MWEZI WA UFUNUO
Na Bishop Dankton Rudovick Rweikila
9TH October 2019
Leo tunakweda kupokea fungua ambazo zitakuwezesha kufungua malango yako. Kila hatua kuna mlango ambao upo na leo tunapokea ufunuo wa funguo hizo. Iwe ni kwenye elimu kuna mlango, kwenye ndoa kuna mlango, kwenye biashara kuna mlango kila hatua unayopiga kuna mlango.
Mathayo 16:18-19
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Unaweza kuona ni kwanini tulianza na toba, unapofungua duniani na mbinguni wanafungua. Kwa hiyo kama unafungua na hauna uhalali wa kufungua si rahisi kufungua wala kufunga. Maandiko yanasema maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za Bwana kwa hiyo kama hauna msamaha hautaweza kupamba na malango ya kuzimu.
Funguo hizi ni za ufalme wa Mungu.Unapopokea ufunguo wa Mungu na ufalme kuingia ndani yako ndipo unahamuru mambo yaliyoshindikana.
Luka 11:52
Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Yesu anawakemea wakuu wa dini waliokuwa wanafundisha maarifa na kuwaambia watu kuwa alikuwa anawaondolea hekima na maarifa ya Mungu. Ndiyo maana maandiko yanasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa . (Hosea 4:6). Maarifa ya kwanza ni kumpata Mungu mtenda miujiza ndani yako. Ukishampata Mungu aliye ndani yako hakuna utakachokosa kwa jina la Yesu. Ukiwa na Mungu ndani yako hamuangalii mtu mwingine bali Mungu aliye ndani yako. Mungu aliye ndani yako ndiyo anashungulika na maisha yako na ukimkosa Mungu ndani yako na kumpata Mchungaji haikusaidii.
Maandiko yanasema walimleta mgonjwa kwao na wakamuombea yule mgonjwa mwenye pepo bubu hakumtoka yule mgonjwa. Yesu alipofika mahali pale akamfungua yule mgonjwa na akapona na wanafunzi wake wakamuchukua faragha na kumuuliza kwanini wao walishinwa kumtoa yule pepo (Marko 9:14-29). Akawaambia mengine hayatoki ila kwa kufunga na kuomba. Unapofunga na kuomba nguvu inaongezeka ndani yako. Yesu alipofunga siku 40 alipomaliza alijaribiwa na aliposhinda mtihani ule na akapewa malaika wamtumikie. Kila unapofunga elewa kuna mtihani ambao utakusaidia kupanda daraja. Usihesabu mifungo yako bali majaribu yaliyoko mbele yako na namna ulivyoyashinda.
Ufunuo unapojifunua kwako Mungu anakuonyesha mahali pa kupita. Walitokea watu wawili ambao walikuwa na Yesu kwenye msalaba. Wa kwanza alijifananisha na Yesu na kuona kama na yeye amekosa na wa pili akapata ufunuo kwamba hata kama Yesu yuko msalabani anaweza kumuokoa. Na kwa kupitia ufunuo huo Mungu akamuokoa. Luka 23:43
Ufunuo 3:7
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
Kinachotesa walokole wengi hawajui Mungu aliye ndani yao. Wao wanaamini Mungu wa mtumishi au wa madhabahu lakini Mungu aliye ndani yao hawamuamini. Maandiko yanasema Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Yohana 15:7. Kwa hivyo basi kuponywa kwako kunategemeana na Mungu aliye ndani yako. Mungu anahitaji kukaa ndani yako ndiyo maana anasema miili yetu ni hekalu ya Roho Mtakatifu. Yesu akiwa ndani yako unakuwa na funguo lakini akiondoka ndani yako na funguo zinaondoka. Ndiyo maana unaweza kuona viitu vizuri sana na hata kuwa na ujasiri mkubwa sana wakati ukiwa na Yesu lakini akiondoka ndani yako ghafla kila kitu kinastop.
HAKUNA JAMBO LISILOWEZEKANA KAMA UKIWA NA MUNGU NDANI YAKO. Watu wengi sana wako tayari kumpoteza Mungu ndani yao lakini hawako tayari kupoteza mafanikio ndani yao. Wengi huwa wanajiuliza pale mafanikio yanapokuwa yanaondoka lakini Mungu akiondoka hawapati shida.
Unapopoteza fungua tambua na kuanza kutafuta funguo zako. Using'ang'anie kusimama kwenye mlango kwa kuwa hautaweza kujifungua wenyewe pasipo kuwa na funguo.
Shuhuda
Jana nikiwa nyumbani kuna mtu alinipigia simu na akaniambia Mchungaji nimefukuzwa kazi na nimeona maombi yako wenye mtandao na nikasema nikutafute. Baada ya kuongea naye nikamwambia lazima nikuongoze sala ya toba na umepata neema kwasababu tuna siku za maombi na tupo ndani ya siku saba za kuona jambo likitokea. Nikaomba naye na alikuwa analia nikamwambia ndani ya siku saba kuna jambo litatokea. Jumanne jioni akanipigia simu na kusema amerudishwa kazini.
Unapodhamiria ndani yako na kurudisha mahusiano na Mungu wako ninakuambua kwa hakika hizi siku saba za kwanza za maombi haziwezi kukupita. Hizi ni siku saba za kwanza za watu waliomaanisha kwenye maombi.
Endea na maombi haya leo.

No comments:
Post a Comment