MUNGU WETU NI MOTO ULAO WAEBRANIA 12:29.

Saturday, October 19, 2019

UTAWALA WA KITI NAMNA AMBAVYO UNAWEZA KUTAWALA KITI AU KUTAWALIWA NA KITI.


Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila

Mwanzo 41:40
Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.

Maana ya kiti ni nafasi ya kiutawala kwenye ulimwengu wa Roho.

Kabla ya wewe kuwa kwenyw ndoa, yenyewe ipo maana yake inasubiria mtu atakayeingia kwenyw nafasi hiyo na kuitwa mwanandoa. Kabla ya kuitwa mkurugenzi nafasi hiyo ipo (kiti) lakini inasubiria mtu atakayekalia kiti hicho.

Kama unatamani nyumba ipo lakini inasubiria mtu atakayetawala eneo na kujenga nyumba. Kwa mfano madhabau hii ilikuwepo kabla ya kuzaliwa sisi siyo kwamba tulipozaliwa na yenyewe ndo ikawepo. Ilikuwepo tangu enzi na enzi.

Ukishatamani kitu ndiyo maana unakuta unaota ndoto. Kwa mfano kiti cha utawala cha Yusufu kilikuwepo kabla ya yeye kuzaliwa. Ndiyo maana Yusufu alipozaliwa alijichunga sana aimtende Mungu dhambi ili asije kupoteza nafasi yake.

Ndiyo maana mtoto akizaliwa unashangaa anaanza kufundisha fundisha na anapokuwa anakuwa mwalimu, alianza tangu kitambo na anapokuwa anaingia kwenyw nafasi yake.

Nafasi yako ipo (kiti)

Haijalishi wachawi wamekuweka wapi ninachojua malaika wa Bwana watakutoa kwenye mapori na kurudi kwenyw nafasi yako na kuikalia. Nafasi ya umasikini siyo ya kwako, nafasi magonjwa siyo yako.

Nami kwa mamlaka ya jina la Yesu ninakuondoa kwenye nafasi ya umasikini, magonjwa na nakupeleka kwenye nafasi yako ya utawala kwa jina la Yesu.

Yesu alipozaliwa akiwa mdogo Mamajusi wa mashariki wakaiona nafasi yake utawala, wakatafuta alipokuwa mtoto na kumsujudia mfalme wa wafalme. Mathayo 2:1-12

Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa nguvu ya kutawala na kutiisha Mwanzo 1:28. Na leo ipo nguvu inakuja kwako kwa jina la Yesu.

 Naongea na watu wanaojua nafasi.....

Mungu ndiye aliyeumba nafasi na akaziweka. Na ndiyo maana Shetani anashindana na nafasi za wana wa Mungu. Kama shetani akiwahi mahali maana yake watu wa Mungu wanatakiwa kupigana ili shetani aachie nafasi zao. Na vile vile wana wa Mungu wanapowahi shetani anapambana kwaajili ya kuwatoa. 1 Yohana 5:4

Mwanzo 41:38-44

Shetani anachofanya akitaka kuwahi nafasi anageuza watu wake wanakuwa na hekima ya dunia hii.

Ili mtu akutawale lazima hajue siri zako na nguvu yako. Ili Yusufu atawale misri Mungu alimfunulia shida ya misri. Kwa kupitia ndoto ya Farao ambao wanganga na wachawi wa Farao walishindwa kutafsiri Yusufu akatafisiri na kuanza kutawala.

Yusufu alipata kibali kila mahali alipokwenda, aliinuliwa kila mahali na alikuwa mtawala. Alipoingia gerezani aliinuliwa na akawatawala wafungwa wenzake.

Usifurahi kuwa mahali na unarudi nyuma kwasababu utatawaliwa. Muombe Mungu akutambulishe mapema. We ujawahi kuona mtu anajitokeza hali na wanamuangalia tu watu wanasema hawezi kukosa Millioni. Ghafla watu wote wananza kumgeukia yeye na anaanza kutawala wengine.

Farao alimtamani Yusufu na kusema apate wapi mtu mwenye akili kama yeye, kwa maana ya kwamba Misri walikuwepo wasiokuwa na akili kama ya Yusufu.

Siyo kwamba Yusufu alivyopewa ile nafasi wamisri wote walifurahi. Walinung'unika lakini walikuwa hawana namna ya kufanya. Siyo kwamba ndoa uliyonayo wanafurahi ni kwamba hawana namna.... Mungu akikuchagua maadui zako hawana NAMNA jiamini kwenye nafasi yako.

Ndugu zake Daudi wanataka kumpinga na ana kiherehere lakini hawakuwa na namna ya kumzuia. Walishaona kwenye ulimwengu wa Roho kwamba Goliathi anakufa wakati wao walipigana naye kwa muda mrefu.

Mungu anapokuinua kuwa mtawala anakupa nguvu ya utawala. Ili utawale mahali lazima ujue mambo. Yusufu alipewa muhuri, pete na mkufu kwaajili ya utawala. Mungu anapokupa utawala kwenye familia Mungu ananza kukuonyesha kwenye ndoto anakupa maono. Usipomsikiliza Mungu baada ya muda unapoteza maono na ile nguvu ya utawala.

Kila mtu juna jambo ambalo mtu amempa lakini ili uweze kukua na kuongezeka kiwango ni namna unavyotendea haki nafasi ambayo unayo ya kawaida. Yusufu alianza kutawala kwenye familia alipokuwa anaona mabaya alikuwa akimuambia Baba yake. Na akashonewa kanzu ambayo ilimtambulisha kanzu pekee kwasababu ya kupendwa na Baba yake.

Sifa ya mtawala ni kutatua changamoto iliyombele. Kama jambo linatokea na wewe hauna suluhisho jua kwamba wewe siyo mtawala.


 Na leo tutaondoa Roho ya hofu. Roho ya hofu inapokaa juu ya mtawala inzuia kufanya maamuzi fulani. 

No comments: