari wanamuacha Mungu. 📖Biblia inakuambia hata wakati umeshiba na miaka yako imerudishwa bado utalihimidi🙏🏼 jina la Bwana. Utaendelea kistawi lakini kipaumbele chako ni Mungu wako. Kama vile wakati wa njaa ulipolihimidi jina la Bwana ndivyo itakavyokuwa wakati wa shibe . Hii taiona kwa Yusufu ambaye baada ya kuwa waziri mkuu ndugu zake walipokwenda kwaajili ya kutafuta chakula Misri, aliwaambia wasiofu kwasababu ya yale waliomtendea, kwasababu Mungu alimuweka kwa wakati kama ule. Yusufu alilihimidi jina la Bwana. Katika vitu vya kuomba🙏🏼 wakati Mungu anakuinua ni pale unapostawi ili usiache kulihimidi jina la Bwana maana Biblia📖👉 inasema yakufaa nini kupata ulimwengu wote na ukakosa ufalme wa Mbinguni.

Kuna wengine wanajua kistawi ndicho kipimo cha kwenda mbinguni.

5⃣KUTOTAYARIKA
Kutoyarika maana yake kutoeleweka.
Kuna watu wanabaraka lakini awaeleweki;
✔Ndani ya ndoa
✔Familia
✔Kazi
✔Hiduma n.k

Wengine baraka zinapokuja anaondoka. Unakuwa mtu wa kupanda na kuondoka wakati wa mavuno.Ndiyo maana 📖👉Biblia inasema utapanda mavuno na utavuna mwenyewe. Hata kwenye ufalme wa Mungu kuna wengine watatayarika wale ambao umewahubiria parapanda🎷 ikilia wao wanaenda mbinguni. Yule mchawi unayedhani atakosa mbingu ndiye anayeokoka na ni punde tu kabla ya parapanda 🎷kulia,Hautatayarika!!‼

Ndiyo maana Yesu aliwaita mafarisayo Makaburi kwasababu walikiwa wanajua kweli ya Torati walikini wanapotosha watu. “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.” Mathayo 23:27

Unapoongeza maharifa📖 ndiyo unaongeza adhabu zaidi kwasababu unajua siri za Ufalme wa Mungu.

No comments: