MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Thursday, May 28, 2020

VIWANGO VYA KUMTAFUTA MUNGU


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

28th May 2020

Image may contain: 1 person, text

1.    MUNGU ANATAKA UMTAFUTE KWA BIDII
Neno bidii ni nguvu ya ziada kuvuka viwango vya kawaida. Kwenye maisha ya kila siku kuna watu ambao tunatambua kwamba wana bidii kwenye maisha yao. Kwamba kama wanafanya kazi lakini wanaongeza nguvu za ziada za kutafuta. Tunaposema kwa bidii maana yake utoke kwenye viwango vya kawaida na uongeza bidii ya kumtafuta Mungu.

Mithali 8:17  
Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

Wote tunaweza kuomba na wote tunaweza kutoa sadaka lakini kuna nguvu ya ziada ambayo mwingine anaweza kuvuka na kumtafuta Mungu kwa bidii mpaka machozi yanatoka. Watu kama hao wamevuka viwango vya kawaida na kumtafuta Mungu kwa bidii.

Kulikuwepo na wanawake wakitunza nyumba ya Mungu na kufanya utumishi wao lakini Dorcas aliiingia kwenye viwango vingine vya kumtafuta Mungu kwa bidii. Wanawake waliangalia juhudi zake na bidii yake na hata alipokufa walilia na Dorcas alifufuliwa kwasababu ya bidii hiyo. Unapomuendea Mungu kwa bidii lazima aonekane kwenye maisha yako. (Matendo ya Mitume 9:36-43)

Wewe mwenyewe ni shuhuda ulipokuwa unamtafuta Mungu kwa bidii mchana unaomba, usiku unaomba kila muda unaomba kwa bidii namna ulivyomuna Mungu. Hakuna mtu yeyeote ambaye aliwahi kumtafuta Mungu kwa bidii akaacha kumuona. Wote tunampenda Mungu na ndiyo maana unakwenda kwenye ibada lakini kuna wanaotafuta kwa bidii. Hakuna mtu ambaye amefanya bidii asifanikiwe hata kwenye maisha ya kawaida.

Ndiyo maana wakati Yesu akihudumu alitokea mtu mmoja akiumwa na wagonjwa walikuwa wengi sana akiwa kwenye nyumba moja. Wakati wale ndugu wamembeba ndugu yao kwasababu ya bidii ya kumtafuta Yesu walimpitisha ndugu yao darini. (Luka 5:17-20)

Bidii inakutoa kwenye hali ya kawaida na ndiyo maana Ninawi walipoambiwa wanaangamia waliacha kila kitu wakafunga mpaka wanyama wao. Hii ilikuwa bidii kwa maana hakuna ambaye alikuwa anakumbuka mifugo yake wala watoto walikuwa wanamtafuta Mungu kwa bidii. (Yona 3:6-10)

Ukiwa na changamoto kubwa haiwezi kuondoka katika hali ya kawaida bali ni kwa bidii ndipo changamoto inatoweka.

Yesu aliongelea habari ya Kadhi mdhalimu na yule mama ambaye likuwa akimsumbua kila wakati. Alimuendea yule Kadhi  kila siku kwa bidii na maandiko yanasema alipomuendela mara nyingi yule Kadhi alimpa haki yake je si zaidi yako wewe unayemuendea Mungu wa mbingu na Nchi mwenye huruma. (Luka 18:1-8)

Mtu mwenye bidii achoki , kwa hiyo ukisikia hali ya kuomba na kutochoka tayari umeingia kwenye nafasi ya bidii. Si unakumbuka hata wale ambao shuleni walikuwa vichwa kwa maana ya kushika zile nafasi nzuri wakati wengine wamelala wao walikuwa wakisoma kwa bidii.

Zaburi 105:4 
Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake siku zote.

Unapomtaka Mungu ni pamoja na nguvu zake, siyo swala la kuomba siku za ibada tu. Unakuta mtu anaomba ibada hii mpaka ibada nyingine tena. Tunapoongelea Danieli mbona wengine walikuwepo lakini tunaongelea Danieli, tunapoongelea Dorkasi mbona wengine walikuwepo lakini alifufuliwa Dorkasi mwenyewe. Wao walikuwa na kitu cha ziada ndani yao ambacho ni bidii.

Danieli alitoa sadaka ya uhai wake hakujua kwamba atapona kwenye makanwa ya simba lakini alitoa sadaka ya uhai wake. Esta alitoa sadaka ya maisha yake alikuwa tayari kufa lakini wayahudi wasife ndiyo maana tunawasoma. Unapojitoa kikamilifu Mungu hawezi kukaa kimya.

2.    WANAOMTAFUTA MUNGU KWA BIDII  WANAAMUA KUMPA MUNGU MOYO KIKAMILIFU.

Moyo wako ndiyo ambao unakuzuia kwamba umpe Mungu masaa mawili au matatu, moyo wako unaamua kwamba umechoka au la. Ukimpa Mungu moyo wako kila wazo linalopita kwenye moyo wako linakuwa halina upinzani. Kama moyo wako haujamilikiwa na Mungu kwa maana ya ushindani kwa kila jambo linalopita bado haujautoa kikamilifu.

Yeremia 29:13
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Angalia mahali ulipo kuna Zaidi ya mawazo mawili kwa maana unawazo nyumba, unawaza watoto na vitu kama hivyo maana yake umegawanya moyo wako. Kwa hivyo ujampa Mungu moyo wako wote.


No comments: